Fomula Ya Maisha. Ni Muhimu


love-God-1024x768 Fomula Ya Maisha. Ni Muhimu

Watu wengi wanafikiri  kwamba  maisha hayana fomula , sio kweli.

Maisha yana fomula yake. Ukitaka uwe tofauti na ulivyo sasa, ni lazima uifahamu fomula ya maisha.

Neno la Mungu liko wazi kabisa , Mpende Bwana Mungu wako Kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, kwa nguvu zako zote na kwa roho yako yote. Mpende jirani yako kama nafsi yako.

Hakuna fomula inayopita hii.  Ukikosa fomula hii utapoteza muda mwingi na kupoteza maisha yako yote.

Ukinunua simu utapata na kitabu chake, yaani menu yake. Mwanadamu pia ana kitabu chake, menu yake ni neno la Mungu, Biblia.

Watu wanalazimisha maisha bila fomula. Watu wajinga wasiotaka kujifunza hawana fomula. Mtu asijidanganye mwenyewe kuwa ni mwenye hekima Dunia hii kwa kufuata Elimu ya Dunia peke yake. Bora awe mpumbavu ili apate kuwa mwenye Hekima ya Mungu. Maana hekima ya Dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu.

Mungu hawezi kumpa mtu mjinga pesa, kwa kuwa pesa hio itamuua. Pesa ambayo umewahi kuishika  inalingana na kiwango cha akili yako .

Sasa jiulize leo hii, unawezaje kuongezeka kama hauna fomula ya maisha?

Anza kuangalia mazingira yako , unamiliki gari nzuri, nyumba nzuri, smartphone, mke au mume mzuri, watoto au watoto na vitu vingine vingi tu, lakini huna kitabu chako cha Imani. Huna  dayari, huandiki mafundisho  ya neno la Mungu , Unakutana na changamoto kadhaa katikati ya maisha yako.  Mungu hapo atakusaidiaje?

Umeoa umelipia gharama mwanamke milioni na zaidi , lakini umeshindwa kununua Biblia  shilingi 25. Ndoa inaenda hovyo. Hapo Mungu atakusaidia vipi?

Stuka basi, anza kufikiri  ili kiwango chako cha akili kiongezeke. Unaenda kwenye mafunzo huandiki, wakati wewe ni mjinga, na unafahamu kabisa kuwa ujinga wako uko wapi. Husomi vitabu na huendi semina, utatokaje?

Ndio maana Yesu alilia kwa ajili ya watu wasio na akili, watu wajinga. Akasema laiti hawa watu wangejua kuwa hawana maarifa ya neno la Mungu. Ndicho ulichokosa. Maarifa ya neno la Mungu. Fomula ya maisha umeikosa. Watu wangu wameangamizwa kwa kukosa maarifa.

Kanuni nyingine kubwa  ni hii. Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo. Maana hio ndio torati na manabii.

Ukiona watu wanakufanyia vibaya wewe ndio uliyewafanyia hivyo, hapo unavuna ulichopanda, umekaribisha mwenyewe. Msidanganyike Mungu hazihakiwi , kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Kanuni ni Kumpenda Mungu. Weka thamani yako kwa Mungu, Kipaumbele chako kiwe ni Mungu kwanza. Maisha yanafuata baada. Fomula ya kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na Haki yake.

Iko hivi.

Ukimpenda Mungu utatumia muda wako vizuri katika kufanya kazi za imani. Kazi za imani ni kama zifuatazo.

Kazi za Yesu ni kuhusiana na watu, injili, kwenda kwa watoto yatima , wajane wafungwa, wazee na kuwatembelea wagonjwa na kuwaombea. Kufanya usafi na kuwafulia nguo watoto yatima na kuwasaidia kama unao uwezo wa kununua chochote, chakula, nguo, mahitaji yote ya mahali wanapoishi. Kama huna pesa toa muda wako tu.  Utampendeza Mungu. Hii ni fomula.

Kazi ya Adamu ni usafi wa mazingira. Safisha bustani yako ya Edeni ili ikupatie Baraka. Edeni yako ni mahali ulipo sasa, kama ni Mwanza, Arusha, Dar, Dodoma, Nairobi, Kampala, , Kigali na kwingine kote ulipo unayesoma makala hii. Usitupe takataka ovyo, wala usiwe mmoja wa watu wanaokojoa kila mahali, hasa wanaume, msichafue  ardhi, unachafua akili na ufahamu wako. Funguka kwa kufanya usafi.

Unganisha imani yako na neno la Mungu.

Yakobo 1:27  neno linasema, Dini iliyo safi mbele za Mungu baba ni hii,kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao,na kujilinda na Dunia pasipo mawaa. 

Mathayo 25:35-46  Neno linasema kwa maana nalikuwa na njaa mkanipa chakula,nalikuwa na kiu mkaninywesha,nalikuwa mgeni mkanikaribisha,nalikuwa uchi mkanivika, nalikuwa mgonjwa mkaja kunitazama, nalikuwa kifungoni mkanijia.,

Mwanzo 2:15  Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu , akamweka katika bustani ya Edeni ailime na kuitunza.

Mathayo 28:16-20. Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la baba na mwana na Roho mtakatifu…

Mungu atakupa Kazi, Ndoto yako, Maono yako, Biashara Yako, Maisha yatakuwa mazuri.

Lazima ujipange mapema, hujachelewa maadamu bado uko hai. Fuata kanuni hii utaona matokeo mazuri. Usiwe kama watu wasio na hekima bali kama mwenye hekima ukiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Anza kumthamini Mungu. Mpe Mungu kipaumbele kwenye kila kitu chako. Mshukuru Mungu kwa kila kitu. Usiwe mtu wa kulalamika, kunyoshea watu vidole,  kusema serikali , kumsema raisi,  acha!!.

Weka akili yako mezani. Usipende kuweka ugali tu  mezani kwako. Hakikisha akili yako inatokwa jasho sio mwili utoe jasho kila siku.

Fuata fomula ya maisha utafanikiwa.

Subscribe.

Previous Kuwa Single Sio Laana Wala Ugonjwa , Twende Tuone.
Next MAOMBI YA UKOMBOZI WA NAFSI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.