JIFUNZE KUPENDA KWA UFAHAMU ZAIDI, KWA NDANI ZAIDI, KWA UKWELI


passionate-love JIFUNZE KUPENDA KWA UFAHAMU ZAIDI, KWA NDANI  ZAIDI, KWA UKWELI

Unataka kujijali? Na kuwapenda wengine. Unavyowapenda wengine, unajifunza kujipenda wewe kama  mtu anaestahili kupata upendo huo.

Kujijali ni kazi ambayo  kila mtu anatakiwa kuwa nayo  na ni kusudi la kisaikolojia  ndani ya miili yetu. Usawa wa hisia ni sehemu ya kujijali, hisia zingine  ni za hasira,   za huzuni, za wasiwasi na woga.

Ukitaka kuondokana na hisia hizi , unahitaji kuwapenda watu , wengi watashangaa vichwani mwao, na kuwa na maswali mengi. Ni nini basi upendo wa  aina nyingine ambao unatuchoma kila mara tunapojaribu kupenda watu.

Inachanganya . upendo wa kweli hata siku moja hauwezi kukuchoma, wala kukuumiza.  Kama utampenda mtu kwa kutambua  ukweli wa upendo.

Upendo ambao unatumiwa duniani , sio upendo ambao uliagizwa kutumika.  Umebadilishwa. Kuna maana nne za upendo .  

Upendo wa mama na mwana

Upendo wa  kaka na marafiki ambao wanakupenda pia

Upendo wa mapenzi

Na upendo wa huduma , kuhudumia watu.

Kila aina ya upendo huo inaeneza upendo (affection), nguvu. Lakini nguvu yake inategemeana na kila upendo. Ukweli huo ni kila mmoja anavyopenda. Unahitajika upendo wa agape. Ambao ni wa kuhudumiana sisi kwa sisi. Kwa ajili ya wengine kuwa na hali nzuri.

Tunaongea ukweli hapa . Unataka kujijali? Basi anza kuwapenda watu wengine.

Unataka kugundua haraka mabadiliko ya mwili wako?  Basi anza  kupenda kufanya mazoezi na tafakari.

thegreenslate-1024x683 JIFUNZE KUPENDA KWA UFAHAMU ZAIDI, KWA NDANI  ZAIDI, KWA UKWELI

Unataka kujua jinsi gani watu  wanakataliwa na wengine?  Basi chagua upendo juu ya kila baya.

Nadharia ya upendo inahusiana na mambo ya kisaikolojia , lakini  hayapewi umakini vile kama inavyotakiwa.. Kwa hio ni kufanyia kazi upendo ili upate upendo ndio afya ya upendo ilivyo. , sio kusubiri kutoka upande mmoja kwanza  kwa ajili ya kutosheleza  upendo  kwako.

Tumezaliwa kupenda na kupendwa.  Ukweli kwa wale ambao wameonyeshwa upendo toka wakiwa tumboni  mwa mama zao , wameonyesha kuwa na upendo mkubwa kwa wenza wao na hata kwa watu wengine.  Na wamekuwa wakipendwa pia.  Wakiwa katika ukumbwa wao.

Sayansi ya kusamehe iko wazi; unataka kupona kutoka kwenye hisia za maumivu uliopata?  Basi ingia kwenye hali ya kusamehe  na jitahidi kuwapenda wale ambao hawakupendi. . hata kama wako mbali , mahali ambapo huwezi kufika, samehe na kuwapenda kwa hisia.  Na hii sio  kufikiria , ni kufanya uamuzi mara moja.

Kwa kadri unavyozidi kuwapenda  watu unakuwa binadamu wa kweli.

Unatafuta kujijali kwa sababu ya tatizo la afya yako, au hali yako ya kisaikolojia , au changamoto za mahusiano? Kwa hio jaribu mazoezi haya

1.Rudisha hali yako ya utoto , ambayo ulikuwa unapendwa bila ya sababu yoyote.  Ilionekanaje? Hali hio inakuwaje? . fahamu huu upendo sasa kwa sababu  upendo haufi  ila unapoa.  Hata kama hakuna mtu ambaye anakuonyeshi mapenzi  kama haya.

2.Halafu mpende mtu  wakati huu.  Inaweza kuwa kwa kutuma ujumbe  au kumkumbatia  au maneno mazuri ambayo yatamfanya huyo mtu ajisikie tofauti. Be creative

3.Kuna mtu  ambaye yuko mbali  bado una hasira naye? Sasa mpe upendo  ambao ulifanya kwenye namba 2 pale juu.

4.Kuna mtu yeyote kwenye maisha yako  sasa ambaye  anaweza kuwa karibu  yako , na angeweza,  lakini wewe unajiweka mbali?  Msamehe huo mtu kwa kumpa upendo wa namba 2, na  namba 3.

5.Sasa jipende wewe upendo huo ,  kama unahitaji kujisamehe. Jitambue sasa kuwa ni wewe. Mtu unaestahili  kupata  upendo huo.

Hata hivyo, unapopenda , wewe ni mtu wa upendo, na sasa ni mtu.  Na kwa sababu watu wote  wanastahili,  unapowapenda wengine  na hapo utagundua uzuri wako kutoka ndani mwako.

Self-Care-Logo-Web-Edit JIFUNZE KUPENDA KWA UFAHAMU ZAIDI, KWA NDANI  ZAIDI, KWA UKWELI

Jifunze kupenda kwa ufahamu , kwa ndani zaidi na kwa ukweli.

Previous UMEWAHI KUDANGANYWA? UTATAMBUAJE NIA NA MBINU ZA UDANYANYAJI
Next SIFA 5 ZA MWANAMKE MWENYE MVUTO WA JUU

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.