KWA NINI DIET SIO NJIA YA KUPUNGUZA UZITO KWA WENGI


4 KWA NINI DIET SIO NJIA  YA KUPUNGUZA UZITO KWA WENGI

Kama kuna kitu kimoja ninachotaka mwaka huu kwa ajili yako ,ni   kile kitu chenye majaribio makubwa  ya kuendelea  na diet nyingine  ambayo inakufanya  ujilaumu, uone aibu , na kukata tamaa.

Tumaini langu  kwako ni kwamba  uchague kitu kinachofaa, cha kukufurahisha na kukufanya ujione mkamilifu,  na kweli hicho kitu kipo.

Hii sio makala ya kukufanya utupilie diet zingine kule, ni mwaliko   wa kukufanya uache  kulazimisha  na kujisukuma au kujifungia  kwa sababu tofauti, tuwe serious, diet inaboa sana katika maisha ya kila mtu.

Tunachopata kwenye diet ni vitu visivyotosheleza kwetu., diet nyingi zinasema kuwa utakuwa mwenye afya lakini  inakufanya uzidishe unene zaidi ya ule mwili ulionao kwa sasa au uwe dhaifu. Ni kuhusu kupunguza uzito  kitu ambacho kitafanya kila  kitu kiwe kizuri na utakuwa mwenye furaha na afya. Badala ya kujihangaisha akili yako  na diet inayokuharibu.

Ukweli ni kwamba huhitaji kubadilisha kitu ili kutaka uwe tofauti, diet sio ya kweli . unatakiwa kuacha vyakula unavyovipenda na kula vyakula usivyovipenda, halafu unarudi kujilaumu mwenyewe , hio sio diet unapoanza kuingiza huko.

Diet  inakufanya wewe  uone kama unaenda kutengeneza kitu, mpendwa , hutengenezi kitu , maana wewe hujavunjika.

Najua zipo diet ambazo unaziona watu wakitumia , hizo sio diet bali ni mtindo tu  wa maisha. Nakutia moyo  kwenye changamoto hii, bila shaka kama utapata njia nzuri ya kula chakula chako , jipe nguvu dada, kaka. Napenda kusema kwamba sio watu wote wanapenda kupunguza uzito.

Kuna watu wengi wamekuwa hawaelewi wamezidiwa , na kuchanganyikiwa  na uzito walio nao, dieting,  na mahusiano ambayo sio mazuri na chakula na miili yao.

Ukianza kuchunguza jinsi roho yako inavyofanya kazi ya kuelewa kila hatua, linapokuja suala la kupunguza uzito, afya na furaha,  ni rahisi kuliko hata unavyofikiria

Uhuru wa chakula

Tunakuwa tunapoteza malengo yetu.tunaacha kujaribu kujitawala, kujisimamia, kuhesabu, kuogopa kuona aibu, na stress kuhusu  kitu gani tutakula . tunaharibu hali ya ndani  na sio nzuri kiafya, tunaacha kula tunapokuwa tunahitaji kula, halafu tunakula wakati ambao hatuhitaji kula.

Kila unapokuta chakula unajinyima kwa kuwa unahitaji chakula cha kupangiwa , na sio chakula ambacho roho yako inapenda, huoni kama kuna tofauti hapo? Diet yako inakuja kutokana na kupenda au kutopenda?

Kwa kula chakula unachokipenda , utafurahia na kuwa huru , hutakuwa na stress.

Kukubalika kwa mwili

Hivi unajua kwamba huu ndio mwili ulionao? Huo mwili wako  ni mmoja tu  unakalia nao ,Unajua hio shape ya mwili wako hapo kuwa ni shape nzuri ulionayo hata mwisho? Kwa kuwa hatujui  roho inahitaji nini ndani yetu.

Tunahitaji kuchagua kwa ndani kabisa , kuupenda mwili bila sababu,  kwa mapenzi yote.

Kama unahitaji kuwa mwenye afya, nafikiri hapa ndio  naamini pakuanzia.

Lishe nzuri inayoaminika ni muhimu?  Ndio , kwa hio hatutakiwi kuanza kujificha , tuanzie kwenye mizizi.  Changamoto ya chakula  iwe ni njia  ya uponyaji, kwa hio fanya hivyo. Ni matumaini yangu  kwa mwaka huu  hutajihangaisha , utakuwa ni mtu mwenye positive, Unastahili  kila kilicho bora .

Ishi maisha unayoyapenda , mwili unaoutaka, afya ni muhimu kuliko diet. Fanya mazoezi ili uwe mwenye furaha na maisha yako.

Umeipenda hii makala ? shirikisha na wengine

Previous SABABU AMBAYO HUJAWAHI KUSIKIA KWA NINI NI MUHIMU WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI
Next MAHUSIANO YENYE MAFANIKIO HUHITAJI MUDA NA NGUVU

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.