KUONYESHA NAKUPENDA. HAKUNA KUIBA


Steal-from-butt KUONYESHA  NAKUPENDA. HAKUNA KUIBA

Kuchukua muda wa mtu mwingine , utulivu wa mtu mwingine , kitu cha mtu, au nafasi ya mtu  bila ruhusu ni wizi.

Wabudha wanasema  usichukue chochote  usichokuwa huru nacho. Au hujapewa ni sawa na amri  mojawapo iliopo kwenye kitabu cha kutoka inayosema , Usiibe.  Njia moja ya kufikiria hio amri ni kwamba kuchukua kitu  ambacho kinastahili kwa mtu mwingine ni wizi  , labda iwe ni ruhusa kutoka kwa mwenye nacho.

Kuonyesha upendo ina maana  kuepukana na kumuumiza mwingine kama vyote vinawezekana.  Njia moja ambayo inaweza kumuumiza mtu mwingine ni kuingilia mipaka yao.  Hicho ni kitu ambacho kilitakiwa kifanyike  kwenye kiwanja  chao,  kilindwe na uhuru wao.

Kitu ambacho kinaweza kuibiwa.

Muda.  Moja ya rasilimali kubwa maishani ni muda.  Kuna mtu mmoja alikuwa akimwomba mungu kwa ajili ya  kutunza muda, alisema Mungu niwezeshe nisipoteze muda  na wala nisije nikawapotezea watu muda wao.  Hakupenda kuona watu wanaoiba muda hasa makazini.

Kipaumbele. Kuteka kipaumbele cha mtu ni kuiba.kama mtu anafanya kitu chake na ndicho ambacho anapenda kukitanguliza , halafu wewe ukaingilia na kumfanya asahau alichokuwa anakitanguliza na kufanya ya kwako , huo ni wizi.

Mali.  Mara nyingi kitu kinapoibiwa , kitu cha kwanza huo ni mali ya mtu. Unaweza kuwa umetumia kalamu yangu bila ya kuniuliza , umechukua gari yangu bila ruhusa yangu,  hivyo vitu ni vyangu. Hata kama mnaishi nyumba moja , kama kitu sio cha kwako na ukaamua kutumia bila idhini ya mtu huyo ni wizi .

Nafasi. Rasilimali nyingine muhimu ni  nafasi  ya kila mtu ndani ya mahusiano , ni sawa na mali na muda,  inaweza kuibiwa iwapo hakuna mipaka. Ni kama kulalia kitanda cha mtu mwingine..  Bila ya  kupewa ruhusa… au kula chakula  cha mtu bila ruhusa yake…ni uhalifu, ni kosa kubwa. Unaharibu nafasi.

Maamuzi. .Maamuzi ya kila mtu yaheshimiwe,  kwa maana kwamba kila mtu na asikilizwe katika maamuzi yake, asipuuzwe hata kama  maamuzi yake ni ya kijinga. Lakini ni bora kusikilizwa. Kuliko kuzarau kile mtu anachokisema, mwisho wake sio mzuri.

Wizi Unatokeaje.

Kushindwa kuuliza, njia rahisi ya kuepuka kuiba ni kuuliza,  ungependa…..?, Unataka …..? Ningependa…. Ni sawa kwako hio?  Unapata wazo

Ukiukwaji. Wakati mtu unaempenda anapoomba au  kukuambia usifanye au  kufanya kitu fulani , kukataa hilo ombi  ni wizi pia.  Unamfanyia mtu kama vile hayupo au  labda mbaya  zaidi atajisikia kama anataka zaidi  kuliko wewe.

Kuingilia.  Kama wazazi ambao huwalazimisha watoto kufanya vitu ambavyo hawavitaki kuvifanya , kama kusoma masomo ambayo hawataki na pia hawawezi. Au kuingilia  mambo yao ya siri,  , kutowaamini kwa kile wanachofanya ,  kuingilia mawazo yao, vipaumbele vyao,  au maamuzi yao , huo ni wizi.

Kuonyesha kuridhika wakati hudhiriki;  Wakati  mwingine unaweza kujiibia hata haki yako mwenyewe, kwa sababu ya kiburi au kutokujua kuwa una haki ya kupata kitu utakacho kutoka kwa mtu unaempenda. Unaibia nafsi yako mwenyewe unapokataa hisia zako kwa mwenza wako.  huo ni uwanja wako  kwa nini hauko huru.,

Kwa nini sasa, moja anaweza kuiba kutoka kwa anaempenda.

Aina hii ya wizi  ni rahisi kuwa mzuri  au kufanya kitu sahihi  kwa kusema hivi kuwa hakuna chumba cha mitazamo hio  kwa sababu  sheria hio ni sahihi,

Unaweza kuwa unajua hitaji la mtu na kitu gani anataka  vizuri zaidi kuliko wewe, inategemea na  nani anahitajika kutambua kwanza  hitaji la mtu  ili kuepuka wizi wa  kumdhania mtu.

Kutaka unachokitaka na kuchukua, . kilicho chako ni chako, na cha mwingine ni cha mwingine  sio chako.Au mwingine ni hivi, kilicho chake ni chake na cha mwingine chake.

Kutokukubaliana na mipaka  iliowekwa,  mipaka inaweza kuwa imewekwa , na kutokubali maamuzi ya mtu  na kudai kusahau ni kosa. heshimu mipaka ya ko na mipaka ya mwingine.

Umewahi kuibiwa mapenzi?  Ulijisikiaje?  Ulifanyaje? Athari zako ni zipi kwenye mahusiano? Umewahi kumwibia mpenzi wako? Unaweza kukarabati huo uvunjaji?

toa maoni yako katika makala hii.

Previous KANUNI AMBAYO ITAKUWEKA KARIBU NA MUNGU
Next NGUVU YA MABADILIKO INAYODHIHIRISHA UPENDO WA KWELI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.