Kazi Nyingi, Pesa, Na Maisha Ambayo Nimejifunza 2017


xblack-woman-sitting-in-chair-thinking_n1y0t8hzg__F0000-750x375.png.pagespeed.ic_.cT_cA1N5LZ Kazi Nyingi, Pesa, Na Maisha Ambayo Nimejifunza 2017

1.Watu wengi huacha kusoma vitabu mara tu wanapomaliza shule, Usiwe mmoja wa wale. Kazi yako kubwa siku hizi ni kusoma, japo utaanza kushangaa kusikia hivyo.  Nasoma kazini,nasoma sehemu nyingine mbali na kazi dakika 30 mpaka 60. Nafurahia kujisomea.

2.Tawala Pesa Yako Kabla Haijakutawala.

Ni jukumu lako kutawala.Ndio .Wazazi wako huenda hawakuweza kufanya hivyo lakini wewe anza kufanya hivyo. Lakini haina maana kwamba hutakuwa na muda wa kujisomea na kujifunza mambo mapya. Kuna watu kwenye mitandao wengi sana ambao wanajitolea kukufundisha na kukushauri jinsi ya kutunza pesa na kuzitawala., Mara utakapojifunza misingi, bajeti, kutunza, kujenga uaminifu na kutunza kwa ajili ya baadae, nikiwa na maana kwa kizazi chako , utajisikia mtu mwenye nguvu kubwa.

3.Unaweza Kuwa Tajiri Lakini Ukawa Hauheshimiwi Na Watu.

Hakuna kiasi cha pesa ambacho kinaweza kuficha  utu wako, uhalisia wako. Hakuna pesa itavuta watu ambao wanaoona kabisa wataharibu maisha yao. kwa wenye hekima wanajua hili. Hakuna uhakika wa Furaha na Amani . Hakuna ukamilifu.

4.Ili Uwe Bora Kwa Kila Kitu, Ni vizuri Kufanyia Zoezi Kila Siku.

Hakuna nyakati hata moja ambayo itakubadilisha wewe kutoka kutofanikiwa na kufanikiwa  kwa ghafla. Vyovyote unavyochagua ni lazima ufanye kwa bidii kila siku kwa misingi iliyopo. Wakati mwingine utajikuta kushindwa, Wakati mwingine huna msukumo kabisa, Lakini unatakiwa kufocus kwenye picha kamili . Kama utakuwa unafanya kitu hicho kila siku lazima kitaendelea kukua.

5.Muda Ni Muhimu.

Kuna masaa mengi sana kwa siku. Panga masaa yako ya kazi, kupumzika, kumpa Mungu muda, Familia, na wengine. Naamka mapema saa 11 30 mara nyingi kila siku , Nafanya mazoezi mara tatu kwa wiki, nafanya meditation kila siku . Nikimaliza napata kikombe cha kahawa naandika makala nilioandaa jana yake kwa muda wa saa moja au zaidi. Najiandaa kwenda kazini. Napata chai nzito ili nisihangaike kula kula nje.  Nalala kawaida masaa 4 mpaka 5 kama sijachoka  nikiwa nimechoka naongeza saa moja ya kulala . kwa hio nalala masaa 6 ili kupumzika vizuri.  Napenda kufundisha , kuongea na watu. Kwa hio tumia muda vizuri.

6. Kuamka mapema.

Ni ngumu lakini lazima ujiwekee nidhamu ya kuamka mapema kila siku, itakusaidia kubalance kazi zako na kujenga ubongo wako kuwa na nguvu ya tofauti.

7.Ujasiri Sio Asili, Unahitaji  kuendeleza.

Kama miaka miwili iliopita nilikuwa sina ujasiri wa kufanya chochote zaidi ya kufanya kazi ya kuajiriwa. Lakini nilipoanza kufanya meditation nilianza kuona nguvu ya tofauti ndani yangu. Nilianza kuona ujuzi wa tofauti, Kusikia mambo ambao sikuwa nasikia hapo awali. Mara ya kwanza nilipoanza kutafakari nilikuwa naogopa sana, lakini nilijitahidi kuendelea.Kadri nilivyozidi kuendelea ndivyo urahisi ulivyokuja kwangu katika kugundua mambo mengi ndani yangu.

Lakini usihofu hakuna mtu mwenye kuwa na ujasiri wa kuzaliwa, kila mtu huwa nao wa fake tu. Nakuambia kuwa Fanya zoezi la kupata ujasiri wako wa kweli. Haijalishi ni mwoga kiasi gani.

8.Uvumilivu Ni Ufunguo Wa Mafanikio.

Mimi ni mtu mvumilivu sana. Naendelea kuvumilia. Mwaka huu nimejifunza kwamba hakuna lengo linalokuja kirahisi, lazima  kulipa gharama. Kupata ndoto yako, mshahara wa ndoto yako, Hata kuendeleza ujuzi wako, Ni kukazania vitu vidogo kwanza halafu ukiwa unalenga mambo makubwa pichani mwako. Hapo ndipo utaona muda ukienda haraka  na malengo yako yatakaribia kukufikia, ni lazima yafike.

9.Kujifunza mambo mengi katika kushindwa na kuanza kila siku.

Usitulie jaribu mambo mengi kwa kadri uwezavyo. Lipo jambo ambalo ni lako utakutana nalo kwenye juhudi uliyonayo.  Kumbuka kuwa kile ambacho kinafanya kazi nzuri kwa mtu hakiwezi kufanya vizuri kwako. Usikimbizane na ndoto za watu.

Mwaka huu nimeamua kufanya kitu ambacho nakipenda.  Najiendeleza kuongea na kuandika, Sauti yangu ya kuongea na kuandika pia. Haijalishi nitapata watu wangapi wanaosoma, Lakini kitu gani kinanipa furaha ninapokifanya. Naamini Mungu anatafuta mtu mmoja tu . Na mtu huyo ni mimi  Sijui wewe unasemaje.

10.Upekee wako ndio Nguvu Yako.

Hakuna mtu hapa Ulimwenguni ambaye atafanana na wewe. hii ni nguvu sio udhaifu. Kitu chochote kinachokupa furaha, amani . Pigania.

11.Furaha Iko Ndani Yako

Acha kutazama watu  wana nini, Ufunguo wa furahaha ni kujitambua. Pata muda wa kufikiri  kuhusu mafanikio ni nini kwako.  chukua kipande cha karatasi  na uandike list ndefu . anza kuvifanyia kazi . vyovyote ambavyo unaona unajilinganisha . Haupo kwenye mashindano na mtu yeyote ila ni wewe tu. Jiweke bora kuliko ulivyokuwa jana yake.

12.Sukuma Mipaka yako.

Jitahidi kulipa madeni uliyonayo. Jiwekee akiba zaidi. Usinunue vitu ambavyo havina umuhimu kwako. Usijiumize kwa vitu visivyo na umuhimu. Weka mipaka yako vizuri na utaona matokeo.

13.Zawadi Kubwa Ambayo Utaweza Kumpa Mtu Ni Usikivu.

Miaka ya leo ina mambo mengi, Smart phone inatawala maisha ya mtu. Popote unapokuwa unaongea na rafiki, familia, mke mume, Weka Simu mbali jihusishe kwenye mazungumzo vizuri. Kitu kikubwa ambacho utampa mtu ni kuona anasikilizwa.

14.Pesa Haiwezi Kununua Juhudi.

Kama nilivyoongea kwenye point ya juu . Kumpa mtu usikivu ni zawadi kubwa kuliko kumnunulia zawadi ya gharama kubwa.  Watu wanapenda kuona juhudi sio kumilikiwa. Kila mtu anaweza kufanya vitu hivyo lakini kama unajuhudi ni tofauti.

15.Jifunze Kwa Watu Tofauti Kwako

Ukiwa umefanya kazi sehemu mbalimbali, utakumbuka kila kitu ambacho umejifunza hizo sehemu. Lakini kitu kikubwa upande wangu nimejifunza kusikiliza watu ni vizuri kuliko kumkatisha mtu tamaa. Hata kama unapita porini ukiona ndege wanakupigia kelele lazima ujifunze wanakutaka ufanyeje , huenda unaekekea sehemu ya hatari. Jifunze kwa watu ambao unaona kama hawana uelewa, lakini ndani yao kuna hekima unaweza kuipata.

16.Wekeza kwenye Uzoefu Sio kwenye Vitu.

Fanya kitu unachokipenda kila siku. Tafuta mahali hicho kitu kilipo kajifunze, Usipende kuwa na vitu ambavyo hujui vina maana gani maisha mwako. Tafuta uzoefu kwanza, tafuta kufahamu , Tafuta kujifunza.

17.Kujifunza Kuhusu Pesa Ni Rahisi . Lakini Kuelewa Hisia Zetu Ni Taabu Sana.

Thamani ya mtu,Tabia ya mtu na mtindo wa maisha ya mtu hata hivyo ni mtihani tu. KItu cha thamani kubwa ni Uelewa wa mtu. Pesa ni kwa ajili ya Ulinzi wa mtu kwa akili ya kibinadamu sio ya Mungu.  Kwangu mimi naona kama mtu angeona maisha kwa uelewa kwamba anaishi vizuri akiwa na amani, upendo, na ana chakula na mavazi  , kitu ambacho hawezi kukosa, akiangalia kuna wengine hawana afya kama ya kwake,  hawana macho, miguu, mikono , wengine aliokuwa nao hawapo tena, Huko ni kuelewa.

Hata hivyo haya ni baadhi tu ya masomo ambayo nimeweza kujifunza mwaka uliopita. Bado tuna miezi mingi mbele yetu , tuangalie ni kitu gani kitatufanya tujifunze ili kukamilisha mwaka huu 2018. Ni vizuri kama utaepuka madeni, uwe huru , Fanya kitu unachokipenda na penda hicho unachokifanya.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Kitu Gani Cha Muhimu Sana Katika Maisha Yako Mwaka Huu
Next Usiseme Eti Kwa Sababu Mama Amepitia Mahusiano Mabaya Na Wewe ...Hapana

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.