KWA NINI KILA MWANAUME NI MUHIMU KUFANYA MEDITATION


Yoga- KWA NINI KILA MWANAUME NI MUHIMU KUFANYA MEDITATION

Ni lazima Vinginevyo…

Hata kama wewe ni mwanaume mwenye kazi nyingi au mwenye tamaa ya mambo mengi, unaeshindwa kujidhibiti kwa kuwa na mpenzi mmoja. Au mwanamke una mume mwenye macho yasiotulia. Amini katika hili.
Kila mwanadamu ni muhimu kwake kufanya tafakari , nimejuaje?. hii kitu imemtokea mtu ambaye alikuwa na tabia kama hizo na amekaa sawa.

Wanaume wengi wanaamini kuwa furaha na mafanikio ya maisha yanatokana na kufanya kazi kwa bidii bila ya kupumzika, matendo ya kimwili na kukamilisha mambo ya kidunia.

Lakini kama watagundua meditation, mtazamo wao utabadilika .Weka uwezekano wa kutafakari , utaanza kugundua faida nyingi zilizopo ndani yako , kwenye nafya ya mwili, ya akili, na kiroho na maisha ya kila siku.

Meditation itakusaidia kufanya mambo kwa urahisi na kwa usahihi bila ya pressure.
Utagundua kiasi cha nguvu ulizonazo ndani yako, utulivu uliopo na hisia ulizonazo.. hutakuwa na stress.

SABABU 5 AMBAZO KILA MWANAUME NI LAZIMA KUFANYA MEDITATION

1.Inaondoa Stress na Wasiwasi

30ish-black-guy-worried-feb-12 KWA NINI KILA MWANAUME NI MUHIMU KUFANYA MEDITATION

Kama una stress ya mahusiano, ya kazi au chochote kile , tafakari itaondoa , utakuwa mtu usiekuwa na woga, utafanikiwa kimwili, kiakili na kiuchumi na utakuwa salama. utakuwa mtu mwenye ujasiri kwa kila kitu.

2.Inaboresha Utendaji wako

Inakuweka bayana na ina sharpen akili yako na utaweza kufanya maamuzi sahihi na kwa urahisi na kwa wakati maalumu ili kupata suluhu ya tatizo lililopo.
Inakuongezea nguvu ya afya yako katika utendaji.

3.Itakusaidia uweze kuishi wakati uliopo

Mbali na kuhangaika na yaliopita au kuogopa wakati ujao, itakupa utulivu na kuwa mwenye furaha hata kama unapita kwenye magumu kiasi gani.

4.Meditation Inaongeza Intuition yako

Inakusaidia kupata mguso wa kweli katika maisha yanayotokana na silika yako. utaweza kuyafahamu mawazo yako ndani kuwa ni mazuri au ni mabaya. na kila kilicho karibu yako utakitambua .Itazalisha mawazo mapya , itakufungua kupokea ulinzi wa Mungu na Usikivu kutoka kwa Mungu.

5.Inaboresha Utendaji wako katika Ngono

Panapokuwepo stress kuhusu ngono na utendaji huwa unapungua. Tafakari inafanya kazi ya kurudisha nguvu yako ya utulivu wa mawazo yako, nguvu za kiume zitaongezeka. .
Inakusaidia kujenga mahusiano mazuri na mwenza wako.

Yep; Tafakari ni kitu kizuri na bora kwa ajili yako. Ondoka huko na Anza leo kufanya meditation na utaona matokeo yake.

Unataka kuanza na hujui ni jinsi gani utafanya . Usisite kuniuliza. kwa meseji nitakusaidia kupata urahisi wa kutafakari.

Previous SABABU ZA KAWAIDA KABISA AMBAZO ZINAHARIBU MAHUSIANO
Next TUNAPOFIKIRI UPENDO ULIVYO NA UKWELI HALISI WA UPENDO WENYEWE

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.