IMANI YA KWELI INAONEKANAJE .UMUHIMU WAKE NI NINI


slide_2 IMANI YA KWELI INAONEKANAJE .UMUHIMU WAKE NI NINI

Mungu ni wakushangaza, tena ukubwa wake haujulikani, anaabudiwa na kila kiumbe , wapo wanaosema kuwa Mungu yupo juu  mbinguni, na wengine wapo wanaosema kuwa  kuwa  anakaa minguni. lakini mungu ni  mkuu  hatuwezi kufikiria ukuu wake.  angekuwa ana nyumba basi hio sehemu  ingekuwa ni patupu.

Lakini kuna nafasi  kubwa kati ya  kuamini na ukweli wa kila siku . Na tunahitaji kupona katika  nafasi hii iliopo.

Kila kinachoonekana, tulichonacho , kimeumbwa  kutokana na vitu visivyoonekana, tena ni zaidi ya muda na nafasi , hiki kisichoonekana  ndio chanzo cha yote haya yanayoonekana. Sio patupu bali  kitu fulani kimetengeneza  nguvu hii.

Kuwepo kwa nyota , mvua, wanadamu  na mawazo yetu, hisia zetu, kumbukumbu zetu, na  nia zetu.

Haijalishi ni kwa njia gani ila lazima uamini yupo Mungu, ambaye hufanya mambo kwa wakati unaohitajika , mfano katika hizi hatua zifuatazo.

1.Mungu  hutuokoa

Mzazi hawezi kumwacha mtoto wake  aungue kwenye moto, ataingia ndani kumuokoa . na ata hakikisha usalama wa mtoto wake. ndio maana tunamkimbilia mungu , kwa sababu  tunahitaji kuishi.

2.Mungu anayejibu.

Hii ni kazi ya ubongo , ni zaidi ya  kuishi , kila mtu  ana mahitaji anayoyahitaji  , mimi kama mimi nahitaji  mahitaji yangu   ya kipekee.  na katika mahitaji haya  utakuta  Mungu mpya huanza kutokea, ambaye ana nguvu, na sheria na utaratibu. kwa hio tunarudi  kwa mungu  kwa sababu  tunahitaji kufanikiwa, kukamilika na hata katika kushindana sisi kwa sisi.

3.Mungu wa Amani Na Ufahamu.

Ubongo unaweza ukawa unafanya kazi , na unaweza kuwa na utulivu, kwa kuwa ni wajibu wa ubongo  kufanya hivyo  panapohitajika amani na utulivu na ufahamu. Mungu anayeleta amani na utulivu wakati wa matatizo. Ndio maana tunarudi kwake kwa sababu  tunahitaji kujisikia kwamba  dunia haiwezi kutumeza na kutushambulia.

4.Mungu ni nuru.

Ubongo wetu unaangalia ndani na nje ,  lakini ufahamu wa nje  ni lengo,  wakati ufahamu wa ndani ndio Nuru yenyewe, tunajifahamu ndani yetu kuwa tuna amani, au tuna matatizo, tunajifahamu kuwa tuna upendo au hatuna.  tuna furaha au hatuna. tuna huruma au hatuna.. Mungu anahusika katika haya  na hutuelewa  na kutusamehe. tunarudi kwake  kwa sababu  tunamuhitaji atuhalalishie ulimwengu  wetu  wa ndani  kuwa ni mzuri.

5.Mungu Muumba

Mungu wetu anawajibika katika kuumba, Ubongo wa mwanadamu  unaweza kugundua kitu  kipya  cha kweli na kukiumba.  uwezo huu hautoki popote ila  ni katika  kisichojulikana ndio kilicholeta  wazo jipya .

tunaita hivi kwa sababu  umetokana na yeye mungu  ndie  alieumba  ulimwengu na vyote  vilivyopo pasipo  na chochote.  ndio maana tunarudi kwake  kutokana na ukuu huu  usiojulikana.

6.Kuwajibika katika maono.

Ubongo  unaweza kuona nuru  na ufahamu  halisi ambao  una furaha na baraka . lakini kunakuwa hakuna mizizi ndani yake  hasa katika ulimwengu  wa vitu. inakuja kwa maono, unapata uponyaji na miujiza kwa maono. lakini usipoweka mizizi inabaki kwenye maono.

Kwa hio tunamwitaji mungu  ili atuelezee  kwa nini  miujiza ipo upande wote , kwenye kawaida na ukweli.

7.Utakatifu.

Kuwajibika katika utakatifu,  hapa ubongo  huzaliwa  ukiwa mtupu , hauna kitu chochote. hakuna kitu kinachofanya kazi ndani yake, hata kama mambo milioni ngapi  ya mabaya yakija  hayawezi kufanya kitu. wenyewe unaishi  tu bila ya  Hatia., tena kwa urahisi sana.

Akili ndani ya ubongo ni chanzo cha  asili cha kulinganisha.tunaye mungu anayeishi , ambaye hutufikiria  hivyo. tunamuhitaji huyu mungu  kwa sababu yeye ni chanzo , bila chanzo  hatutapata  msingi  wa kitu chochote hata kama ni kidogo. Kwa sababu kila jambo linaanzia kwake

Yeye ndiye mzabibu wa kweli, yeye ndiye chakula chetu cha kila siku,  yeye ndiye njia ya kweli ,  yeye ni nuru ya ulimwengu, na pia ndiye mchungaji wetu. tunamwitaji  yeye.Bila yeye tutakuwa gizani.

Wahirikishe wengi facebook wajifunze  ufahamu huu.

Ubarikiwe.

 

Previous VYAKULA VINAVYOFANYA KAZI KWA WANANDOA WANAOTAFUTA KUPATA MTOTO
Next USHAURI BORA KWA WANANDOA KWA AJILI YA KUDUMISHA MAHUSIANO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.