KITU GANI KINAFANYIKA KUHUSU SIKU YA IJUMAA KUU?


Msamaha

 

Ni nini ijumaa kuu na kwa nini tunaita Ijumaa kuu, Wakati ni kukumbuka kuhusu kuteswa na  na kuhangaika kwa  kifo cha Yesu?

Kwa wakrito, ni siku ya maombi kwao , ni siku ya  kusherehekea kwao kutokana na  imani   iliopo kwenye historia  duniani kote. Toka kipindi Yesu Alipokufa na kufufuka, Wakrito   wanautangaza Msalaba   na  kufufuka kwa Yesu  kwa ajili ya kufanyika upya ndani ya mioyo yao. Kwamba  Yesu alikufa kutokana na dhambi zao, alizikwa na kufufuka siku ya tatu. Na ahadi hii ilitimia  kutoka kwa  1 Wakoritho 15:3

Katika siku hii ya Ijumaa kuu tunakumbuka Yesu alipokubali kuteseka kwa ajili ya wengi   1 Yohana 1:10 . ilifuatiwa na Pasaka  ambayo ni kusherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo. Kuonyesha ushindi kutokana na kifo  cha dhambi na  ikiwa na maana kwamba kila atakaye mkubali  atafufuka  baadae pamoja na yeye kwa imani.  Warumi 6:5

Kwa nini hii siku inaitwa Ijumaa Kuu wakati ni siku ambayo Yesu aliteswa kwa sababu ya Dhambi za Wanadamu badala ya kuitwa  Siku mbaya?  Au kitu kingine ambacho kingefanana na hicho. Ingawa kuna wengine wanaita siku ya masikitiko, Siku ya furaha,  siku ya kweli, lakini kubwa ya hayo majina ni Ijumaa Kuu. Wengine wanasema limetokana na maneno ya kizamani. Neno hili  linaonyesha kuwa liko sahihi kwa sababu ya yale mateso ya Yesu na kifo chake kilikuwa cha kutisha na kuonyesha kuwa ilikuwa ni mpango wa Mungu.

Kwa Ajili ya habari nzuri inabidi  kuwa na maana kwetu,  kwanza inabidi kuelewa  habari mbaya  ya hali zetu na imani zetu   kwa kujilaumu kwetu. Na Habari nzuri ni kutambua kuwa tumeokolewa na tumefanyiika upya katika akili zetu  na mioyo yetu  na kwamba hatutakuwa watumwa wa mawazo mabaya tena . tuko huru   na tumeona mwanga wa njia yetu.

Kwa njia hio hihio Ijumaa Kuu ni siku nzuri.Kwa sababu kama ilivyo siku yenyewe ,  inatisha. Itatokea kwetu baada ya kupokea  furaha  ya Pasaka. Kila kitu kibaya kimechukuliwa  na Yesu Ambaye alijitoa kwa ajili yetu  ili tuweze kupata msamaha  na kuokolewa kutokana na siku mbaya za masikitiko,  za mahangaiko na kukosa amani , kukata tamaa. Amefuta kwa damu yake msalabani. Warumi 3: 26

Msalaba ndio mahali ambapo tunaona  mateso ya Yesu  na  msamaha wa Mungu. Zaburi 85:10 . fadhili na kweli zimekutana,  haki na amani zimebusiana, kweli imechipuka katika Nchi, haki imeonekana, Na amani ya bwana iko pamoja nasi.

4431-crown-of-thorns_edited.630w.tn_-2 KITU GANI KINAFANYIKA KUHUSU SIKU YA IJUMAA KUU?

Ijumaa Kuu Inaonyesha kuwa ni wakati ambao  Ghadhabu na Rehema zilipokutana pamoja. Hii ndio maana ikaitwa Ijumaa Kuu.

Mstari wa biblia wa Ijumaa Kuu

Warumi  5:6-24 . unaona ni wakati sahihi, kwa maana tulipokuwa hatuna nguvu. Yesu alikufa kwa ajili ya   waovu, kwa vile ni shida mtu  kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki,  bali  Mungu alionyesha pendo lake yeye kwetu. Wakati mtu mwingine ni vigumu  kuthubutu  kufa kwa ajili  ya mtu aliye mwema. YEsu alikufa kwa ajili yetu .tulipokuwa tungali wenye dhambi.  Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika  damu yake, tutaokolewa  na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana  tulipokuwa adui tulipatanishwa  na Mungu kwa mauti ya mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tukaokolewa katika uzima wake; wala si hivyo tu , ila pia  twafurahi katika Mungu  kwa Yesu  Kristo,  ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho……

1 Petro 2:24  Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti; ili tukiwa wafu  kwa mambo ya dhambi,  tuwe hai kwa mambo ya haki na kwa kupigwa kwake  mliponywa.

Isaya 53:3-5  Alidharauliwa na kukataliwa na watu,  mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama  mtu  ambaye watu  humficha nyuso zao , alidharauliwa wala  hatukumhesabia  kuwa kitu.

Hakika ameyachukua masikitiko yetu , amejitwika huzuni zetu; lakini tulimdhania  ya kuwa amepigwa,  amepigwa na Mungu, na kuteswa.Bali  alijeruhiwa  kwa makosa yetu  alichubuliwa  kwa maovu yetu ; Na kwa kupigwa kwake  sisi tumepona.

Soma zaidi Mathayo 27:…kifo cha bwana Yesu.

Previous MAHITAJI 4 MAKUBWA YA MWANAUME NA MAHITAJI 4 MAKUBWA YA MWANAMKE.
Next MSAHAMA NI KWA AJILI YAKO KWANZA

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.