Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.


107210986 Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

Siku hizi kuna malalamiko mengi sehemu mbalimbali, sio tu hapa nchini petu bali ni kote.Wanawake wamekuwa wakilalamikia wanaume kuwa hawatimizi haja zao, na kuwa  hawajali hisia za wake zao na mahitaji yao. Lakini pia hata wanaume wanahangaika huku na huku kutafuta namna gani wataweza kuondoa hili tatizo kubwa ambalo linaikumba sehemu maalumu ya maisha yao.

Wakati mwingine mwanaume anaweza asieleweke kuwa ana tatizo, ikaonekana kama  kuna mahali anamcheat mke wake.Kuna wengine hata uume wao hausimami kwa sababu ya vyakula anavyokula.

Lakini mimi nawaambia kitu, acheni kula mafuta ya  NGURUWE. au acha kabisa kula nguruwe.

Kula matunda leo, achana na vyakula  vile ambavyo  vimepikwa tayari kwa muda mrefu, readymade food.

Kula vitu ambavyo ni  vizuri kwa ajili ya afya yako, vinavyokupa nguvu ya kufurahia maisha.

Badala ya kula Donati , kula basi apple,  badala ya kula kipande kikubwa cha nyama, kula basi peasi.

Acha pombe, badala yake kula ZABIBU za kutosha.

Kila wakati ukitaka kula chunguza chakula chako kina virutubisho gani kwa ajili yako. endapo unahitaji kuiweka ndoa yako vizuri au kumridhisha mpenzi wako , uwe makini na mlo wako.

Wapo wanaume wanaofuatilia afya zao kwa umakini , na  wana mafanikio makubwa  sana, wamekuwa ni wanaume wazuri ndani ya ndoa zao na wanaheshimika na wake zao  na hata wapenzi wao. hapa kuna watu wana ndoa na kuna watu wana wapenzi tu si ndoa.

Wanasansi wamegundua hili kuwa wanaume wanaotumia matunda zaidi ndio wanaozidi kuwa na afya nzuri kila siku na ni wale wenye  kuwa na mahusiano mazuri ndani ya ndoa zao.

Nguvu ya asili iliopo ndani ya matunda inaleta uponyaji mkubwa kuliko unavyofikiri.

Kwa hio ukila matunda kwa wing wake na tofauti tofauti,  utazidi kuimarika zaidi kuliko  yule ambae hali matunda kwa wingi wake.  utakuwa na utekelezaji mzuri kwa mahitaji yenu wote . wewe na mwenzi wako .

Sasa basi tuone ni matunda gani hayo ninayoongelea hapa ambayo yana virutubisho muhimu vinavyosaida wanaume kulinda nguvu zao. hapa kuna list nakupa ya aina zake.

1.BLUEBERRIES

freshblueberry Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

2.STRAWBERRIES

Strawberries940x627 Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

3.APPLES

150919153848-01-popular-fruits-apples-super-169-1024x576 Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

4.PEASI

Pyrus-communis-pears_PUB0013436 Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

5.CITRUS FRUITS

2012-Citrus-Show-Fruit-Entries-1024x683 Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

6.KUNA CHAKULA AMBACHO SIO KAMILI LAKINI INASEMEKANA UKITUMIA KAMA DAWA NI CHAKULA KIZURI KWA  AJILI YA KUSAIDIA NGUVU ZA KIUME. NACHO NI .,

RED WINE.

aogwnng46h9iv2kergow-1-1-1024x640 Kuna Aina 6 Ya Vyakula Vinavyomsaidia Mwanaume Kupata Afya Na Nguvu Ya Tendo La Ndoa.

Kwa kuondokana na tatizo hili la kukosa nguvu, kula angalau kwa mlo mmoja kwa siku katika moja ya matunda hayo.

Asubuhi unaweza kula chai yako  na ukaongeza Zabibu  hapo.

Kitu kingine cha msingi  mwanaume unatakiwa kufanya MAZOEZI angalau hata mara 3 au 4 kwa wiki.

Pamoja na kuwa utakuwa bize kuhangaikia kupata nguvu za kukuwezesha kuponya ndoa yako, lakini pia utaweza kuepukana na maradhi ya  mashambulizi ya moyo, kisukari kiarusi na mengine.

Ndugu usisubiri eti uishiwe nguvu kwanza  za tendo la ndoa ndio uanze kula vyakula au kutafuta namna ya kurudisha nguvu zako, anza kula  hizo aina ya vyakula hapo juu. pia kumbuka kuwa kinga ni bora kuliko tiba

Nakutakia kila la kheri katika kujirekebisha  kuhusu ulaji wako. na jinsi ya kujipanga kufanya mazoezi, na maamuzi utakayochukua kwa ajili ya afya yako.

SHIRIKISHA WANAUME WENGINE KATIKA MAKALA HII na kama wewe unafahamu zaidi  , basi karibu utoe mawazo yako ili kusaidia wengine.

 

Previous Mawazo 6 Yenye Kuleta Maoni. Lakini Ni Mawazo yangu:
Next Alikaa Miaka 2 Bila Ya Kukutana Kimwili Na Mwanaume,Maisha Yake Yakabadilika:

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.