Kanuni Za Imani Katika Matendo


faith-statement-pic2 Kanuni Za Imani Katika Matendo

Imani ni sasa. Ni sasa hivi.  fahamu maarifa yatendayo kazi na neno la Mungu. Unachokiamini unakisema. unakuza imani kwenye matendo sio maneno. Kuishi  kwa imani sio kwa kuona.

Pigana vita vizuri vya imani, ushikilie imani yako iwe ya kudumu. Imani ni vita. jenga imani yako , fahamu umuhimu wako kwa Mungu. Fahamu kusudi lako. kama kuna kitu unafanya  amani .

Imani Inatenda kazi katika  Maneno mawili.

Kiroho

Kimwili.

Kinachoonekana na kisichoonekana  katika kuona, kusikia, kunusa,  kugusa na kunusu.

Imani sio mazingaumbwe, ni kitu cha dhahiri, cha kweli, ina uthibitisho.

Imani inategemea maarifa uliyonayo ya Neno la Mungu.

Imani ina vitu vitatu

Ufahamu 

Imani yenyewe

Uaminifu.

Jinsi gani utapata Imani?

My-Promise-My-Faith_17_Social-Media_Blog Kanuni Za Imani Katika Matendo

Ni katika kusoma neno la Mungu. Kufikiria ukweli, kutendea kazi na kutafakari.

Imani inaamua mtindo wa maisha yako. Kulingana na imani yako unaishi. lakini iendane na neno la Mungu.

Imani  inabadilisha kikwazo cha aina yoyote, inaleta mbingu  Duniani. imani inapokuwepo, nguvu za Mungu zinakuwepo. imani ni ujasiri.

Imani ni SILAHA yako,  unapata maarifa zaidi, ufahamu zaidi ubora mkubwa zaidi, ikikaa ndani yako  unapata Hekima kubwa.

Toa imani yako katika kufanya kazi ya YESU, Kazi ya ADAMU.  Katika kukiri maneno yako. ipo nguvu katika kukiri . kuwa makini na maneno unayoongea kila siku. pambana na hofu au imani. utavuna utakachokipanda.

Vifungio vya imani ni Upendo,  Amani, furaha, uvumilivu, fadhili, wema, kiasi na msamaha, haki na shukrani.

Vizuizi vya  Imani ni Mashaka, Hofu na Dhambi.

Subscribe kupata makala mpya.

 

Previous Kuponya Na Kutibu
Next Hayakuwa Mapenzi Ya Kweli

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.