Fundisha Akili Yako Maarifa Na Ukue Kwa Furaha


6456550 - senior couple putting on in line skates in park
agingwellseniorcouple-1024x683 Fundisha Akili Yako Maarifa Na Ukue Kwa Furaha
mazoezi yanasaidia kutunza akili

Unawezaje kujizuia kuwa na mawazo mabaya ili kuishi ukiwa na mawazo mazuri?

Kustaafu. Mjomba wangu  hakutegemea  kuwa na mzigo wa akili  ambao uliambatana na kukosa kazi.

Siku kwa siku alisema, Nina muda mwingi wa kuwa huru. Akili yangu haiko kwenye hali nzuri.  Siwezi kuacha kufikiria sana na  makosa yangu  yaliopita  yameanza kunirudia.

Kama hukuwahi kuajiriwa na hukuwahi kuwa na mambo mengi ya kufanya, Au umewahi kuwa mgonjwa , huenda ukawa unaelewa hali niliyo nayo.

Umetambua hali ambayo mjomba wangu alikuwa nayo , akili ilikuwa inafanya kazi zaidi  katika kuchukua hisia zote mbaya.  Kila mawazo  yaliokuja hayakuwa mazuri. hakuweza kuyathibiti, yalibaki ndani yake.  yalikuwa  yanazidi kuwa mabaya na kumletea hisia za zenye matatizo.

Kuwa na umri mkubwa ina maana, lakini watu wengi hawana muda wa  kukuza akili.  Akili inakuwa rahisi kukumbuka mambo yaliopita zaidi kuliko yaliopo, kujilaumu kwingi na woga unazidi kuwa na nguvu.

Unazo mbinu ambazo zitakuwezesha kutunza akili yako iwe na hali nzuri?

Kama umestaafu na hukuwa mtu wa kutafuta maarifa , huwezi kwenda kuishi vizuri, ni kwenda kuteseka kwa sababu  hutakuwa na kitu endelevu katika maisha yako. Na kwa sababu hio hutaweza kuwa na furaha.

Wewe sio mtu pekee ambaye umekuwa huna furaha , maisha yako yana mchanganyiko  wa furaha na  mafanikio yasiodumu, una hisia mbaya, mahusiano yako sio mazuri, au kushindwa na kupoteza nafasi, kuwa na wivu  ni kawaida katika maisha ya watu wengi.

Unaweza Kuachana Na Kumbukumbu mbaya?

Unaingiza hisia mbaya kuhusu maisha ya baadae na unachanganyikiwa?

Umri mkubwa  unaweza kuleta stress kubwa, Hasa umri wa miaka 60. Kuna changamoto nyingi kama magonjwa na hasa kama hukupata wazo mapema la kumtumikia Mungu . Uliendelea na maisha yako mabaya toka ujana wako, na sasa unajiona  kutengwa na jamii, kuhitaji msaada zaidi, kuhitaji mtu wa kukujali.

Watu wenye umri mkubwa hawatakiwi kuwa na stress,  huzuni. kama wangekuwa wamejiandaa mapema , wangeweza kukua wakiwa na furaha badala ya kuhangaika na mambo magumu.

Lakini hutaweza kuwa na uhuru wa akili.  kwa sababu akili yako ni chombo ambacho ulitakiwa kutunza, kukifanyia  service. Sio njia zingine.

Unawezaje kutunza akili yako isiwaze mambo mabaya, badala yake iwe inawaza mambo mazuri.

Kumbuka kuwa Hakuna umri ambao unaweza kukuzuia  kufungua uwezo wa akili yako. Unaweza  kuwasha taa yako  na ukaanza kuishi vizuri bila ya stress na huzuni nyingi sasa hivi. Kumbuka Imani ni sasa.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

Previous ''Kama'' Ni Neno Ambalo Limetumiwa Upande Wa Mwanadamu Sio Wa Mungu
Next Anza Wiki Kwa Kuboresha Kazi Zako Na Hali Ya Akili Yako

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.