KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.


 

think7-1024x683 KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.

Kwa kawaida tu penye mahusiano ya watu wawili kuna maelewano ya kawaida , na kuna kutofautiana pale mmoja anapokuwa msaliti kwa mwenzake. Wenza wengi wamekuwa wapweke kwa sababu ya kusalitiwa na kuachwa. Pamoja na kutafuta watu sahihi kwa ajili ya maisha yao bado kuna tatizo hili kubwa linasumbua ndoa nyingi.

Maisha ya sasa hivi nimekuwa nikisikia wanawake wakisema vibaya waume zao kwa sababu ya hizi tabia za usaliti wao, wanasema ukigundua kuwa sio mwaminifu achana nae , na wala asikupotezee muda. Kuna wanaume wengi na wazuri tu nje kwa ajili yako tena ni waaminifu. Kwa hio hali kwa kweli sio nzuri.
Basi mimi ngoja tu nikuletee dalili za mwanaume ambaye sio mwaminifu.

1.Wale ambao hupatwa na hasira unapokuwa unaongea na wanaume wengine, na anafikiri unamsaliti.
Mwanaume ambae kila wakati anachunguza simu yako , kujua nini kimeingia , meseji au emails gani zimeiingia na kutoka wapi, kwa nani. Uwe makini nae huyo mtu , inawezekana anakusaliti, kwa nini anakuwa na wasiwasi na wewe, anafikiri kuwa unafanya kama yeye anavyokufanyia. Chunguza utaona.

2.Wale wanaume wanaolalamika kwa kitu kidogo tu basi analeta mlolongo wa mambo mengi ili uonekane kuwa umekosea.

scratching-head-pi_2895834d KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.
Wapo wanaume ambao hawataki ufuatilie mambo yao ya siri, lakini hapohapo hupenda kujua kila kitu wewe unachokifanya kiwe wazi kwake. Angalia hapa.
Endapo kila unapotaka kujua kitu kuhusu yeye, jibu linakuwa Jali mambo yako. Na kila ukijaribu kudadisi huwezi kujua anashinda wapi na kina nani, hicho kitu sio utani ndugu yangu lazima uwe na wasiwasi, lazima kuna kitu kinajificha.

3.Mwanaume anayependa kutoka na wewe kwa sababu tu wewe ni mzuri.

beautiful-girl-Cool-Wallpaper-Beautiful-Picture-1024x640 KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.

Aina hii ya mwanaume hupenda kuonekana mbele za watu kuwa yeye ni mshindi sio kuwa anakupenda, yuko nawe kwa sababu fulani, na hakujali, hana muda na wewe, na hata akikuoa lazima atakusaliti tu, utakuwa mlinzi wa nyumba na mama wa kulea watoto , hutafurahia maisha dada.

4.Yule anayekuona kama adui yake. Huonyesha kama rafiki yake tu mbele za watu.

c09efe61640af758_shutterstock_76299898.preview KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.

Mwanaume ambaye ndani anaonyesha mapenzi lakini nje hataki watu wajue kuwa nyie ni wapenzi bali ni marafiki tu, ukizingatia mmekuwa nae kwa muda mrefu, ipo sababu ya kufanya hivyo. Mwanaume mwenye kukupenda kwa dhati atataka kila mtu aelewe kitu kinachoendelea kati yenu.

Ina maana kama hataki kujionyesha basi hakupendi na ana kitu sio bure kwa nini anaficha.

5.Mwanaume anayeonyesha ukaribu kwa watu na marafiki kuliko kwako.

Wale wanaume ambao huwa karibu na marafiki kuliko wewe kunakuwa na jambo linaloendelea , ni lazima kuwa makini. Mwanaume yeyote mwenye kukuthamini , kwa hali yeyote ile ni lazima awe upande wako , na kila anachofanya atakushirikisha baadhi ingawa sio yote. Tena huwa makini zaidi ili usipitwe na kitu chake anachofanya.
Kwa hio kuwa makini na hao rafiki zake , hasa wale wa kike. Fanya uchunguzi kila anapoondoka na huwa anakuwa wapi na kina nani.

6.Mwanaume ambae hakumwacha kabisa mpenzi wake wa mwanzo.

Keep-Your-Man-From-Cheating-Guy-And-Woman-Holding-Hands KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.

Aina hii ya mwanaume hujionyesha kuwa yupo nawe kumbe bado anazo element za upendo kwa yule wa kwanza. Kama hakuheshimu kwa kweli sio mtu sahihi kwako, inawezekana hana mapenzi kabisa na wewe ila hajui akuambieje kwa sababu watu wengi wanamfahamu na amekubalika kwenu.kwa hio yuko nawe kwa sababu hizo na si kitu kingine.
7.Mwanaume ambaye anakusema vibaya na hata kukutukana.

Anakuwa kama mtu aliechanganyikiwa , na utaoona unaumia kwa ajili yake , nae hana hata habari na wewe, mara nyingine anakupiga bila sababu ili apate nafasi ya kuwa mbali na wewe.kwa sababu huelewi unamwacha anaenda zake na baadae anarudi akiwa vizuri. Elewa kuwa anatumia hizo mbinu  za kukuchanganya ili umpe nafasi ya kuwa na wasichana wengine.

8.Yule ambaye hakuruhusu utoke na rafiki zake au familia yake.

wpid-man-and-woman-talking1 KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.

Endapo utaona mchumba wako anakasirika wewe ukiwa na rafiki zake au ndugu zake, uelewe mapema kuwa kuna kitu anaficha, hataki ukifahamu. Ndio maana hajisikii vizuri wewe utoke nao. Itakuwa labda kuna mtu hapo anatoka nae ambaye yuko karibu sana na familia yake na hata marafiki zake.

9.Mwanaume ambae muda mwingi anakudanganya.

stay-interviews-two-people-talking KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.

Mwanaume ambae hataki wewe uongee chochote mbele za watu, na anataka kuelezea mambo yote hata yanayokuhusu wewe, eti tu kwa sababu yeye ni mwanaume, atakuwa anataka kuizima sauti yako ili akutumie vizuri katika miradi yake na mambo yake ili usipate muda wa kutoka , na yeye awe anatoka muda wote. Amka ndugu yangu hapo utakuwa umefichiwa kitu ili awe na mambo yake .

10.Mwanaume ambae amekusaliti kabla ya ndoa , lazima ataendelea na hio tabia hata kama utajitahidi vipi.

images-12 KUNA NAMNA YA KUMJUA MWANAUME KUWA SIO MWAMINIFU.
Unapoona huruma na kufikiri kuwa huenda atabadilika mkiwa ndani ya ndoa. Pole dada, mapenzi yako hayawezi kumbadilisha, huyo ni msaliti tu, ataendelea kukusaliti hata ukifanya nini.

Kwa mimi ninavyoona , ni bora mwanaume akupende yeye kuliko kumlazimisha akuoe kwa kutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya hitaji la kuolewa. Ni mbaya sana kama mwanamke akimpenda mwanaume asiyefahamu kupendwa. Maana kipo kitu ambacho mimi na wewe hatukijui , wanaume hukitafuta . Labda watuambie. Fanya uchunguzi utaona.

Lakini mwanaume akimpenda mwanamke, na huyo mwanamke akawa na ufahamu mzuri wa kujua kuwa hapa napendwa watadumu na kuheshimiana na kupendana kwa dhati.
Hayo ni maoni yangu.

Usiache kuwashirikisha familia na marafiki makala hii ni nzuri. Kisha toa maoni yako kwa msaada zaidi.

Previous Dalili 10 Za Kujua Umekutana Na Kile Ulichokuwa Unatafuta..
Next JIEPUSHE NA MAMBO YAFUATAYO 10, BAADA YA KUACHWA:

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.