KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARIBU NA MUNGU


Depositphotos_2097109_original-1024x683 KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARIBU NA MUNGU

Huu ni mwendelezo wa nguvu ya nia ya kumtafuta Mungu , kwa wale wenzangu mnaopenda kufanya uchunguzi kama watoto wadogo wanaotaka kufahamu kila wanachokutana nacho. kanuni hizi zimehakikiwa na wengi ,watu ambao wametumia  wameona faida zake.

1.Fahamu Nia Yako.

Nia yako iwe upande wa roho yako , lakini mafuta yanayofanya  nia yako isogee iwe ni Hatima yako. Usipende kuona watu wanapata shida , usifurahie matatizo ya watu,  usichukue kitu ambacho sio chako. nia mbaya unaweza kuzitambua kwa kuhisi kama umeunganishwa nazo. kuhisi woga wa kutokuwa na kitu kikubwa,  hasira na udhaifu wa mambo kama hayo.

Uwe makini katika eneo hilo ili uwe na nia ya kawaida , nia ya chini , nia ya  upendo.

2.Weka Nia Yako Iwe Juu.

Kusudi la kuwa mtakatifu  na kuona miujiza mbalimbali , kwa nini isiwezekane?  sheria hio hio wanayotumia wengine hata wewe unaweza kutumia , kama unafahamu kwamba  mafanikio ya kukua ndani yanahusiana na siri.  Itake hio siri kwa haraka uwezavyo.

Mwanzo wa siri ni maono, ona  miujiza inayokuzunguka , na hio itakurahisishia  kuona miujiza mikubwa ikitokea na kukua.

3.Jione Kuwa Uko Ndani Ya Mwanga.

Kila mara jione kuwa uko katikati ya mwanga, ukiwa umezungukwa na  malaika  wale wafanyao kituo kila mahali.

4.Waone Wengine Wako Kwenye Mwanga Kama Wewe.

hiphopcongregation KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARIBU NA MUNGU

Usipende kuwagawa watu , ya kwamba hawa ni wabaya, na hawa ni wazuri, wote hao wako kwenye mwanga . kumbuka kuwa kila mtu  anafanya awezalo  kutokana na kiasi cha ufahamu wake  kumtafuta Mungu.

Kumbuka si wenye mbio washindao katika michezo, wala  si walio hodari  washindao vitani, wala si wenye hekima  wapatao chakula , na wala si watu wenye ufahamu wapatao mali,  na wala si wenye ustadi wapatao upendeleo. lakini wakati wa bahati  huwapata wote.

5. Imarisha Nia Yako Kila Siku.

Majaribu ya kiroho ni mengi, kila siku katika maisha  ni matatizo.kinachotakiwa ni nidhamu  ya kujikumbusha  kila kukicha  kwenye  kusudi lako mwenyewe la kiroho. watu wengine huandika nia zao , wengine hutafakari, wengine huomba lakini bado haitoshi,  tafuta  kituo chako, tazama kwa karibu , usiache, hakikisha roho yako iko sahihi  ndani yako .

6.Jifunze Jinsi Ya Kujisamehe

Kuna mambo mengi  ambayo tunaona kama tuko sahihi, lakini sio kweli, jisamehe , kuwa mkweli bila ya kusikia hatia  ndani yako , usijifanye mtakatifu , bora ubinadamu wa kweli.

Usiwe mwenye haki kupita kiasi, wala usijiongezee hekima mno, kwa nini kujiangamiza mwenyewe? ni vizuri ukishika neno hilo, kwa kuwa mtu yule amchaye mungu atatoka katika hayo  yote. usiwe movu kupita kiasi ,  wala usiwe mpumbavu, kwa nini ufe kabla  ya wakati wako?

7.Jifunze Kuachilia

Mara nyingi hatuna usahihi katika hiki kitendawili cha kuwa wa kiroho, maisha yanabadilika , jiandae, acha yaliopita , imani mawazo na matendo . kumbuka kila hatua  kuna maisha mazuri na ni tofauti yamewekwa na Mungu.nia yako ndio inayojua haya  kuwa ni wakati gani wa kusogea, na utakapogundua usisite  kuachana na yaliopita.

8.Fahamu Utakatifu Ni Nini

Kuzama ndani ya Hazina hii  itakusaidia  kufungua moyo wako , na Ulimwengu wa  watakatifu  utakuwa ni mbolea  ilio sahihi.

9.Ruhusu Mungu Achukue Nafasi.

Kila unapohitaji kitu roho yako itakupa, ni kuamua tu kitu cha kufanya , halafu mungu  ndiye atakaye fanya sehemu yake   kwa ulaini.

hakuna mtu wa kukuambia kitu cha kufanya  mwenyewe, salimisha kitu fulani, kitu chochote  kwa misingi ya kila siku.

10.Kumbatia Yasiofahamika

Kuna kipindi huwa kinafika huelewi  cha kufanya ,  hapo unakuwa sio wewe kama unavyofikiria,  toka mwanzo ulikuwa hujui utambulisho wako , hakuna kilichoonyesha kuwa wewe ndio wewe. na wala hakuna kilichotenga ukweli na uongo, ilichukuwa muda mrefu kugundua  kuwa wewe ni nani.

ingawa inaumiza kuondoa hayo usiyoyapenda , lakini yale yasiofahamika yanakusubiri , maana mungu anaishi ndani ya hayo yasiofahamika . utakapokumbatia hio hali  kwa nguvu zako  utajikuta umefika  nyumbani  ukiwa huru.

Kama unazipenda makala zangu hizi , washirikishe wengi wajifunze.

Nakutakia  jumapili njema.

Previous KITU KIMOJA KIZURI CHA KUFANYA KAMA WEWE NI MJAMZITO
Next KUONYESHA NAKUPENDA. HAKUNA KUIBA

1 Comment

  1. […] ni upi,  kumbatia usichokijua,  halafu mruhusu Mungu afanye kazi yake. Somo makala hii  -KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARINU NA MUNGU  ikusaidie kufafanua haya […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.