Hawa Ndio Wasichana Wenye Moyo Wa Imani


ab3e4d8a174bda5bfbbf7226ec02fde4-dreads-black-girl-faux-dreadlocks Hawa Ndio Wasichana Wenye Moyo Wa Imani

Wasichana wenye moyo wa imani hujaribu kuwa bora kila wakati haijalishi ni hali ya aina gani. Wanaweza wasiwe sahihi, lakini wana uwezo wa kufanya  wawezavyo .

Wakati wowote unapohitaji  msaada, wataweza kuonekana. Wakati wowote unapohitaji mtu wa  kuongea naye, watakusikiliza. Wakati wowote unahitaji kujisikia vizuri, umekwazika na kitu fulani , watakukumbatia kwa karibu na utalia mikononi mwao.

Wasichana wenye moyo wa imani watatafuta njia ya kukufanya utabasamu. Wanaweza kujitolea furaha yao  ili wewe upate furaha.

Bila shaka, wasichana kama hawa hawapatikani kwa urahisi.  Sio watu rahisi, Wana mambo yao wanayoshughulikia ,Lakini kama utampata utaona utayari wake kila unapohitaji msaada kutoka kwao. Wako bussy, Lakini bado watatafuta muda wa kukuona. Wanaweza kuwa waliumizwa kabla, lakini bado wamefungua moyo wao kwako.

sam Hawa Ndio Wasichana Wenye Moyo Wa Imani

Wanaweza wasiwe marafiki sahihi, Lakini watajaribu kwa nguvu zao  kurekebisha makosa wanayofanya. Hata wakiwa katika moody mbaya bado  watakuonyesha na kukuomba msamaha, watawajibika kwa hilo walilofanya.  kama utaona hawakujibu meseji  au kupokea simu, watajua kuwa  wanahitaji kutafuta muda  ili uweze kuelewa kwa nini hawakufanya hivyo ili kukuhakikishia kuwa wanakuthamini.

Wasichana wa aina hii wako mbali sana na usahihi. Lakini wana  uwezo wa kukufanya utabasamu. Wanaweza kuplan kitu ambacho utakifurahia. Watafanya kila kitu ambacho utakifurahia. Watakwenda zaidi ya unachokiamini ili ujisikie vizuri.

Wasichana wa aina hii wanafahamu jinsi ilivyo taabu kuwa mpweke na kusahauliwa na hawatahitaji kukuona wewe unajisikia hivyo. Watakufanya ujisikie kuwa ni rahisi kupenda.Kama vile unastahili kupata upendo. Hawapendi uwe na mashaka tena.

Wasichana wenye moyo wa Imani wanatambua kutokukamilika kwao, Lakini wanajitahidi kujirekebisha.Hawana Wivu hata wanapokuona upo na wasichana wengine wazuri kuliko wao. Hawapendi ugomvi.

Wanajaribu kuwa marafiki bora iwezekanavyo. Lakini wakati mwingine hukasirika , kwa sababu ni wanadamu bado. Wakati kwa wakati bado wanakosea.

Wasichana wenye moyo wa imani huona ubora ndani ya wengine.  Kwa hio wanatumaini kwamba utaweza kuona ubora ulipo ndani yao pia. Wanatumaini kwamba utawasamehe wanapokuwa wamefanya makosa,  Kwamba utaelewa wanapokuwa wamekasirika,  kwamba utakuwa  mwema pale wanapokuwa wameanguka.

Wasichana wenye moyo wa Imani wanajaribu  kuwa bora. Na wanategemea na wewe kufanya vile vile.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Njia Ya Kuzia UTI ( Usiwe Na maumivu Wakati Wa Sex)
Next Utajuaje Kama Utadumu Na Mwenza Uliyenaye

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.