Jikung’ute Mavumbi Uondoke


 

Huenda kuna kitu kiilikukamata ukawa huwezi kusogea  mahali ulipo,

Amka sasa jivike nguvu zako Ee mwanadamu kwa maana tangia sasa hataingia ndani mwako mtu mbaya anayekuharibu.  Jifungulie vifungo vya shingo yako ulivyofungwa na watu wabaya.

Maana Bwana asema hivi, Uliuzwa lakini sasa umekombolewa  bila fedha , maana  Mungu aliona mateso uliyonayo ya kuwa ni makubwa , ameamua kukukomboa  kwa mkono wake mtakatifu machoni pa mataifa yote na Nchi zote za Dunia zimeuona wokovu wake.

Ondoka sasa kwenye vitu vichafu, uwe msafi ili Mungu akubariki na kukutunza kwenye maisha yako, Lakini kumbuka kuwa hutaweza kutoka kwa haraka wala hutaweza kwenda kwa kukimbia , kwa maana Mungu yupo pamoja na wewe ili akulinde.

Tembea kwa Busara ili  upande kidogo kidogo, utukufu hadi utukufu, ukitumia muda wako vizuri, kwa kumpendeza Mungu wako, huku ukitenda haki .

Ni nani aliyesadiki habari hii, Mkono wa Bwana amefunuliwa nani,  Ni wewe mtu wa Mungu. maana alikuwa mbele yake kama  mche mororo na kama mzizi katika Nchi kavu.

Yeye hana umbo wala uzuri, na tumwonapo  hana uzuri hata tumtamani. Alidharauliwa na kukataliwa na watu kwa ajili yetu, mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko, kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao. Alidharauliwa wala hatukumhesabia  kuwa kitu.

Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu, lakini tulidhani amepigwa, amepigwa na Mungu na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu , alichubuliwa kwa maovu yetu , Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake.

Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona kwenye ndoa zetu, biashara zetu, mahusiano yetu, Huduma zetu, Kampuni zetu, magonjwa yetu yote, hasira zetu, umasikini wetu,  na kila aina ya ubaya wa Dunia hii.

Mungu aliweka juu yake maovu yetu sisi sote.

Anza kujichunguza Upya , Mpende Mungu kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote, kwa Akili zako zote na kwa Roho yako yote. Mpende Jirani yako kama nafsi yako.

Chagua uzima ili uishi. Ni uchaguzi wako .Lakini Mungu amesema chagua Uzima ili uishi.

14-14 Jikung'ute Mavumbi Uondoke

Nunua maji ya uzima bila fedha, divai, maziwa bila fedha. Kula kilicho chema. Ifundishe nafsi yako kwa unono wa neno la Mungu.

KUMBUKUMBU LA TORATI 8:18. Bali utamkumbuka Bwana Mungu Wako Maana ndiye Akupaye Nguvu Za Kupata  Utajiri, Ili alifanye Imara Agano Lake aliloagana na baba zako kama hivi leo.

Pasaka Njema.

Previous Sielewi Kwa Nini Umeacha Kunitumia Ujumbe
Next Siri Kubwa Za Mafanikio Kwenye Ndoa, Mapenzi, Kazi, Biashara

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.