Jinsi Ya Kutambua Sumu Za Watu Binafsi Na Sumu Za Kwenye Mahusiano


http-2F2Fo.aolcdn.com2Fhss2Fstorage2Fmidas2Fc655dfada6273694dbd44063370adda52F2048493182F108004829 Jinsi Ya Kutambua Sumu Za Watu Binafsi Na Sumu Za Kwenye Mahusiano

Jifunze jinsi ya kuepuka sumu za watu binafsi  ili uwe na furaha katika maisha yako.

Hivi karibuni nimekuwepo kwenye  mahusiano mabaya  ambayo nilijaribu kujiingiza .Kutoka kwa marafiki zangu, pamoja na wafanyakazi wenzangu na hata kwa baadhi ya ndugu zangu

Nimeshuhudia mambo mabaya mengi, tabia mbaya zenye kuumiza katika baadhi ya  watu  katika maisha, kwa mara moja na zaidi. wanaweza kuonekana kama kweli wanakujali. lakini unaweza ukaona huruma unaposikia maneno yao  mabaya na ya kuumiza . Kitu ambacho unaweza kuchukua hatua ya kuachana nao.

Katika safari tuliyonayo, tunajifunza mengi. Unaweza kuanza kufahamu kwa kuona viashirio, kata mawasiliano na watu wabaya,  na kitu cha muhimu ni kuwasamehe na kuwaachilia. wasamehe watu wote waliokuumiza. hata kama hawana ufahamu na walichokifanya. kuachilia ni kujipenda, na kusonga mbele kwa kitu kilicho bora zaidi katika maisha yako. kwa wale ambao bado wanashangaa na wamezungukwa na watu sumu. Nakupa somo hili la kisaikolojia  kuhusu  kutambua watu sumu na tabia zilizo za sumu  epukana nazo.

Mahusiano ya watu sumu na wenye tabia za aina hio , watakusababisha kupatwa na  magonjwa ambayo hayana tiba. utajikuta huna afya kila siku. utakuwa mtu usieeleweka . kwa maana nyingine utazalisha chemicals mwilini mwako.

Wengi tumekuwepo katika mahusiano mabaya kulingana na muda hadi muda mwingine katika safari  yetu ya maisha. Sumu hii huja kutoka kwenye  majina yanayoitwa, Kunyanyaswa kimwili, kudanganywa, kupiga umbeya,  na mengine. Matokeo hayo huja kwenye mahusiano mabaya, huenda wanafamilia, au marafiki, au katika sehemu ya kazi. Mahusiano haya mabaya yanaweza kuharibu na kuacha madhara ya muda mrefu ndani yako.

Couple-not-communicating Jinsi Ya Kutambua Sumu Za Watu Binafsi Na Sumu Za Kwenye Mahusiano
Couple not talking after a fight

Kwa Nini Ni Muhimu

Mahusiano sio tu ya watu wawili kwa ajili ya kufanya mapenzi yao kama mwanamke na mwanaume. Mahusiano ni ya watu wawili ambao  watakuwa pamoja katika safari yao bila ya kutarajia kitu chochote . wanaweza kusaidiana kwa mambo mengi katika kuelewana kwao. Na kujikuta wanasafiri wakiwa salama katika maisha yao. Na hayo ndio mahusiano mazuri.

Kama wanadamu , tumekuwa tukijihusisha na mahusiano mabaya bila ya kujua.  kujiingiza kwenye mahusiano sumu, utakutana na hasira,  huzuni, misongo, na matatizo mengi ya ndani. Ni muhimu kutambua  dalili zinazotuonyesha kuwa tupo mahali pabaya, ili tuweze kujiondoa kwenye hisia ambazo sio za muhimu ndani mwetu.

Wanawafanyiaje watu wengine?

Utafahamu, ni rahisi. Tazama watu walio karibu yake.  Anaongeaje kuhusu familia yake, marafiki zake, wafanyakazi wenzake, wazazi wake? Anakuwa na ugomvi na watu? utaona kila mara anakuja kwako analalamika kuhusu watu wengine. kama wamegombana na rafiki wa kiume au wa kike, au hakuweza kuelewana na mama yake , anahitaji kama kuondoa hali yake ya kuchanganyikiwa kwako.

Kama ni hivyo chukua hatua mbele au amua kuyachukua hayo na kumsaidia kama itawezekana. lakini maamuzi mazuri ni  kuchukua hatua mpya kama hawezi kubadilika tabia yake.

Utawezaje kushughulikia matatizo haya?

Watu wengi hawawezi kufurahia kushughulikia matatizo. Inaweza kuwa ngumu , na ukakosa mawasiliano mazuri kwenye hisia zako, itakufanya uwe na mazingira magumu unapokuwa hukubaliani na hayo. mtu anayekuwa mgumu kuleta matatizo yake ili  kuyatatua, anayekataa kuwasiliana au kuomba msamaha  kwa ajili ya vitendo vyake. Halafu anakuongelea vibaya. hio ni dalili mbaya. mtu anayekujali kweli  atakuwa wazi kwako. utaweza kujifunza mengi kwa mtu ukiwa mchunguzi, jinsi gani anashughulikia matatizo.

Mkiwa pamoja unajisikia Vizuri?

tiess Jinsi Ya Kutambua Sumu Za Watu Binafsi Na Sumu Za Kwenye Mahusiano

Mkiwa pamoja na mtu huyo anaongea kuhusu yeye  muda wote?  anawasema wengine vibaya kwa umbeya?  Unajisikia vizuri kuwa naye muda huo au unajisikia kuboreka?  unatembea kwenye ganda la yai kwa kuwa unaogopa kumuudhi mtu huyo?  unajisikiaje kwa kila kitu. kama unajiona kuwa na matatizo kuliko kuwa na furaha. UNahitaji kuweka mipaka na chukua hatua ili kujilinda wewe mwenyewe. Kitu kizuri zaidi jipende mwenyewe.

Tazama kama anakuthamini. anadharau mahitaji yako na maombi yako?  anakupa hisia mbaya? na kujikuta huna furaha naye unapokuwa kwenye hali mbaya  , anaona umuhimu wa kuwepo karibu yako? Angalia dalili hizo ni za hatari.

Dalili za Hatari kwenye mahusiano sumu  ni;

-Udanganyifu

-Kukataa kushughulikia matatizo

-kutokuomba msamaha

-Wasiwasi

-Ubinafsi

-Aina yeyote ya uharibifu

-Kutokubali makosa

-Kulaumu wengine

-Kutawala wengine

-Uongo

Kukataa kusikiliza maoni yako

Hakuna suluhisho rahisi.

Kutambua na kukubali kuwa upo kwenye mahusiano ya sumu ni ngumu,  Kama jinsi watu walivyo vipofu kwa mapenzi na furaha ya muda.  kwa kufikiria kuwa hawawezi kuwa peke yao au kuogopa upweke wa kuishi bila rafiki, ndugu au mpenzi. wanaweza kuwa wametambua tatizo lakini  wanakuwa hawawezi kuamua kitu sahihi kutokana na woga huo.

Kusema kweli watu wengi wanakuwepo kwenye nyumba ambazo ni sumu kubwa katika maisha yao, wanajikuta wanashindwa kukubali mahusiano ya mapenzi, kwa sababu  wameyazoea.  kwa sababu hii, wanaishi kwa mazoea. watu wengine wanaona kwa urahisi  kuwa kuna tatizo , lakini mwenye kuwepo kwenye tatizo ni ngumu kutambua hilo. sio rahisi kumshauri kuondoka katika tatizo. itakuwa ni woga mkubwa kwao kutaka kuondoa hali hio. Kukubali hali ya mapenzi bila ya hisia , wanavuta sumu nyingi zaidi, kitu ambacho wamekizoea. Wanaweza hata kuamini kuwa wewe unayewaambia ndio sumu yao, kwamba unawaambia kuwa wao ni wajinga, wabaya, hawastahili, hawana thamani au vingine.

Habari njema ni kwamba  hizi sumu zinaweza kuondolewa kwa tiba,kujipenda, kuwa na mipaka, kujenga mahusiano mazuri na kuwepo kwenye makundi ya msaada  ya kujenga akili  mawazo na hisia zako.

Kama umependa hii makala like kisha share kwa wengine

Previous Hatutaki Kisasi , Tunafikiria Tu Tunachokitaka
Next Misemo 10 Ya Mapenzi Ya Kweli

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.