FANYA KAZI KWA MUDA NA KWA AKILI


 

Mafanikio ni funguo ya kila mwana wa Mungu ambayo hupewa  katika nchi

zaburi 115:16 “mbigu ni mbingu za bwana bali nchi amewapa wanadamu.”

3yohana 2 “mpenzi ufanikiwe katika mambo yako yote uwe na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo” roho haiwezi kufanikiwa bila akili kufaikiwa tunapaswa kukubali kwamba Mungu ametupa zawadi ya Akili kila mmoja wetu ila kuchukua hatua kuitumia ipasavyo ni jambo lingine ili kuleta matokeo Chanya yeye mvuto katika maisha yetu ya kila siku.

kazi  yeyote hupaswa kujua unachagua  ya namna gani, kwani kuna nguvu kubwa sana ya kuchagua jambo lolote lile, Filemoi 1:14 neno la Mungu linasema “lakini sikutaka kutenda neno lolote isipokuwa kwa shauri lako ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima bali kwa hiari.”

Kundi la kwanza hufanya kazi kwa Muda  – wachache sana duniani na ndio wanaofanya vizuri  kazi hizi, sifa yake kubwa hazihitaji cheti cha shule yeyote zinahitaji kutumia akili mpaka itoe jasho kwa kufikiri kutegeneza wazo na kuliweka wazo kwenye makaratasi  mpaka uone mwisho wake.

Muda hufanya kazi na Akili kadhalika huambatana na  Imani kuona visivyoonekana. Makampuni mengi sana makubwa huhitaji watu katika kundi hili kwa gharama yeyote ile , kwa ajili ya  kufikiri kwenye  kampuni husika.

Yoshua 1:8 “kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako bali yatafakari maneno yake usiku na mchana upate kuangalia sawasawa na  maneno yote yalioandikwa humo maana ndipo utakapoifaikisha njia yako na ndipo utakapostawi sana”

Mungu humpa maelekezo Yoshua juu ya kufanikiwa kwake kuwa kutatokea endapo atajiwekeza katika kufikiri kupitia kitabu cha torati  ,nikuulize mtu wa Mungu huwa unasomaga nini na huwa unatafakari nini ?  kuwa mtu wa kufanya kazi za Akili kwa muda humaanisha kutafuta taarifa kusoma vitabu vitakavyoongeza ufahamu na maarifa maishani mwako na kitabu cha kwanza kabisa kama kweli unahitaji mabadiliko ya uwezo wa kufikiri wa Akili yako ni BIBILIA ,hichi ndio kitabu tu ambacho kitakupa maarifa sahihi yenye ukweli na uhai ndani ya nafsi yako.

Mtu mmoja akasema kuwa bibilia ni kitabu cha zamani chenye taarifa mpya ni bayana haswaa kuwa  hakuna kitu chochote utakachokihitaji leo kukifanya hakijawekwa kwenye maandishi ya bibilia. Muhubiri 1:9” yaliyokuwako ndio yatakayokuwako na yaliyotendeka ndio yatakayotendeka wala  jambo jipya hakuna chini ya jua”

Hivyo neno la Mungu ndio dira sahihi katika maisha ya kila mtu  katika kundi la watu  wachache duniani, tunapowasikia wanasayansi na wagunduzi wakubwa duniani walikiwa ni wasomaji wa neno la Mungu kama mtindo wao wa maisha. Mfano aliyegundua mambo ya internet alitizama mfumo wa roho mtakatifu anavyofanya kazi aliyegundua ndege ya abiria alipata ufunuo kutoka kwa njiwa ,aliyeanzisha majeshi alipata ufunuo kutoka kwenye siafu, alitengeneza basi la abiria alipata ufunuo kutoka kwenye mdudu jongoo. Na vyote hivi Mungu alishamaliza uumbaji hivyo hakuna budi kutambua kuwa chochote kile unachokiona duniani Mungu ametupa upendeleo wa kuvitumia na ili tufuate maelekezo tunarudi kwenye neno lake

Zaburi 24:1 “Nchi na vyote vijazavyo ni mali ya bwana ,dunia na wote wakaao ndani yake”

Kila mtu anapaswa apitie katiba ya maisha yake apate maelekezo ya kufanya kutoka kwenye neno la Mungu.

Kazi za mikono. Zinatumia Imani ya cheti na wako wengi sana na huelekwa kwa ajili ya mshahara na unalipwa kwa mafungu siku  30 na hutumia Akili asilimia ndogo sana eneo kubwa wanalotumia sana ni eneo la kumbukumbu.

Huwezi kuuona muda huwezi ukaiona Imani hivyo vitu ambavyo havionekani vina nguvu sana.

Kazi yetote ya muda inafanya kazi na imani

Kazi yeyote ya mikono mtu anafanya kazi ili apate mshahara.

Kazi yeyote utakayofanya  ukatokwa na jasho hiyo ni laana.

Kuna jasho la kazi ya jasho la mwili na kuna jasho la kazi ya Akili                                                        mathayo 11:28-30 “njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo name nitawapumzisha, jitieni nira yangu mjifunze kwangu kwakuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapata raha nafsini mwenu, kwakuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi”.   

Jasho la Akili linatoka kuanzia saa 7 usiku mpaka 11 asubuhi .

Kazi za Akili hazihitaji cheti zinahitaji uangalie ni nani anafanya vizuri na hicho kitu kiwe cha Mungu kwani unavyotamani chochote kile cha mtu ile roho ya kile kitu kinakuvaa hivyo  usitamani mali ya mtu mwovu

Maisha ni mtihani wa kuchagua kwani  hakuna mtu wa kukuchagulia kazi filemoni 1;14 kumbukumbu la torati 30:19

Jifunze kumuuliza Mugu amekuleta duniani kufanya kitu gani. Mungu atakuoyeshea mtu mwenye Akili aliye na uwezo wa kukupatia kitu kwa njia ya muingizio ukae naye na kile kitu chenye upungufu kwako kinakamilishwa nawe unaanza kukifanya mwenyewe vizuri mfano , Musa na Haruni, Musa alikuwa na kigugumizi hawezi kuongea vizuri

Mungu akamwambia akae na Haruni mpaka akaweza kuongea vizuri kadhalika wanafunzi wa Yesu hawakwenda shule yeyote lakini wakiwa na hekima na ujasiri wa kushangaza kwa kuwa walitembea pamoja na Yesu  matendo 4:13 “Basi walipoona Ujasiri wa Petro na Yohana na kuwajua kuwa ni watu wasio na Elimu wasio na maarifa wakastaajabu wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.”

Kwani roho dhaifu ikiambatana na roho ya kiungu ile roho chafu inakimbizwa na inaondoka.

Ukiona mtu ana roho ya Mungu ndani yake unayoihitaji kaa naye unapata ile roho na ile kazi pia, ukubali kulipa gharama ya utii na kutambua dira ya unapoelekea inakuwa kazi kwenye maisha yako.

Tambua kuwa hichi ni kipindi cha neema unaweza kufanya jambo lolote lile unalolipenda kwa moyo wako wote na akili zote kwa kutoa muda wako kujifunza hicho kitu na kuweka bidii katika kitu hicho kimoja mpaka kiwe kazi kwa kutoa muda mrefu wa kufanya mazoezi na kuamini mawazo yako kwani Imani kwenye jambo lolote huambatana na kurudia na kurudia mara nyingi Zaidi.

Tafuta mtu mwenye kufanay kitu ambacho unakipenda kaa hapo jifunze kitakuwa chako.

Usisahau kulike page yetu.

Kama una swali lolote, una changamoto , una mauza uza mengi, hujui pa kuanzia, tutafute, uliza hapo kuna sehemu ya meseji,  Hakuna kitu kizuri ambacho kitakuijia ukiwa umelala

Subscribe.

Previous MAAGANO AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUWABARIKI WATU WAKE
Next MAJUKWAA YA TAARIFA SAHIHI (PLATFORM OF INFORMATION)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.