Hii Ni Njia Sahihi Ya Kupunguza Uzito Wako


1-2 Hii Ni Njia Sahihi Ya Kupunguza Uzito Wako

Zaidi na zaidi tunajifunza kila siku kuhusu kupunguza uzito, sio tu katika mazoezi na kupunguza calories.

Tunapozingitia mwili wa mwanadamu kwa ujumla na kuelewa  umuhimu wake, tunaweza kuamua  kwamba tunachokiona kwenye kipimo ni namba ndogo kuliko kinachoendelea ndani ya miili yetu.

Hii ni kwa habari zote nzuri na mbaya. Kwa msaada mwingine , tunapohangaikia uzito  wetu,  hatutakiwi kuona ugumu ; kutunza uzito sio tu katika nidhamu na kujidhibiti. kwa upande mwingine, ina maana kwamba ili kufikia uzito wa kufurahisha na kubaki nao huo uzito ,  inabidi kufanya kazi ya kutosha ili kuiponya  mifumo wa  miili yetu kuanzia ndani.

Kwa kushughulikia matumbo yetu, hormoni zetu, kiasi cha sukari. Kuacha dhambi. kujifunza kutumia muda vizuri kuliko kupoteza muda kutazama TV, instagram, Facebook na mitandao mingine. Badala yake tuwe na utaratibu wa kujisomea kwa bidii, Hasa vitabu vya Hekima kama Biblia, Kurani, na vingine. Vitabu vya wenye hekima. Kutafuta maarifa .

Kama hujui kazi ya MUDA ngoja nikuambie leo. Ukifuata utapunguza uzito wako kwa urahisi bila ya ugumu wowote. Kazi ya muda ni

1.Kufikiri – THINK

2.Mawazo au Fikra- IDEAS

3.Kutafuta Taarifa Sahihi — INFORMATION

Kazi ya pesa  ni kukokoa muda sio za kutumia kwenye Chips Kuku,Pombe, Nyama choma, Ugali mkubwa, Nyama choma nyingi,  vyakula vilivyotunzwa kwenye makopo. Tumia pesa katika kutafuta taarifa sahihi, kununua CD za magunzo mazuri. vitabu vya wenye Hekima, sikiliza Video zenye msukumo .

Anza kupunguza uzito wako leo, hapa nakuambia kwa nini

stock-photo-handsome-young-woman-in-pajamas-with-cup-of-tea-sitting-on-floor-709347067-1024x752 Hii Ni Njia Sahihi Ya Kupunguza Uzito Wako

1.Itasaidia afya ya utumbo wako.

Unapojiona unaongezeka uzito ni kwa sababu machine yako haifanyi kazi vizuri, Imezidiwa na kiwango cha vyakula unavyokula, kwa nini? Kwa sababu hata bacteria waliopo ndani  ambao husaidia uweze kupata choo, hawana afya ya kutosha  kwa kuwa umewazidishia kazi yao. hawapati muda wa kupumzika.

2.Inasawazisha Sukari ya damu

Ni ngumu na Sio rahisi kupunguza  sukari inapokuwa imeingia ndani ya mwili wako, unapokuwa na presha, kuumwa mgongo, miguu, kiuno. Lakini kama ukiwa mtu wa kutumia muda vizuri hutaweza kukutana na magonjwa haya kwa sababu wewe utakuwa ni mtu wa kupigana na UJINGA sio mtu wa Kupigana na Umasikini.

Ukipigana na ujinga ,huwezi kukutana na magonjwa kama hayo hapo juu, hutaweza kuwa na uzito mkubwa, utautoa wapi ikiwa uko bize . Ugonjwa utaingiaje kwa mtu aliye bize kutafuta taarifa nzuri, anayekaa kufikiria na kuandika mawazo yake na kuchora  ramani ya matarajio yake.Anafikiria atawasaidiaje wengine kupiga hatua hapo walipo. Ni wapi ugonjwa utamkuta mtu kama huyu? ni wapi ataweza kuwa na uzito mkubwa?

3.Itaondoa njaa Isio na sababu. 

Siku hizi vyakula vipo kila mahali. Tena vinaonyeshwa kwa nje ,  vinavutia macho na kuongeza hamu ya kutaka kula. kwa maneno mengine, Ubongo wetu umeshambuliwa na ladha ya vitu vitamu kila mtaa unaopita, inarahisisha dalili za njaa kuanza kwenye akili zetu. Kwa hio watu wanashindwa kuelewa kama ni njaa au sio hali ya njaa bali ni tamaa ya macho na kushambuliwa kwa ubongo.

Usipopangilia masaa yako vizuri , hutaweza kupunguza uzito ulionao. Dawa kubwa ya kupunguza uzito wako ni kujua kutumia muda wako vizuri. Usiwe mtu wa kukaa muda mrefu bila ya kufanya kitu chochote. Anza leo kupunguza muda wa kukaa kijiweni kuongea habari za mpira, acha kukaa barazani kuongea umbea, acha kukaa kwenye Tv muda mrefu kutazama movies. Badala yake soma vitabu, nenda kwenye seminar mbalimbali, tafuta makala nzuri jifunze kupigana na ujinga. Acha kupigana na umaskini.  Hutaweza kusikia njaa hovyo hovyo kama utafanya hivi vitu .

Tafuta picha ambayo unatamani uwe  kama hio. au mtafute mtu akuchoree picha ya umbo unalolitaka , halafu tundika juu, mahali ambapo kila wakati utakuwa unaangalia hio picha, Na ndivyo utakavyokuwa.  Haijalishi uko umri gani, hakuna kisichowezekana. Jump anza kuondoa uzito ulionao kwa kutumia njia hizo zote nilizokupa. Fanya kwa imani bila ya kuwa na shaka wala hofu . jiwekee malengo.

Nina maana gani hasa katika kukuambia hivyo. Bila ya kutumia Muda vizuri , utajikuta umebakiwa na muda wa kutibu magonjwa yasiopona kutokana na uzito ulionao. Lakini nina habari njema. Hata kama umefikia uzito ambao unakukatisha tamaa, usiogope. Rudi nyuma huko ulikoelekea umeenda mbali. Mrudie Mungu sawasawa. Acha dhambi.Kwa nini nasema hivyo, kwa sababu kama unafanya dhambi yoyote unayoijua , au kama unapenda kitu fulani na huwezi kuacha. hivyo vitu vinageuka na kuwa magonjwa.Ukiacha dhambi utakula vyakula vizuri. Utalala usingizi kama mtoto mdogo. wala hutalala masaa mengi, maana utaona unapoteza muda.

Nina mengi ya kukuambia lakini najua wewe ni mvivu wa kusoma. ngoja niishie hapa . hata hivyo Mungu akukumbuke kwa kusoma kwako. Anza kumsuhukuru Mungu kila baada ya dakika 60. Mungu anapatikana mwanzo wa lisaa. Mkumbuke Mungu, Mshukuru Mungu, Msifu Mungu.Atakufanyia wepesi wa maamuzi yako.

Subscribe kupata makala mpya.

 

Previous Acha Mambo 18 Ya Kuomba Omba Radhi Katika Mwaka 2018
Next Tofauti Kati Ya Uongozi Wa Kiungu Na Mwanadamu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.