Imani Inayofanya Kazi Ndani Ya Maisha Ya Mtu


christ-apostles-large-300x300 Imani Inayofanya Kazi Ndani Ya Maisha Ya MtuKatika maisha chochote unachokiamini utakifanya.

Imani ni ujasiri alionao mtu, imani ni Nuru iliopo kwa mtu, Imani ni mbegu ambayo mtu akiitumia vizuri lazima impatie matunda, Imani ni kuthubutu kufanya kitu ambacho kinaonekana hakiwezekani kwa wengine lakini wewe unaamini kukifanya. 

Imani sio suala la Dini.

Ukiamini utafanya. Matokeo ndio yatakupa imani .

Ukimwamini Yesu  na kazi zake na neno lake kwamba yeye ndiye njia ya kweli na uzima, Na ukaamini kuwa alikuja kwa ajili yako  , utaona matokeo.

Anasema , Aniaminiye mimi , kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atafanya; Naam na kubwa kuliko hizo atafanya. 

Kazi kubwa hapa ni kuamini. Je imani yako iko wapi. Yesu akirudi ataikuta imani? Ukiomba kitu kwa Mungu, akiangalia  ndani yako ataiona imani?

Kitu kinachoangaliwa ni Imani kwanza.

Kuna kaka mmoja alienda kwa Mganga wa kienyeji baada ya kusimuliwa na mwenzake jinsi alivyofanikiwa kwenye kazi zake, Jambo la kwanza mganga alichomuuliza ni hili, Nani amekuambia, Akamtaja huyo rafiki yake. Swali la pili lilikuwa , Alikuambia kila kitu? akasema ndio. la Mwisho lilikuwa hivi , Unaamini?  akasema ndio. Mganga hakuwa na kazi kubwa tena kwa sababu yule rafiki yake tayari alishaifanya kazi yote, alichomwambia ni maagizo ya kwenda kuleta ili aje apewe maelekezo.  Imani.

Ukimjua Yesu utamjua Baba. Yesu ni njia ya kweli na uzima. Huwezi kwenda kwa Baba ila kwa njia ya yeye. Ukitaka kuwa karibu na Mungu , anza  kuwa na ukaribu na Yesu, Fanya urafiki na Yesu . Yesu ndio Imani tosha. Roho mtakatifu ni muda. Mungu ni Upendo.

Ukimwamini Yesu , Moyo wako utakuwa na furaha, Amani Upendo, utu wema, fadhili, Uaminifu, uvumilivu, unyenyekevu, nidhani na upole, Sivyo kama ilivyo vya Ulimwengu huu.  Amani ya ulimwengu ni ya muda mfupi, Furaha ya Ulimwengu ni ya muda mfupi, Upendo wa muda mfupi, mafanikio ya muda mfupi, lakini  vya Yesu ni vya kudumu milele na milele.

Imani ni sasa. anza kuamini sasa sio kesho. Kama kuna kitu unataka kufanya, fanya sasa usisubiri kesho, Siku ikipita imepita, Fadhili za Bwana ni mpya kila siku na rehema zake ni mpya kila siku. Amini .

Ukiamini hutajiuliza uliza, Utaomba kwa jina la Yesu na kwa kuwa utakuwa tayari umefanya kazi za Yesu,  Amin, Amini nawaambia , Mkimuomba Mungu neno lolote kwa jina la Yesu atawapa.

Ukijua kweli, ambayo ndio neno la Mungu, Utakuwa mzima kiakili, utakuwa mzima kiroho na kimwili, utakuwa huru, hutakuwa na chuki na watu, utawasamehe watu , utajisamehe wewe mwenyewe, utamuomba Mungu TOBA Kila mara, utamshukuru kila wakati, utamtukuza kila wakati , kwa kuwa utakuwa umejua kweli , umeitambua nguvu itendayo kazi ndani yako.

Ukiamini utakuwa mtu wa kufikiri. Utatumia Muda wako kutengeneza tabia mpya, kawaida mpya maishani mwako. Tabia njema inatengenezwa na muda.

Maisha ni Muda,

Muda ni Upendo

Upendo ni Mungu

Mungu ni Imani

Imani ni Hekima

Hekima ni neno la Mungu.

Amini neno la Mungu, wala usiifuatishe namna ya Dunia hii, bali geuzwa  upya nia yako ili upate kujua Hakika  mapenzi ya Mungu yalio mema na ya kumpendeza.

Angalieni sana jinsi mnavyoenenda si kama watu wasio na Hekima bali kama watu wenye Hekima; Mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Huenda hufanikiwi kwenye kazi zako, biashara zako, ndoa yako, huduma yako, sio kwa sababu huna akili, bali ni kukosekana kwa Imani ndani yako.  Changanya kazi na imani, changanya ndoa na imani, changanya huduma na imani, changanya biashara na imani.

Amini kuwa umefunguliwa mlango mkubwa kwa ajili yako , FIKIRI ni kitu gani kinakuzuia , kinakupinga usiingie mlango huo.  kitu gani kina kupinga usifanikiwe.

Mungu anasema , nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi, Ng’ombe amjua bwana wake, Punda ajua kibanda cha bwana wake, lakini  watu wangu hawajui, watu wangu hawafikiri.

Mungu anataka kuona IMANI yako kwake. Mungu anakutaka Ufikiri.

Subscribe.

 

Previous Unajihisi Uko Kwenye Umri Gani?
Next Kuona Vitu Ambavyo Havionekani

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.