INAMAANISHA NINI KUWA MWANAUME. HAPA NI KWA WANAUME WOTE AMBAO…


What-it-means-to-be-a-man-with-Dr-Massimo-Stocchi-1 INAMAANISHA NINI KUWA MWANAUME. HAPA NI KWA WANAUME WOTE AMBAO…

Leo nataka  nimuadhimishe mwanaume ambae  anajaribu  kujielezea upya  kuwa ina maana gani  kuwa yeye ni mwanaume.

1.Hapa ni kwa mwanaume ambaye anaitikia badala ya kujibu,  hapa ni kwa mwanaume anaejali mwili wake na kula kama mtu mzima, sio kula kama teenagers.

Hapa ni kwa mwanaume anayetaka ubora na kutembea na nuru inayomwangazia,  sio kuwa mtu wa kutembea na kioo , lakini anaangalia tabia yake  na kuwa makini  na maneno ya kuongea  na vitendo  ambayo  vinaleta athari kwa wengine.

Hapa ni kwa mwanaume anayekubali mapungufu yake  na kujitahidi kuwa bora.

Hapa ni kwa wanaume ambao wanafanyia kazi mahusiano yao  kwa ajili yao. Badala ya kutaka kuwabadilisha na kuwatawala  wenza wao.

Hapa ni kwa wanaume  wanaocheck  tabia zao, mara nyingi . Hapa ni kwa wanaume  ambao hawalalamiki au kuwa na udhuru kwa wenza wao.

Hapa ni kwa wanaume  wanaoamka mapema  na kutaka kujenga kitu fulani.

2.Hapa ni kwa wanaume wanaochagua kuwa wanafunzi kila siku, ili kujifunza kutoka kwa wengine badala ya kufikiria  kuwa wao ni bora kuliko  wengine.

Hapa ni kwa wanaume wanaofungua mlango na kukiss kwa kumaanisha , na kupenda kwa juhudi.hapa ni  kwa wanaume wasio na pepo, hapa ni kwa wanaume wanapiga simu wakati wanapokuta misscall, hapa ni kwa wanaume  wanaoamini katika foreplay.

Hapa ni kwa mwanaume ambaye haishi yaliopita , anaishi sasa. Hapa ni kwa mwanaume mwenye kushikilia  wazazi na familia yake  kwa ujasiri. Hapa ni kwa wanaume wanatengeza amani . hapa ni kwa mwanaume anayewajibika anapoona amekosea au kumuuza mtu

ja061 INAMAANISHA NINI KUWA MWANAUME. HAPA NI KWA WANAUME WOTE AMBAO…

Hapa ni kwa mwanaume  anayeweza kuamini vitu vikubwa kuliko wao wenyewe.hapa ni kwa wanaume ambao  wana moto kwenye matumbo yao, hapa ni wanaume wenye kufanya maamuzi ,kutembea kwa uhakika na kuwa na ndoto kubwa.

3.Hapa ni kwa wanaume wanaoweza kutenganisha  uwezo kutoka kwenye ustahili, hapa ni kwa wanaume  wenye kukumbuka siku ya kuzaliwa na siku za anniversaries.

Hapa ni kwa wanaume wenye uwezo wa kuweka mawazo yao kwenye  vipaji  vyao. Hapa ni kwa wanaume wanaoelewa majukumu  ya kuwa  baba wa  familia, hapa ni kwa wanaume  wanaotumia muda wao kuwa karibu na watoto wao.

Hapa ni kwa wanaume wasioogopa kuonyesha   upendo. Na hapa ni kwa wanaume wanaochagua  mazingira magumu

Hapa ni kwa wanaume wanaosema Nakupenda.  Hapa ni kwa wanaume ambao wanaweza kudhibiti hasira zao , pombe au ulevi, na pesa. Na hapa ni kwa wanaume wanajitahidi kujipenda kila siku. Hapa ni kwa wanaume ambao si masikini na wala hawategemei mtu kipato chao.

Hapa ni kwa wanaume  ambao mara zote wao ni positive inapokuja jambo.

Hapa ni kwa wanaume wasiobadilika kwenye ushirika wao , ni wa kweli siku zote.hapa ni kwa wanaume  wanaoelewa huruma  na Uelewa  

Hapa ni kwa wanaume  wanaoosha vyombo  na kufanya usafi. Na hapa ni kwa wanaume  wanaotaka kufanya  mabadiliko.

Umeipenda hii makala shirikisha wengi  wajifunze.

Previous NJIA 3 ZA NGUVU NI KUWA POSITIVE , HAIJALISHI UNAPITA KWENYE CHANGAMOTO GANI.
Next NI KWA NAMNA GANI HISIA NZURI ZINA ATHARI MAISHANI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.