HIVI UNAJUA KWA NINI MATARAJIO  YANAUA HAMU YA SEX KWENYE MAHUSIANO YA KUDUMU


www.usnews_.com_ HIVI UNAJUA KWA NINI MATARAJIO  YANAUA HAMU YA SEX KWENYE MAHUSIANO YA KUDUMU

Jinsi gani utaweza kurudisha hamu hio?

Ni mwisho wa siku. Tuko nyumbani na wenza wetu , tumesafisha jiko na vyombo vyote, watoto wamelala.

Tumekaa kwenye kochi na tumepumzika ,Wenza wetu wanapotuangalia lile jicho– unafahamu jicho hilo ninaloongelea.Jicho lenye maana ‘’i want sex’’

Halafu tunabaki kuganda.

Mapumziko yetu yanayeyuka hayapo tena. Ngozi inasisimka,misuli inakosa amani. Tunaweza kuwa tunawapenda na kuwajali wenza wetu–lakini bado tunakosa hamu ya kushiriki. Huenda pia tulitaka kufanya sex hata kabla ya kuona hilo jicho, lakini tumejikuta tunakosa nguvu .

Kwa Nini Inatokea Hivi Mara Nyingi? —hasa kwa wanawake– waliopo kwenye mahusiano ya kudumu?

Jibu huenda lisiwe lile unalofikiria.

Jibu la mada hii ni kwamba;

-Inasemekana Wanaume wanahitaji sex zaidi kuliko wanawake wanavyohitaji

-Usawa ulipo kwenye dhana hii ya kale  ni kwamba , kwenye mahusiano ya kudumu cheche hupungua.

Ingawa mitazamo hii imapitwa na wakati bado tunafanana nayo katika mitindo ya mahusiano kutokana na jinsi tulivyoona wakati tunakua.

Niliona baba akimshika mama makalio, halafu mama alimsukumia mbali. Ilionekana kwamba baba alitaka sex lakini mama alikuwa hataki. Sio kweli?

Kwa thamani ya mtazamo ni kweli. Lakini kuna cha zaidi kuliko hili.

Sio kwamba wanawake  hamu yao ni ya chini kuliko wanaume.

Ni kwa sababu ya mazingira , maandalizi yanayofanyika hayatoshelezi, hayana uzito wa kumvuta mwanamke ajisikie kwa wakati.

Tuchimbe kidogo kwenye hili.

Wanawake mara nyingi huwa hawagandi wakati wanaume wao wanahitaji sex kwa sababu  hawataki,

Naweza nikawa na hamu ya sex siku nzima na nikawa na matarajio ya kufanya hivyo. Na siku nzima nilikuwa namuwazia mazuri mume wangu. Lakini  wakati tu akinitazama kwa jicho la kutaka sex, hamu yote inapotea.

Sio kwamba sipendi au sikutaka sex,  ni mume wangu ndiye alieniondolea hamu hio. Ni kwa nini? Ni kuhusu pressure.

Kwa maana hio mwanaume alileta hio pressure.

Tumefundishwa kuwa , kuna hatua za kufanya sex, kwanza mnakiss,pili mnakumbatiana, halafu oral (sex may be),halafu mnafikishana nyumbani. Kwa hio kuna mtazamo kama huo.hasa kwenye mahusiano ya kudumu.

 

 

Nafikiri mtazamo huu umepitwa na wakati, wengi wetu hatujatambua hili kuwa linaharibu mahusiano.

Matarajio sio mazuri.kwa sababu yanatuletea pressure katika utendaji wetu.

Tunatolewa kwenye mood na ile tazama kwa sababu ya matarajio tofauti. Nilitegemea kuongea nae, kucheka nae kwanza , lakini kilichokuja akilini mwangu ni moja kwa moja sex.

Kinachofuatia ni kitu gani? Kitu gani kimejificha  kwenye mada hii? Anategemea kupata sex ,  mimi sijamwambia ninachokitaka wakati huo.

Matarajio sio mazuri. mguso, kuamshana. Tazama na mguso , akili inajaa matarajio. Yanatufanya tuogope kuwa huenda tusiweze kukutana na matarajio ya wenza wetu. Hii ndio sababu kubwa inayotufanya tukose hamu ya sex.

Kitu cha kufanya ni kuachana na mitazamo ya zamani. Ondoa fikra  na misingi ya zamani.  Anzisha Urafiki wa kimapenzi na mwenza wako.

Anza kumgusa mwenza wako bila matarajio, mkisi bila ya matarajio, mkumbatie bila ya matarajio. Toa na kupokea mapenzi bila ya matarajio, na mambo mengine yatatokea kwa urahisi bila ya pressure.

Anza leo.

Kila la heri.

Previous MAZOEZI 3 AMBAYO YATAKUPA NGUVU YA AKILI KWA DAKIKA 5.
Next NJIA NZURI ZA KUWASILIANA NA MWENZA WAKO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.