Jinsi Ya Kulea Ukuaji Wa Kiroho


spiritual-growth-articles Jinsi Ya Kulea Ukuaji Wa Kiroho

Yule mtoto akakua ,akaongezeka nguvu,amejaa hekima , na neema ya Mungu ilikuwa juu yake

Kulea mahusiano yako na Mungu inatakiwa  kujichunguza  ndani ya roho yako. Unaweza kuwa na dini  bila ya kuwa wa kiroho. Sasa utawezaje kulea roho yako?  fuata mbinu hizi zikusaidie kuwa karibu na Mungu.

Soma kitabu kupata hekima na maarifa kila siku.

Maisha yetu huwa yanachanganya , hasa tunapokutana na majaribu na kutufanya kukosa njia . Wakati matukio mbalimbali ya  matatizo au masikitiko yanapotokea katika maisha yetu . Tunaweza hata kuanza kumlaumu Mungu kuwa Hayupo pamoja nasi, yaliopita au yaliopo. Tunapojisikia hivi , tunakuwa  mbali na uwepo wa Mungu.

Uwepo wa Mungu katika maisha yetu unatusaidia kufikia ukweli na kuwa na Amani  kutokana na mipango yake mwenyewe. Njia nzuri ya kujifunza lugha yake ni kuwepo katikati yake. zungukwa na Upendo wake, hapo utajisikia Amani na utakua kiroho.

Jitahidi kuwa na Muda na watu wanao amini.

spiritual-growth-1024x536 Jinsi Ya Kulea Ukuaji Wa Kiroho

Tunapowajenga wengine, imani zetu huendelea kukua, Kuna njia nyingi za kujiunganisha na watu wengine  ili kushirikishana imani,  kama vipindi vya kujifunza, kwenye makundi ya vijana , mikutano,  kushiriki uimbaji, kushiriki vipindi vya kanisani. kuhudhuria ibada za kanisa.

Uwe na maombi ya kila siku ili kupata neema  ya Mungu

Hakuna njia sahihi au mbaya ya kuongea na Mungu.  Maombi ya kawaida yanatuweka karibu na Mungu Na pia hutufanya tuwe na Amani. Mwambie maswali yako, woga ulinao, furaha, na kuhangaika kwako. Kuomba ni njia nzuri ya kupata uzoefu wa upendo wa ndani. Mwambie asante uweponi mwake,  omba kwa mwelekeo,  haijalishi ni tatizo gani, omba mara nyingi utakuwa karibu naye kwa imani.

Tunza moyo wako kama  bustani.

Fikiria unavyotunza bustani ya mboga, Unapopanda mbegu vizuri na kumwagilia maji vizuri na kuweka mbolea. Kwa uvumilivu  matunda huja . Lakini kama ukipanda  mbegu yako vibaya  na usipoweka umakini jua litakausha na hutapata matunda uliokuwa unatarajia. Ndio hivyo hata katika kulea roho yako, kama utajali na kutunza kwa uzuri , imani yako itakuwa na kukushangaza. lakini ukiwa hukutunza utabakia na ganda lake tu. Imani yako na roho yako vinahitaji  utunzaji na utii.

Utakuwa na mahusiano mazuri na Mungu kama ukiwa na muda na yeye, kujitunza na kujipenda kwako ndio  kuwatunza wengine na kuwapenda wengine na huko ndio kumuhudumia Mungu, Hapo utweza kuwepo katika uwepo wake kila siku .

 

Previous Kukimbiza Furaha Haitakufanya Kuwa Na Furaha.
Next Sababu 4 Mazoezi Ya Cardio Yanahujumu Lengo La Uzito Wako

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.