KITU KIMOJA KIZURI CHA KUFANYA KAMA WEWE NI MJAMZITO


122092-850x563-pmeditate KITU KIMOJA KIZURI CHA KUFANYA  KAMA WEWE NI MJAMZITO

Siku unapogundua una mimba , nafikiri huwa ni siku ya furaha hasa kwa wale wanaodhamiria kupata mtoto .  lakini hata wale ambao huwa mimba zinatungwa bila ya maamuzi yao.

Siku hizo za mwanzo , tuseme wiki ya kwanza ya pili na tatu  unafurahia  sana. Lakini baada ya muda mambo yanaanza kubadilika , mara hasira, mara  magonjwa ya hapa na pale. , wasiwasi mkubwa  na woga  ambao hujui unatoka wapi.

Kinachofuatia hapo ni kupima afya ya mama  na mtoto ili wakue wakiwa na nguvu na afya.  Maamuzi haya ya kupima ni mzuri  kwa ajili ya baadae , ili usishindwe kufanya kazi, usije ukazidiwa  wala kukosa usalama.

Katika kipindi hiki  kigumu cha miezi mitatu mpaka minne , kitu kizuri cha kufanya ni kutafakari , jaribu tafakari.   Utapata nafuu, hutawachukia watu, wala hutamchukia mumeo.

Hata kama umewahi kujaribu au hujawahi kabisa kujaribu zoezi hili ,  fanya maamuzi  sasa anza kujizoesha  tafakari , weka mkakati kila siku mara mbili  ikiwezekana hata mara tatu kwa siku ili uone utapata utulivu gani .

Jinsi gani tafakari itabadilisha maisha yako  kwa muda mfupi tu.

Baada ya siku chache kabisa utaanza kuona mabadiliko  ndani ya mawazo yako , hisia zako, msukumo wa damu , msongo, na wasiwasi  vitaondoka, na badala yake utaanza kusikia  ujasiri na furaha pamoja na mahusiano mazuri na familia uliopo. . utaanza kusikia amani ambayo hujawahi kuisikia , utakuwa ni mtu wa shukurani kila mara  kwa mumeo na , watu wanaokusaidia  na marafiki wa karibu .  Itakupa ujasiri , hutaogopa wakati unaokuja , utafurahia. Utajisikia karibu na mtoto wako  na wewe mwenyewe pamoja na mume wako.

 

Baada ya muda  utaona mabadiliko makubwa  . lakini ni pamoja na kula vizuri na kupumzika muda wa kutosha .

Baada ya kuona faida yake hio , sasa itakubidi uangalie nyuma ya pazia  kuna  kitu gani  cha ukweli kuhusu ujauzito na tafakari. .

Nakupa baadhi tu ya faida zake .

Tafakari inaongeza ukaribu wako na mtoto na mahusiano yako na mtoto pamoja na mume wako . maelewano yataongezeka, utakuwa unajisikia kuwa nae  kabisa na kuongea nae.

Utakuwa na ujauzito mzuri wenye afya , na utapata mtoto mwenye afya.  Utajifungua vizuri bila hofu.  Kwa sababu ya  tafakari,   mapafu yake  yatakuwa safi  na kupumua kwa urahisi na ataweza kutoa  sumu zote kwa urahisi  kutoka mwilini .

Itakusaidia kukulinda wewe na mtoto wako  kutokana na maradhi mbalimbali kabla na baada ya kujifungua na pia utapata mtoto mtulivu .

Kwa hio haitakusaidia kuelewa peke yako au kuwa mtu wa positive kila mara , lakini pia hata mtoto wako  atakuwa na uelewa huo. Atakuwa mwema, mwenye kujua huruma  kwa kadri anavyokua.

Uamuzi utakaofanya  sasa  wa kuanza  tafakari , utakuwa ni uamuzi  ambao hujawahi kufanya wala kusikia . Utakuwa mama mwenye hekima ya kumlea huyo mtoto na watoto wengine watakaokuja . Utaweza kuvuka  nyakati ngumu bila ya wasiwasi. Jitahidi kujua mbinu  nzuri za tafakari ili uweze kuwa na  akili yenye rutuba ya kutosha  wakati wa mpito wowote. Utabadilisha maisha yako.

Kama umeelewa  na kama una swali  usisite kuuliza nitakusaidia kadri niwezavyo.

Shirikisha wengi wajifunze.

Previous UKITAKA KUJENGA UAMINIFU KWA HARAKA, KUNA MAMBO 5 YA KUFANYA
Next KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARIBU NA MUNGU

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.