JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:


How-to-Get-Over-a-Breakup-According-to-Science JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

Watu wengi  hawana bahati ya kuwepo kwenye mahusiano ya kudumu, ingawa kuna msemo usemao kuwa , kuolewa ni bahati na sio lazima. Ni kweli kabisa kuolewa ni bahati. maana ingekuwa lazima basi hakuna mwanamke  ambae angeishi peke yake.

lakini kuna hili nalo la kuachwa , au  kubwagwa na mtu ambae ulimtegemea  kuwa ndio wa kufa na kuzikana.  au kuna ile kuolewa kuondoa nuksi  halafu baadae matatizo matupu, kwa sababu umelazimisha  , hasa upande wetu wadada, ukiona muda umeenda , utajitahidi  njia nyingi  ili uolewe na mtu hata hakupendi, matokeo yake kubwagwa.

Ngoja twende kwenye pointi yetu, Ni ngumu sana pale mwenzako anapokueleza ukweli kuwa hakupendi na anahitaji kuondoka, wakati huo labda wewe tayari una mtoto au watoto.

Lakini kumbuka kuna mateso makubwa kuishi na mtu ambaye humpendi, hasa kwa wanaume ni ngumu, lakini nataka wewe utambue hilo , endapo utagundua hilo  na kama umetamkiwa kabisa , anza kujiandaa kisaikolojia., ili akiondoka usije badilika kwa tabia tofauti na ulizokuwa nazo.

Panga akili yako vizuri na umruhusu aondoke kwa amani, lakini kama hutafanya hivyo, basi akiondoka na kwenda kwa mtu mwingine , utaumia sana, matokeo yake  ni  kuchanganyikiwa. epuka kufanya mambo yafuatayo,

1.Epuka kufanya kisasi, mwachie Mungu.

images-1 JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

 

Unapoachwa  ni kama adhabu  fulani hivi, akilini mwako utajiona kama hukufaa , hukuwa mzuri, hukumridhisha, na mambo mengi utafikiria. lakini nakuambia hivi, haijalishi ulipigwa , ulitukanwa, ulikuwa na mahusiano kama ya kumbikumbi, ni uongo gani umeambiwa, hayo yote yamepita.

mpendwa funga mlango,  kaa kimya kama vile hakuna kitu kilichotokea, usitafute kurudi, hauhitaji mchezo wa kuigiza na kushangiliwa na watu baada ya kuvujwa moyo wako.AMKA jikung’ute kwa ajili ya maisha mapya. mshukuru Mungu kwa hilo.

2.Epuka kusikiliza nyimbo za huzuni:

images-7 JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

Baada ya kubwagwa, epuka kusikiliza nyimbo za kukuumiza kwa mawazo, nyimbo za kukunyima usingizi, za kukuvunja moyo, nyimbo kama, Tulikuwa tunapendana. nyimbo zote za mapenzi,. sikiliza nyimbo za kufurahisha za kukufanya ujione mshindi, mwenye amani  tele.

3.Epuka kuyaita mahusiano yako kuwa ni magumu.

Unapoulizwa na watu kuhusiana na aina ya mahusiano yako , usiseme kuwa yalikuwa magumu. kwa mfano, mimi ni Single, neno hili kwangu  ni sahihi na linanipa amani kubwa sana kulitumia. endelea kuhudumia moyo wako usipatwe na mawazo mabaya. kuongea kuwa ni magumu haitakusaidia kuponya  maumivu yako. acha kuwaza yaliopita

4.Epuka kumsema vibaya ulieachana naye.

h-FRIEND-BREAKUP-628x314 JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

Mwenza wako anapoamua kuondoka na kwenda kwa mwingine usiwaambie walimwengu, uswaambie mashoga zako kuhusu yeye, itakufanya uonekane mtu mbaya bila wewe kujua, utaharibu mwonekano wako, na tabia yako, ukisema vibaya kuhusu yeye., pia utaonekana la mkosaji, maana wakosaji ndio huongea mabaya kwa wale ambao  hawakufanikiwa kuwapata.

5.Epuka kutuma meseji za ajali, yaani za bahati mbaya.

meseji kama , ooh, samahani, pole, nimekosea. habari yako, sikuwa namaanisha kukutumia wewe. yote ya nini. jaribu tu kuongea naye kwa kawaida maana utakuwa kama unaongeza chumvi kwenye jeraha lako mwenyewe. na hutakuwa unaumia upande wako tu, bali hata yeye atakuwa anaumia kwa mtindo huo.

Kwa kuwa utaonekana hujali kitu. pia uwe mwangalifu katika maongezi hasa pale inapokuja kuamua kurudi kwa ajili ya msamaha. punguza kutuma au kupiga simu. kumbuka kuwa watu hawapendi pale unapojaribu kuwa smart. pamoja na kusema umekosea meseji , lakini huamini kuwa unahitaji kurudi hata kama ilikuwa ni makosa kiukweli.

6.USIKUBALI KULALA NAE TENA.

break-up-sofa JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

Ukikubali kulala nae umekwisha , maana yeye atakuwa anakutumia kwa ajili ya  mahitaji yake  ya kutoa  mawazo wakati anatafuta mwingine. na hapo ndipo utakuja umia zaidi kuliko mwanzo. unachotakiwa kufanya wewe ni kumtoa kabisa maishani mwako, chukua muda ili upone majeraha. tafuta nafasi ya kusonga mbele.

Koma kabisa kulala nae,  hakuna kitu anachohitaji kwako zaidi ya hicho.

7.Epuka kujibadilisha mwonekano wako.

1-1 JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

Kuachana ni huzuni, tena ni vibaya sana. lakini inaweza kuleta mabadiliko makubwa sana maishani mwako.

inakubalika kufanya mabadiliko baada ya hilo, ni sawa na ni busara kubwa , hasa mabadiliko ya  baadae ya maendeleo mazuri.  lakini kubadili  ngozi yako, kama ulikuwa mweusi na kuwa mweupe sio jambo zuri, na pia kubadili  uvaaji wako mzuri na kuwa na nguo za kiajabu ajabu utapotea, maana utakuwa unatafuta kuwatega watu.

pamoja na kuweka tatoos au kuongeza maumbo sehemu za mwili haitakusaidia chochote, utaharibikiwa. wewe fanya mabadiliko ya muhimu kwa ajili yako , sio kama mtu  ambaye anatafuta kujitangaza.

8.Epuka kuomba msamaha ili urudi , au arudi.

ni kawaida kwa wanawake kuomba msamaha kwa ex wao kurudi, ni jambo zuri  tu  sikatai. lakini kama mwanaume amesema basi ni basi. mpendwa mwache aende moja kwa moja. na kama ameamua kukaa kando  ina maana wewe ndio uliemlazimisha akuoe haitakusaidia.

muda huo sio wa kumsihi, kumuomba, kumpigia magoti kama ndio kitu kizuri cha kufanya. lakini kama mwanaume ameamua  kuondoka kabisa, hakuna namna nyingine, labda utafikiri ataona huruma kuona machozi yako ili abaki. ndugu yangu hutakuwa na amani maana  utaonekana wewe si kitu bila yeye.

9.Usikumbuke yaliopita mkiwa pamoja.

woman_onlineshopping JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

 

Tafuta kitu cha kufanya ili kukuweka bize muda wote,  wakati mwingine soma vitabu vya namna ya kufanya ili kupata maendeleo,Angalia   tamthilia mbalimbali ,isipokuwa za mapenzi achana nazo. tafuta marafiki wazuri wa kutoka nao na kufurahi pamoja. usikumbuke ya nyuma, jinsi mlikuwa mnafanyaje, labda sasa anafanyaje na mwingine, achana na hayo mawazo.

Hayatakusaidia badala yake utaumia. ukikaa muda wa kutosha fungua akili yako  kwa ajili ya mambo mengine yanayostahili maisha yako. lakini ukirudisha mawazo ya nyuma sio tu utaumia bali  hata wale wanaokuzunguka watashindwa kukusaidia.

10.Usifanye urafiki naye.

Really-Sweet-Things-To-Say-To-A-Girl JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

Ningumu kwa watu wawili waliokuwa wapenzi  kuwa marafiki.kama huwezi kuamini jaribu,. lakini usijaribu mpaka hapo majeraha yapone kabisa.kukubali urafiki wakati  mmeachana, mkaenda mkono kwa mkono na hata kuamua kulala nae, baada ya kuvunjika kwa mahusiano, hutapata nafasi ya kusonga mbele.

Ndugu kata kamba hio haraka sana mpaka hapo  utakapopona majeraha  uliopata .

 

shirikisha rafiki na familia yako makala hii , kisha toa maoni yako.

 

 

 

Previous KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.
Next JIFUNZE MANENO BORA 150 YA UAMINIFU KATIKA MAISHA:

2 Comments

  1. Avatar
    yona
    July 7, 2016
    Reply

    mimi naitw yona ninatatizo la over filling love hata shule nawaza mapenz tu nifanyajw

  2. […] -Jiepushe na mambo yafuatayo 10 baada ya kuachwa […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.