Kuona Vitu Ambavyo Havionekani


mail_image_preview-558x320 Kuona Vitu Ambavyo Havionekani

Ukiona mtu amekuzidi kwa kitu chochote, tambua kuwa kuna kitiu amekiona ambacho wewe hukioni.

Atakuwa anaishi kwa mafunuo sio kwa mawazo ya kawaida.  Mafunuo ni Mungu anakupa lakini mawazo yanatoka kwa watu.

Ukiwa na mafunuo  ya kazi yako, yatakuwa ni ya kudumu kwa sababu yanatoka kwa Mungu, lakini  wazo la mwanadamu huwa halidumu.

Ziko siri ambazo zimejificha , na kama ukitaka kujua siri hizi , ni kutafuta mahusiano na Mungu, kutumia Muda vizuri , kumwamini Mungu na kumpenda Mungu.

Kutumia muda vizuri ni kufikiri kwa muda wa kutosha. Fikiri mpaka akili itoke jasho. Muombe Mungu akupe mafunuo  ili uweze kuona vitu ambavyo havionekani.

Kuna watu wamefungwa macho na masikio yao, Wapo gizani japo wanajiona wapo kwenye Mwanga. Akili zao zimefungwa na giza kubwa la kukosa maarifa ya neno la Mungu.  Ukiona huwezi kutambua vitu vizuri, unatambua vitu vibaya , umefungwa kama sio kujifunga mwenyewe.

Walakini iko Hekima tusemayo kati ya mwanadamu, ila si hekima ya Dunia hii. Wala ya wale wanaoitawala Dunia, wanaobatilika, bali Hekima ya Mungu  katika siri. Ile Hekima iliyofichwa ambayo Mungu aliiazimu tangu Milele. Kwa  utukufu wetu. Ambayo wenye kuitawala Duinia hii Hawaijui hata mmoja.

Kama ilivyoandikwa  Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio kusikia , mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Mungu anawafunulia wale tu wampendao, kama humpendi Mungu utapata mawazo ya kawaida lakini hutaweza kupata mafunuo ya Mungu.

Mungu hawezi kukushushia kiti , meza, kitanda, mbao za kujengea.

Mungu anakupa MTI ili upate mafunuo ya kutengeneza kiti, meza na kitanda na vingine.

Mungu hawezi kukushushia gari bali atakupa  HEKIMA ya kutengeneza gari, pikipiki,  meli, treni , ndege na vingine.

Ukiona mtu analalamika, analalamikia serikali, wazazi, ndugu, marafiki na kujilalamikia mwenyewe, Muda wake umekufa, hafikiri na yupo gizani. ana macho lakini haoni furusa, ana masikio lakini hasikii  . Hana mafunuo . Hayupo na Mungu.

Siku ukiona fursa umeona maisha.Watu wanaweza wakakudharau lakini kumbe ulichonacho ndani yako ni kikubwa. umebeba mafunuo makubwa.

Kwa hio usilegee, bali ijapokuwa utu wako wa nje umechakaa, lakini utu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. maana dhiki yetu  nyepesi, iliyo ya muda kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio.

Tusiangalie vinavyoonekana bali visivyooonekana, kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu, bali visivyoonekana ni vya kudumu.

Usikubali mtu akudharau, wewe una akili , wewe ni wa kipekee, wewe ni shujaa, Jitambue upesi.

Mungu atakutengeneza na kukuthibitisha na kukutia nguvu.

Tafuta kupata mafunuo ya Mungu.

Subscribe.

 

Previous Imani Inayofanya Kazi Ndani Ya Maisha Ya Mtu
Next Sheria Ya Upendo

1 Comment

  1. Avatar
    Faik Said
    July 29, 2018
    Reply

    Safi sana nimependa hii mada ni nzuri sana. +255778 353535

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.