KITU CHA KUKUSAIDIA UNAPOPATA UPWEKE WA KUZIDI KUTOKANA NA TALAKA ULIOPATA


dreamstime_xl_10073739-1024x683 KITU CHA KUKUSAIDIA UNAPOPATA UPWEKE WA KUZIDI KUTOKANA NA TALAKA ULIOPATA

Nyenzo tatu  za kukusukuma kuondokana na maumivu na kuweza kusonga mbele.

Fatuma amekuwa mpweke tangu alipoachana na mume wake mwaka uliopita.

Aliniita baada ya kusoma makala moja kuhusu jinsi ya kupambana  na upweke. Alisema  kuwa ni vizuri kama nikiwaona wanawake wengine ambao wako kwenye mpito kama huu. Yeye wakati huu yupo katikati ,  tangu alipopata talaka na bado anasikia hali ya upweke.

Alisema kuna rafiki yake mwingine anapata ugumu kukutana na watu wengine wapya kwenye maisha yake. Na hii imekuwepo kwa watu wengi ambao wameachwa. Hata siku za leo. Karne hii  imekuwa ni ngumu watu kukubaliana na hali hii ya talaka. Ni ngumu sana. Jamii inaangalia sana  kufundisha ndoa, lakini haiwaangalii watu ambao wameachwa. Ni ngumu sana kama utachukulia hivyo na hali hii itazidi kuumiza wengi.

Kwa Fatuma hili lilikuwa jambo ambalo hakulitegemea katika maisha yake.Ndio maana iliongeza maumivu  makubwa ndani yake .

Nilichomshauri ni kujiunga na gym,  na kujitahidi kwenda maktaba kujisomea vitabu mbalimbali,  na atafute kazi ya kufanya badala ya kukaa na kufikiria jambo moja. Lakini cha ajabu kila akienda alinipa majibu kuwa kule kila mtu ameoa na hakuna mtu anayetaka kutoka na mtu ambaye ameachwa. Shida yake ilikuwa ni kupata mtu ambaye angekuwa naye muda  wa kudumu.

Familia yake ilimsaidia kwa kiasi kikubwa, badae walimwacha , na hana mtu wa kuongea nae 

Hali hii kwa kweli inanisikitisha kupita kiasi , Njia nzuri zaidi ya kuondokana na hali hii ni kujifunza kujipenda, kujifunza kujikubali, kujiheshimu, kubadili mtazamo wako wa kutengwa na kujiona kuwa unafaa. Wewe ni wa thamani , unaweza.  Fanya mazoezi, Fanya meditation, kula vizuri. utashinda upweke wa aina yoyote.

Au,

Kama wewe unasoma hapa na hujui ni wapi utaweza kukutana na watu wapya, Nakushauri uingie  kwenye mitandao. Kuna online dating, Au nenda kwenye mikutano, sherehe, kanisani, club. Inategemea na sehemu ambayo utaona uko  vizuri .

Zipo pia nyenzo muhimu ambazo zitakusaidia kuondokana na mpito huo na kuwa bora na kuacha kuona kama umetengwa.

1.Huzunika mpaka uone huzuni imekwisha.

Unapozidi kuikubali huzuni  ndio inapoanza kuondoka taratibu. Lakini ukianza kupigana nayo itazidi kujirudia kwako. Kumbuka kuingia kwenye mahusiano mapya ni wakati ambapo huna huzuni tena.

Kaa na huzuni yako kwa muda na itakuachia mapema.

2.Usikwamishwe na yaliopita kwa muda mrefu

Ingawa unahitaji kujihisi huzuni na hasira  kuwa ni sehemu ya mpito wako, Usivitizame  hivyo, unatakiwa kusonga mbele . Unatakiwa kuamka , ujikung’ute na kuanza safari mpya ya kufurahia maisha.

Kuna maisha hata baada ya kuachwa, kumbuka.

3.Omba msaada.

Hiki ni kitu cha muhimu sana ambacho utakifanya ili uweze kuondokana na maumivu  yako ya moyo.

Wale wanaohitaji msaada huwezi kwenda  kwa miguu yao  na  kumaliza  mateso waliokuwa nayo. Unaweza kujiunga na vikundi mbalimbali , unaweza kuwa na marafiki, Au mtu wa kwenda nae kuangalia movies, au unaweza kusafiri ili kubadilisha hali ya hewa.

Kujiunganisha na watu inakusaidia kusahau maumivu, na hata hutaona hali ya kutengwa na utajiona kama unaishi tena.

Tafuta jamii mpya.

-Nitamsamehe vipi mtu aliyenisaliti na kuniumiza moyo wangu

-Jiepushe na mambo yafuatayo 10 baada ya kuachwa

 

Previous HATUA 3 NILIZOCHUKUA  KUPONYA MWILI WANGU NA KUPATA AFYA.
Next JISAIDIE MWENYEWE , CHUKUA HATUA UNAPOONA MAPENZI YAMEKWISHA

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.