Kitu Gani Cha Muhimu Sana Katika Maisha Yako Mwaka Huu


43421-feeling-lost-1 Kitu Gani Cha Muhimu Sana Katika Maisha Yako Mwaka Huu

Tabia au sifa zipi  zinakusukuma jinsi ya kuishi  maisha Yako?

Kama mtu atakuuliza swali hili utalijibu vipi? Hili swali sio kuhusu mwaka mpya tu, ni kitu ambacho kinahusiana na undani wa maisha yako,  thamani yako, point of view, mtazamo wako wa ndani kabisa unaokusukuma wewe.

Kitu gani cha kukufanya uwe na furaha wakati wote , unapokuwa kazini, nyumbani, kwenye jamii yako, safarini, kila mahali. Kama ukiwa na jibu hili utajikuta na mafunuo mengi kuliko ambavyo ungefikiria.

Mfano. Viongozi wengi wana kiwango kikubwa kuridhika na maisha  pamoja na ustawi wao ni mzuri.  Wana malengo makubwa  ambayo wamepanga japo ni wazee, lakini vijana  wengi hawako hivyo. Viongozi wanaishi kama vijana wadogo wa miaka 25, ndani ya akili zao , japo wana miaka 80.

Turudi kwenye swali letu. Sifa zipi zinakuvutia wewe na zinakupa msukumo mkubwa katika maisha yako?  Hapa kuna baadhi ya vitu vinavyowezekana, vyenye ujasiri, vyenye wema , ukamilifu, usawa. kwa sababu tunaishi katika nyakati ambazo tunashambuliwa na taarifa nyingi, na nyingine zinatufanya kuwa na usikivu, zinatuokoa , zipo vizuri, zinalenga jinsi gani ya kukabiliana na  changamoto ambazo zinatulemea, hasa ukiwa kama kijana au kiongozi.

Jinsi gani utakabiliana na changamoto za maisha . Lazima uwe na vitu vinavyokuongoza. Nakushauri  kufanyia kazi hili neno ATTITUDE, kitu ambacho unatakiwa kufanyia mazoezi kila mara.

1.Heshimu maisha yako, undani wako. 

mwakaika-1024x768 Kitu Gani Cha Muhimu Sana Katika Maisha Yako Mwaka Huu

Utaweza kuheshimu maisha yako kwa kuwa mtu wa  kutumia muda vizuri. Hasa katika kutafakari, maombi, kupata utulivu wa kipekee hata kwa dakika chache kila siku. itakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi .Lisha akili yako taarifa sahihi.

2.Fanya zoezi la Kusimamisha hisia mbaya.

Acha kutazama taarifa mbaya, achana na mitandao kama haikuletei faida maishani mwako, achana na vikao mbalimbali vinavyokufanya ukose muda wa kufikiri  ili kupata wazo jipya. Acha na tazama undani wako, moyo wako unakuambia nini.

3.Jizoeshe kuwa na utulivu.

Acha kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.  Fanya kitu ambacho kinaleta mabadiliko kwenye maisha yako kwa muda wa kutosha. penda utulivu. furahia kila unachokifanya mkononi mwako, na utambue ubora wa hicho kitu unachokifanya.

4.Jijengee Furaha, Amani .

310756_264985573551957_572923187_n Kitu Gani Cha Muhimu Sana Katika Maisha Yako Mwaka Huu

Pata Nuru ya uchangamfu, ukichagua  furaha na amani utapata upendo. Kila changamoto itakuwa ni ndogo kwako. Angalia wakati ambapo unaweza kuwa mchangamfu kitu gani huwa kinatokea, tambua ni jinsi gani mwili huwa unarelax, pumzi zako na akili yako. ni zoezi rahisi lakini linakupa mafanikio makubwa na ya miujiza mikubwa.

5.Kuwa mtu wa Shukurani.

Shukuru kwa kila jambo. liwe zuri au baya. unaweza ukakutana na vipengele vigumu kwenye maisha yako, na ukasahau kushukuru jinsi gani kila kitu Mungu amekiweka kiwe hivyo.Shukurani inaweza kuwa ni zoezi zuri,  litakusaidia kuwa na upole na kutambua nyakati mbalimbali katika maisha. Sema asante kwa afya uliyonayo, kwa wema Mungu anaokutendea, Kwa uzuri wa hali ya hewa.

Zoezi hili litakuwa rahisi kwako kama utaanza kumkumbuka Mungu kila ikifika saa kamili. haya ni mashariti madogo, kuliko kama ungeenda kwa mganga wa kienyeji. Achana na maombi ya kulalamika, kusikitika, kusononeka, kulaumu, kusema Mungu mbona mimi, Mbona umeniacha. Anza leo zoezi la kumkumbuka Mungu kila inapofika saa kamili ili akupe nguvu ya kujenga sifa ya ndani yako . sifa hio ndio ambayo itakusaidia wewe katika kila sekta ya maisha yako. Mpe Mungu dakika moja tu  kwa kila dakika 60. ni mbegu unapanda.

Omba Mungu akupe Roho ya Hekima, Maarifa , Uweza,Ufahamu , Roho ya Ushauri, Roho ya kumcha  yeye.  Muombe MUngu akusaidie uwe na Upendo , Amani, Utu wema , Fadhili, Uaminifu, Upole, Uvumilivu, Nidhamu ya Muda, Na uwe na kiasi kwa kila unachokifanya. Hakuna mahali utashindwa endapo ndani yako utakuwa na sifa hizi. Ukitumia muda vizuri hutatenda dhambi.

Hakuna kitu ambacho kinakuja kwa urahisi maishani kinachoweza kudumu. Lazima ufanyie kazi kwa bidii ndipo utapata kitu cha kudumu. kwa hio anza leo. Mkumbuke Mungu, Msifu Mungu, Mshukuru Mungu kwa kila kitu .Kila inapofika saa kamili mpe Mungu dakika moja tu, msifu, mshukuru. uwe mtu wa toba kila mara.

Haya ndio maisha ambayo unatakiwa kuwa nayo kila mahali unapokuwa. kazini, kwenye ndoa, kwenye jamii. hakuna mahali utashindwa. sikuambii ujaribu. fanyia kazi.

Upendo na Baraka nyingi ziwe kwako.

Subscribe kupata makala mpya kila siku.

 

Previous Uko Tayari Kujaribu Kitu Kipya?
Next Kazi Nyingi, Pesa, Na Maisha Ambayo Nimejifunza 2017

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.