Hivi Ni Kwa Nini Mungu?


Mungu hubadili mioyo iliovunjika, katika miujiza yake ya mbinguni, upande mwingi  na upande mwingine, amefanya kwangu hata kwako atafanya na zaidi ya  unavyofikiri.

11596-10296-woman-crying-looking-up-big.1200w.tn_-1024x512 Hivi Ni Kwa Nini Mungu?

Nafsi iliofungwa.

Alikuwepo kaka mmoja muda mrefu alikuwa na matatizo ndani ya moyo wake, na alikuwa na maumivu kwenye mguu wake kuanzia magotini  mpaka kwenye unyoya, na haikuwa maisha  yake ilitokea tu.

unafikiria mbali, jali mambo yako.

Na baadae utatoka wapi sijui, imetokea kwenye maisha yako, umefungwa nafsi,  ni huruma sana.

KWA NINI?.

Kwa nini magonjwa?. kwa nini njaa, kwa nini matatizo ya akili?, kwa nini kuhangaika ?,kwa nini ndoa zinaharibika?, kwa nini huduma zinaanguka?, kwa nini kifo?, kwa nini usumbufu?, kwa nini madawa ya kulevya? kwa nini mashimo?.

Ni sawa sisi kuuliza kwa nini?

Mfalme Daudi alifanya.

Kwa nini wewe uwe mbali na mungu?

Ayubu alifanya. hivyo

alisema nitasema kwa mungu, msinilaani, nionyesheni kwa nini mnashindana nami?

Hata Yesu alisema, wakati alipotundikwa   msalabani,

Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?

Yesu aliuliza kwa nini, kwa sababu alikuwa msalabani, na alikuwa ni mungu kamili,  na upande mwingine ni mwanadamu kamili. katika ubinadamu alihisi uzito wa maovu yetu na yalimtenga na Mungu baba  kwa mara ya kwanza, Alilia kwa nini?

Tunauliza kwa nini kwa sababu sisi ni wanadamu, tumefungwa hatuoni njia , tunataka kuona sababu, tunataka kuondoa mawazo mabaya yaliopo kichwani mwetu, na kuweka mawazo mazuri. tunajaribu kuangalia tatizo na madhara, labda hio ni njia yetu.

Ukweli ni kwamba hatuna kithibiti cha kutuonyesha ili kujua kwa nini kule upande mwingine wa mbinguni.

Bado naendelea kuuliza kwa nini, Uliza kwa nini bado tunachochea kusikiliza  na wakati hatuelewi kwa nini?

Uwe makini usikwame pale.

KUKWAMA

Nakumbuka rafiki yangu mmoja alikuwa ni mzuri  sana, lakini siku moja aligundulika kuwa anatumia madawa ya kulevya., swali hili la kwa nini lilibaki ndani ya ulimi wangu. lakini yeye alisema oh dia  bado unajiuliza kwa nini? basi niliganda, na yeye alilijua hilo.

Baada ya muda rafiki yangu mwingine aliolewa na ni muda mfupi sana ulipita, mara akapoteza mume wake. nilizidi kujiuliza zaidi kwa nini. kumbe nilikuwa ndani ya shimo sielewi kinachotokea kule juu.

Ni kama vile mahabusu anapokuwa ndani ya selo, maisha yake  yanazoea huko, hajui upande mwingine kunaendelea nini.tunapoendelea kukaa shimoni kwa  kuchagua au kulazimishwa na matukio, ndio hapo Adui anapokufanya uamini kuwa hakuna tumaini na kuona kuwa hakuna njia ya kutoka shimoni.

Mwenye hekima mmoja alisema, huwezi kupata majibu ukiwa kwenye tatizo.

Kwa hio kwa nini tunafanya hivi?

matatizo yetu yametukaba shingo, tusiache  yatuangushe. lakini tukizidi kuyafungia macho tutaangusha treni yetu.

Miaka mingi nilikuwa na matatizo ya mgongo, nilishindwa kuelewa hilo tatizo ni nini hasa , nilitembea  hospitali mara nyingi kwa ajili tya mazoezi sikufanikiwa , nilivaa mkanda kama nilivyoshauriwa na madaktari , lakini haikusaidia. sikuwa naweza kusimama muda mrefu, dakika mbili ni nyingi sana.

Nashukuru mungu nilishinda, nilijitahidi kusimama kwa muda mrefu kwa imani , tena bila mkanda, na nikaacha kwenda hospitali. hapa ndipo nilipoweza kutoka ndani ya shimo.

Tunatakiwa kumwona Mungu katika tatizo , simama anza kwenda bila woga.

BADILIKA.

Ni wakati wa kubadilika.

Daudi alifanya baada ya kuuliza kwa nini, akasema bado nitamtukuza Mungu.

Ayubu alifanya baada ya kuuliza kwa nini, akasema, bado nitamwamini Mungu.

Yesu alifanya  baada ya kuuliza kwa nini, akasema Imekwisha.

Kila mmoja alitoka ndani ya shimo .

Tunaweza kubaki tunaumiza mioyo, tukabaki na magonjwa ya mwili, ndoto mbaya, tukabaki kujihukumu siku nzima, haitabadilisha kitu.

images-14 Hivi Ni Kwa Nini Mungu?

LAKINI KILA KITU KITABADILIKA ENDAPO TUTABADILI MTAZAMO WETU.

Najua unafikiri nini,.

Unataka kubadilika, pia unataka kumaliza kile ulichakianza,. au umekuwa ukijaribu mara nyingi kubadilika  umekwama na kuchoka, umechanganyikiwa. umechoka kuumwa, umejaribu kila kitu imeshindikana.!

kama huo moyo wako uko sawa , basi jua ya kuwa mungu anataka ubadilike, na  uko kwenye fast truki ya mungu ya miujiza yake. miujiza bado ipo inafanya kazi . itatokea tu ukimwamini mungu na kumkubali .

Neno siwezi,  yeye anaweza, kwa hio mwache yeye.

Mwache yeye akutoe kwenye shimo, akutoe kwenye magonjwa, masikitiko,maumivu,  kuachwa,  akutoe kwenye woga, mwache yeye akubebe akupeleke kwenye dunia ya rehema na wema ili upate rehema na neema wakati wa mahitaji.

MWACHE YEYE.:

Mwache yeye akubebe na kukubeba tena na tena na tena salama  kwake mahali ambako kutakuwa hakuna  kilio tena  sehemu ambako hakuna kwa nini?

Shirikisha rafiki na familia yako.

 

 

 

 

Previous Utafanyaje? Inapofika wakati Ukakata Tamaa Mwenyewe:
Next Vitu 8 Vya Kuwa Macho Kabla Ya Ndoa.

5 Comments

 1. […] -Hivi ni kwa nini Mungu. […]

 2. Avatar
  ombeni
  April 19, 2016
  Reply

  Nimefarijika sana kwa ujumbe mzuri

 3. […] HIVI NI KWA NINI MUNGU? […]

 4. […] =Hivi ni kwa nini Mungu […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.