Ili Ufanikiwe Lazima Ushinde Vita Ya Ndani


g Ili Ufanikiwe Lazima Ushinde Vita  Ya Ndani

Kushindwa na kushinda ni kazi ya ndani.

Aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Unachokiamini ndicho unachokiishi. Huwezi kuamini kitu kingine  halafu uishi tofauti. 

Mara nyingi sana Wazazi ndio wanaharibu msingi wa watoto wao. Fikiria ni kitu gani mzazi huwa unamtamkia mtoto wako, hasa anapokuwa na maendeleo mabaya kwenye masomo. Ni muhimu sana kuelewa hilo. Kinywa cha mzazi kinaweza kikawa Hatma ya mtoto wake.

images-1 Ili Ufanikiwe Lazima Ushinde Vita  Ya Ndani

Shida inatokea wakati wazazi wanapokuwa hawataki kuwasikiliza watoto wao , hawasikilizi wala kufuatilia ndoto za watoto.  Matokeo yake badala ya kukuza ndoto za watoto , wanaziua kwa maneno  mabaya.

Kwa kila mwanadamu kuna mimba mbili, Mimba ya ndani na ya nje. Mimba ya ndani  ni uwezo, mipango, maono, ndoto iliopo ndani yako. Sikiliza mimba ya ndani ili iweze kukua  na kukuletea mtoto.

Mimba ya nje ni  Mazingira. Ukiwa mtu wa kuangalia mazingira yaliokuzunguka , watu waliokuzunguka, maneno yao, kusikiliza sauti ya kushindwa, Hutaweza kufanikiwa katika maisha yako. Kuza mimba ya ndani . Sikiliza kwa makini sauti ya ndani ya kushinda.

images Ili Ufanikiwe Lazima Ushinde Vita  Ya Ndani

Kanuni 10 Za Kufanikiwa Au kushindwa.

1.Mafanikio Ya Mtu Hayanzii nje bali yanaanzia ndani . Chanzo cha kila mafanikio ni mtu mwenyewe.

2. Kama mtu atakuwa na tabia ya mitazamo mizuri , mtu wa kufanikiwa kuanzia ndani mwake , hata nje kwake kutafanikiwa. mtu yeyote mwenye kutendea kazi  sauti ya mafanikio ni rahisi kufanikiwa.

3.Haijalishi ukubwa au udogo wa tatizo lililopo, iwe ndani au nje. matokeo yote yanaanzia ndani ya mtu. Chanzo ni mtu mwenyewe.

4.Mchakato wote unaanzia ndani yako, sio nje. Sikiliza ndani ya moyo wako. Moyo wako ndio wenye mchakato wote.

5.Kabla mshindani hajakushindwa, unakuwa tayari umeshindwa ndani yako. Lakini kama ungeona ushindi kabla hujaiingia ulingoni ungeshinda .

Rigobert-Song Ili Ufanikiwe Lazima Ushinde Vita  Ya Ndani

6. Ushindi wa kitu chochote huanzia ndani ya mtu mwenyewe kabala hajaanza kufanya kitu alichokitaka.

7.Ukiona kikwazo chochote tambua kuwa umekianzisha wewe ndani yako. Umekamatwa na hofu kubwa kabla hujaanza kufikia kitu chenyewe. Unakuwa umejenga picha ya kushindwa ndani sio kwenye mwili.

8.Vita kubwa ya kushindwa inatoka ndani. Haijalishi ni kiasi gani cha mazingira yanayokutatiza. Ni mtazamo wako tu .

Kuna watu hawana viungo  vyote kama ulivyonavyo wewe. Lakini wamejiona ndani mwao kuwa wanavyo na wakathubutu kufanya kitu kikubwa kama walivyojisikia ndani yao na kufanikiwa. Mafanikio yanaanza ndani sio nje. Badilisha picha uliyonayo leo utafanikiwa.

9.Usiruhusu sauti ya kushindwa ipenye ndani yako. Epuka mitazamo hasi. Tafuta taarifa nyingi zilizo sahihi utafanikiwa.

10. Mungu huwa anakuza uwezo mdogo uliopo ndani ya mtu ili kufanya mambo makubwa yatakayoonekana nje.

Bila ya kumkumbuka Mungu hakuna kitu kitatokea lazima nikuambie ukweli. Mrudishie Mungu Muda wake aliokupa ili akufunulie uwezo mkubwa uliopo ndani mwako. Una masaa 24, Je unajua kama unadaiwa muda na Mungu? Umekuwa ukifanya kazi zako nyingi sana lakini hukumbuki kumpa Mungu muda. 

Mkumbuke Mungu Akutatulie matatizo, changamoto zote unazopitia.

Ukiona mtu yeyote anapitia changamoto nyingi , tambua kuwa  Ndani mwake hakujakaa vizuri, Mungu hayupo pamoja naye.

Subscribe upate makala mpya kila mara.

 

Previous Kabla Hujampata Mtu Wa Kudumu Kwenye Mahusiano ,Jitafute Kwanza Wewe. Ujitambue.
Next Tofauti Kati Ya Urafiki Wa Kawaida Na Urafiki Wa Kimapenzi

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.