ITAKUAJE ENDAPO MTOTO WAKO ATACHAGUA KUFANYA VIBAYA?


talentedkid ITAKUAJE ENDAPO MTOTO WAKO ATACHAGUA KUFANYA  VIBAYA?

Itakuaje kama  mtoto wako atachagua kufanya kitu ambacho sio sahihi na wakati anaelewa kuwa ni mabaya kutoka kwenye mazuri?

Watajuaje kizuri kutoka kwenye kibaya kama hawajawahi kuambiwa  kitu gani kitatokea endapo watafanya kitu kibaya? Tutafanyaje endapo  mmoja wa watoto ataharibu kitu? Tutafanyaje endapo  tutawaambia kufanya kitu na wao hakutaka kusikia? Itakuaje kama akimpiga mtoto mwingine?

Kwa nini kuwaumuza  watoto sio fundisho la kweli, na watoto watajifunzaje kujua kitu sahihi na ambacho sio sahihi , siku za leo.

Kwa nini mtoto anajua kuwa hiki kitu sio sahihi na bado anachagua kufanya  kisicho sahihi?

Wazazi wanawajibika   kutokana na kukosa nidhani kwa watoto na kupata matatizo. Hii inasababisha maumivu ya kimwili au ya kihisia.  Watoto wanaweza kuepuka  hayo matatizo kwa kuchagua tabia nyingine watakapokua. Lakini inaonekana kuwa mtoto anaweza kurekebisha tabia yake na hisia zake.

Tunatakiwa kuwasaidia watoto kutokana na hisia mbaya  ili wasije wakakua nazo na kuwaletea matatizo baadae, na tunawasaidia  kutowaumiza  wengine na kutoharibu vitu. Kuliko kuwaadhibu kupitiliza. Inatakiwa sisi kuwa ndio mfano wao .

Inawezekana kuwafundisha watoto kwa upendo.

Kama  umemwambia mtoto wako  kufanya kitu fulani  na hakutaka kusikiliza .

Inawezekana hakusikia vizuri au  wanakuwa wanapenda zaidi wanachokifanya kuliko kusikiliza tunachowaambia . Na kuna mtoto mwingine anaona ni muhimu kucheza kuliko kwenda kuoga au mwingine anaona ni muhimu kwenda kuoga kuliko kucheza.

Kitu cha msingi ni kuwa karibu na mtoto wakati unapomwambia kitu, usiseme wakati uko mbali na yeye na kutegemea kuwa  amesikia na atafanya kile unachomwambia.

Ukiwa karibu yake tambua kile kitu anachokifanya , na ukichunguze kwa umakini, na umpongeze  kwa anachokifanya kuwa ni kizuri, ukishaona anakusikiliza hapo ndipo pa kumwambia kitu ambacho unataka kumwambia.

Kama utamwambia na utaona hasikilizi , usirudie kusema . huwezi kupata usikivu wa mtoto wako. Rudi kwenye hatua ya kwanza   ya ukaribu na kumpongeza kwa kile ambacho anakifanya na kwamba unakubaliana nae , lakini pia unataka  yeye afanye kitu….

Sidhani kama kutosikia ni deal kubwa sana , kitu kikubwa hapa ni  Utii.. vipi kama utamwambia mtoto kufanya kitu fulani na hakutii.? Huo wakati ambao ulitaka atii.

Kama akimpiga mtoto mwingine.

Hio ni dalili nzito sana. Inahitaji msaada wa haraka  kwa kutokana na woga. Woga huo unaweza ukawa nyuma ya   familia. Au wazazi wanapopigana ? kuna kitu nyumbani kinachompa woga huo Labda ni picha anazotazama kwenye Luninga ndizo zinamfanya awe hivyo? Au anakuwa na woga kuwa hawezi mahesabu shuleni na watoto wenzake wanamcheka na kujiona mjinga? Au anaogopa kwa sababu baba yake ni mkali  anafoka foka kila wakati ? Au anaogopa kutokana na adhabu zetu na kupigiana makelele sisi wazazi? Au anahofu kuwa humpendi  vya kutosha?

Ni muhimu kuelewa kuwa endapo tutaendelea kuwaadhibu, hatutaweza  kujifunza  chochote kutokana na haya.  Hatuwezi kujua ni kitu gani kinamfanya akose furaha, asiweze kusikiliza, asiweze kutii. Ni lazima kutafuta vitu ambavyo vinafanya kazi ya kurekebisha tabia yake..  Ili aweze kukabiliana na mambo hayo baadae akikua.

Kama utamzuia kutazama Tv ,  bila ya kutambua tatizo linalomsumbua, unafikiri utakuwa umetengeneza kitu gani. Kitu cha kufanya hapa ni kutambua tatizo la mtoto na kulitibu kwanza  ili kuondoa woga na huzuni , na kutokuwa na utii, kutazama ni wapi haya yanatokea. Na kuanza kumjenga upya ili awe na hisia nzuri na kuepuka  kuingia hisia mbaya.

Kama utagundua kuwa ameharibu kitu, kumbuka hata wewe unaweza kuharibu kitu , hasa wakati mwingine  bahati mbaya .  hivyo ni vitu vya kawaida sio vya kumwadhibu mtoto.

Lakini kama kila mara anaharibu vitu , hapo ni mahali pa kuwa makini kumfuatilia, lazima kutakuwa na tatizo kwako, hizo ni alama nyekundu zinajionyesha.. Hutajifunza kwa kumwadhibu , na huenda hukumfundisha jinsi ya kujali vitu . kumwadhibu hali itakuwa mbaya zaidi ya ile ya kwanza. Wakati mwingine unakuta mtoto anapiga kelele wakati anaharibu hivyo vitu. Hapo  utambue kuwa anahitaji msaada kutoka kwako, kuna kitu kinamsumbua.

Ukimwadhibu  unapoteza  uwajibikaji wako kama mzazi wa kutaka kumjua mtoto ili umsadie.

Adhabu huharibu hisia na kumfanya mtoto awe mbaya zaidi, Uponyaji wa hisia  unabadilisha tabia na  kuondoa tabia mbaya.

hqdefault-1 ITAKUAJE ENDAPO MTOTO WAKO ATACHAGUA KUFANYA  VIBAYA?

Ni wakati gani Watoto huchagua  kitu sahihi kutoka kwenye kibaya.

1.Wanakuwa karibu na wewe, kwa hio wanakuwa na sababu ya kuchagua hata kama kitamgharimu.

Watoto wanakuwa mbali na sisi wazazi kwa sababu ya kutokujali kuwasikiliza wao, na kujua hisia zao.  Ni muhimu kuwa karibu yao , ni kama tunavyokuwa na   mwenza unayempenda.

2.Wanaweza kudhibiti hisia zao,  zinazowaruhusu kudhibiti tabia zao.

Watoto wanapoharibu , ina maana hakuweza kujidhibiti wao wenyewe.  Ni kama watu wazima , kumbuka siku ambayyo ulisema  samahani nimechelewa kwa ajili ya kitu fulani.  Kuadhibu haisaidii , badala yake utazidisha hali mbaya ya mtoto. Na kumletea ugumu.

3.Kama mtoto wako atakuwa hajali , iwe anafanya sahihi au sio, ni kawaida.  Bado atakuwa anaonyesha kuwa anaweza  kuwa mwenyewe bila hata ya kusema  hapana kwa kila kitu unachomwambia. Lakini watoto ambao wamekua na ambao wapo karibu yako   usiwakatishe tamaa.  Kwa hio huwezi kutatua bila ya nidhamu.

Ni kazi ya wazazi kuwa na umakini katika kuhakikisha watoto wao wanakua wakiwa na nidhamu,  utii, afya, uwajibikaji na mengine.

Previous NI SAWA URAFIKI UKIVUNJIKA - INA MAANA KWAMBA UNAKUA
Next NILIPOBADILISHA MTAZAMO, HAPO NDIPO NIKAPATA UPENDO USIO NA SABABU

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.