FIKIRI MABADILIKO  (THINK FOR CHANGE)


4840A5BE-6969-42F7-8C7F-35676233A7FB FIKIRI MABADILIKO  (THINK FOR CHANGE)

Kubadilika ni kugeuka, kuacha kufikiri mambo ya zamani na kufikiri upya, kuacha kufuata mambo yasiofaa na  kufanywa upya ndani ya akili yako, ili uweze kutambua mapenzi ya Mungu aliyokuandalia ya kupendeza na ukamilifu.

Kubadilika ni kutubu, na kumrejea Mungu.  Unapofikiria mabadiliko, fikiri vizuri (positive).  Wewe unafikiri nini?

Kitu ambacho unakuwa unafikiria kufanyia kazi kesho, fanyia kazi leo. Kufikiri vizuri ni kufanya kitu kwa wakati , usiseme nitaanza kesho, anza leo.

Badiliko la mtu yeyote linaanzia kwenye akili  ya mtu. Kuna mambo mawili ya kuangalia  kwa umakini ,  unafikiri nini,  kutumika kwanza  au unaangalia utalipwa kitu gani kama ukifanya kazi.

1.Kufikiri pesa

2.Kufikiri kujitolea

kufikiri kubadilika anza kufikiri kujitolea.  Ukifikiri pesa utakutana na pesa za muda mfupi na ni kidogo sana. Hazikithi mahitaji yako, matokeo yake utaanza kuingia kwenye vikoba, mabenki mbalimbali.

Ukifikiri kujitolea utakutana na Mungu, ukikutana na mwenye vyote atakupa kila kitu, pesa, afya, upendo, furaha, amani,  na utakuwa ni mwenye haki, hapo utaanza kuishi kama wengine ndani ya ufalme wa Mungu.

Anza kufikiri kupoteza kwanza kabla ya kufikiri kupata. Mbegu yeyote ni lazima ikae chini ioze kwanza ndipo itakuletea mazao mengi, lakini ikibaki vilevile , hakuna ongezeko. Ni lazima ufikiri kupoteza kwanza ndio utapata.

Ukikaa chini  na kujiuliza kwa nini hufanikiwi, utapata jibu , huenda unafikiri kupata kila wakati, hufikiri kupoteza kwanza.

Kuna vitu vya muhimu ambavyo unatakiwa kuviona kila unapofikiri kufanya kitu.

Fungu la kumi

Mbegu

Ukarimu

Wazazi

Kuwekeza

Ukikubali kupoteza kwanza katika vitu hivyo hapo juu lazima utavuna vya kutosha, kusukwa sukwa na kushindiliwa, hutapungukiwa , hutaona taabu ya maisha, kinachowatesa watu wengine hakitakutesa wewe.

Jiulize je kila siku katika maisha yako kuna kitu chochote cha Mungu unakifanya? Mambo hayaendi kwa kuwa kipo kitu unakosea. Neno la Mungu linasema amelaaniwa mtu afanyaye kazi ya Mungu kwa ulegevu. Yeremia 48:10.

Heri mtu Yule aonae Hekima . Una masaa 24 kila siku  unafanyia nini muda wako. Mungu habariki mtu mjinga hata siku moja,  mtu ambaye hataki kufuata kanuni  zilizopo, anataka vitu vya fasta. Mtu ambaye hataki kufikiri kubadilika.

Ndio maana mahali ambapo utaona majani yamekauka, miti haistawi, mito haitoi maji,   watu wa sehemu hio hawana furaha. Wamekataa badiliko. Ni wagumu wa mioyo. Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii.

Watu hawa  hawataweza kuona mambo ambayo Mungu amewaandalia , kwa sababu ya kukataa kubadilika. Kuanza kumpenda Mungu ni kuanza kubadilika katika  kutubu kwako.  Fomula ya kwanza ya kila mtu anayetaka kubadilika ni kuingia kwenye TOBA.

Zaburi 51:1-19,  zaburi 103:3. kwa kumaanisha. acahana na kutubu kwa jumla, Nenda mbele za Mungu peke yako. wewe mwenyewe kwa akili yako.  Tengeneza madhabahu yako , rejea somo la maandalizi utapata maelezpo zaidi.

Subscribe  kupata makala mpya.

Previous MAANDALIZI (PREPARATION)
Next MLANGO WA IMANI UMEFUNGULIWA KWA AJILI YAKO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.