Kuponya Na Kutibu


healingblogpostpic2-960x250-1 Kuponya Na Kutibu

Mtu pekee wa kukuponya ni wewe mwenyewe. Usitegemee Dactari, huyo Dactari atakusaidia tu lakini wewe utajiponya.

Wengi wetu tunapoumwa huwa tunakimbilia kwa madactari kupima  na kuandikiwa dawa. wakati mwingine sio ugonjwa wa kutumia dawa, ukitumia dalili zinarudi palepale.

Tafuta kiini cha tatizo, huenda kuna mahali umekosea , inawezekana tatizo lipo katika akili yako, Roho yako,  mawazo yako, ikasababisha maumivu ya mwili. huenda kuna kitu ulikula au ulikifanya bila kuwa na imani na hicho kitu au chakula, kikakuletea tatizo.

Watu wengi hufikiri magonjwa ya kurithi hayatibiki. sio kweli. hio ni akili  yako inakudanganya. Unao uwezo mkubwa wa kupigana na hio hali kwa kutafuta maarifa ya kutosha kuhusu hilo tatizo.

young-woman-cancer Kuponya Na Kutibu

Unaweza kubadilisha mfumo wa maisha , ukaanza kutumia muda vizuri, unakuwa mwaminifu kazini kwenye ndoa ,  biashara. unakuwa makini ni vitu gani vinaingia akilini mwako. unalisha nini roho yako, unalisha nini mwili wako. Unasikiliza vitu gani, una mitazamo gani.

Ukijitahidi katika kutafuta kiini cha tatizo ni rahisi kupona badala ya kutumia dawa ambazo zina madhara makubwa.

Nguvu ya uongo ipo ndani ya mtu . Badili mtazamo wako, badili tabia yako, Acha kulalamika, kulaumu watu, kujilaumu mwenyewe, kusononeka, kujihukumu. shughulikia akili yako, roho yako na mawazo yako pamoja na mwili wako.

download Kuponya Na Kutibu

Kuwa mtu wa shukrani. Mkumbuke Mungu, Msifu Mungu, Mshukuru Mungu . Anza kampeni ya kumtafuta Mungu kwa bidii kama una tatizo la kiafya.

Utaanza kuona unapona  magonjwa, umaskini katika kila hali .kutumia dawa bila kutubu  ni sawa na kwenda kwa mganga wa kienyeji. TUBU kwanza.

Bila kusamehewa dhambi hutaweza kupona ugonjwa ulionao. Anza na Mungu maliza na Mungu. Kumbuka kuwa Dactari anatibu lakini Mungu Anaponya. Neno la Mungu linaponya.

Elimu inatibu  Hofu , lakini Imani inaponya Hofu.

forgivness-1024x684 Kuponya Na Kutibu

Umasikini ni ugonjwa. Mathayo 11:5. Matajiri wengi wapo kwenye kundi la umaskini.

Kuwa makini unatumiaje muda wako. Unapigana na Ujinga au Umaskini?

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Jinsi Ya Kufuta Hofu, Maumivu na Kuzitawala Hisia
Next Kanuni Za Imani Katika Matendo

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.