Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza Tatizo


EL-DOLOR-DE-LAS-PERDIDAS-Duelo-a-un-ser-querido-ncp6v0ruhohdxyrupl8skpp650t50kw9pe0q3xj92w Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza TatizoKitu cha mwisho ambacho watu wanahitaji wakati wa mahojiano au migogoro ni  katika kuingiza Upendo,  joto la upendo.

Kuonyesha upendo ni kitu pekee ambacho kinafunika mambo yote wakati wa migogoro mbalimbali.

Kitu ambacho nimekigundua ni katika kukumbatiana,  kumkumbatia   mwenza wako wakati mnapokuwa katika malumbano ya hoja yenu taratibu  inabadilisga hali  yote ya machafuko. ukimkumbatia mwenza wako wakati wa malumbano huwa  inaleta hali tofauti, haiwezi  kuwa kama siku zote ambazo umezoea. imegundulika kuwa inakuwa na hisia za kweli, mtu anaweza kujisikia vizuri zaidi kuliko ile kawaida ya siku zote, inaondoa  hali ya kuwa na shaka  lolote.

image-43344644-hug-image Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza TatizoMtu yeyote anapokuwa na stress , kama akikumbatiwa  vizuri na mtu ambaye ataweza kutumia muda wa kutosha kufanya hivyo, inamsaidia  mhusika  wa tatizo kuepuka kupata shinikizo la moyo

Nimegundua watu wengi wanapata tatizo la ugonjwa wa moyo na hata kufa kwa sababu ya kukosa mtu  maalum wa kumkumbatia anapokutana na changamoto ya mahusiano, hasa katika  malumbano mbali mbali .

Ukiona unapata shida  kama hio na wakati huo labda mwenza wako amekuwa hajielewi vizuri , jaribu kutafuta mtu mwenye Upendo na Ile Huruma ya Mungu.   Yaani   Love and compassion.

Love and compassion ni zawadi kutoka kwa Mungu, ni Neema fulani hivi mtu anapewa na Mungu, Ukikutana na mtu kama huyo , hata kama ulikuwa na maumivu ya aina gani , utajikuta unapona saa ile ile kwa ajili ya mguso ambao utapata  kutoka kwake.

Ni kama vile  umeme  unaingia kwa mtu  haraka na kuponya  kila kitu.

woman-hugging-a-man Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza TatizoKwa hio kumkumbatia mtu sio tu suala la kimwili, bali ni katika kuponya  nafsi ya mtu.kwa sababu magonjwa yote yanaanzia kwenye akili, magomvi yote yanaanzia kwenye akili ya mtu.

Pia kukumbatiana kunaleta ukaribu , uaminifu, na  kuleta ufahamu  wa kikomavu ambao ni wa kujali mtu, inaleta upendo wa kipekee, kujiamini,  urafiki na kuweza kufahamu silika ya mtu  ambayo itakusaidia kuwakumbatia watoto wetu,  wazazi wetu na marafiki zetu.

wapo watu tangu wamekua na akili,  hawajawahi kuwakumbatia wazazi wao, pia kuna watu ambao hawana tabia ya kuwakumbatia watoto wao. Hili ni tatizo kubwa ambalo nimeligundua mimi binafsi kuwa  ipo haja kubwa ya kukumbatiana  kila inapobidi, iwe ni mtoto , au mzazi au rafiki , hasa ukiona yupo katika hali ambayo sio ya kawaida.   Jitahidi kufanya hivyo utaona unamponya mtu kwa namna ya kipekee.

1D274907484375-today-hugging-141222-01.fit-760w Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza TatizoHug inaweza isiwe suluhisho la mara moja wakati wa tatizo, lakini kama ukifanyia zoezi  inaweza kusawazisha hali  mbaya kuwa nzuri.

je unatamani kujua  kama  una nguvu ya kuleta afya  kwa mwenza wako ambaye   anapatwa na shinikizo la moyo ?  uliza maswali, au nitafute  nikusaidie .  Una changamoto yoyote ya kimaisha, Biashara, Huduma, huna kazi kabisa, unajaribu kila kitu hakifanikiwi.

email yangu   lizzdavid@gmail.com

Usisahau,   Subscribe.

 

Previous Wakati Unapofika Wa Kubaki Mwenyewe, Ni Kwa Ajili Ya Kujiboresha
Next MAANDALIZI (PREPARATION)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.