Kwa Nini Ni Ngumu Kupata Upendo Ndani Yako (kujipenda)


Capture-19 Kwa Nini Ni Ngumu Kupata Upendo Ndani Yako (kujipenda)

Wazazi wetu walisema hivyo, marafiki zetu walisema hivyo pia, hata mimi na wewe tunasema hivyo.

Jinsi gani Mtu atajipenda mwenyewe.

Tunaona ni neno la shukurani na la utoshelevu lakini kusema kweli  ni gumu  kulitoa.

Tumekuwa tukikutana na makala nyingi za  kuhusu kujijali, jinsi gani ya  kulinda upendo wa kipeke yako baada ya kuumizwa moyo na mtu uliyekuwa unampenda, au kupoteza kitu ulichokipenda. Kwenye vitu ambavyo ulitaka kutunza na  ambavyo vimekufanya ukwame  sehemu kubwa.

Wanasema kwamba kama ukijipenda utaweza kuwa mkamilifu. Na  wakati ninapokubaliana nao , lakini sio rahisi. Kamwe sio kitu rahisi.

Unaona, huwezi tu kuamka asubuhi  na kujiona mkamilifu tena.  Huwezi tu kuamka asubuhi na kujihisi unaishi kama vile kuna kitu kinawaka ndani yako  na kujiona kama unajipenda.

Sisemi kwamba usikilize sauti  za mapepo tu. Ila ninachosema kwamba kujipenda ni ngumu lakini ni kitu kizuri.

Kujipenda haiji kama mwizi usiku ili kuiba wasiwasi wako  au kuondoa hali yako ya hofu.

Inaanza na kujitambua. Unapokuwa unajitambua na kuwa makini kwenye vitu  ambavyo unahitaji kuvibadilisha,  mawazo mabaya unayohitaji kuyadharau  na hali  ya mazingira ambayo unataka kukabiliana nayo,  Unahitaji kuepuka,  Hapo utaweza  kuona hali halisi  , njia yako itakuwa wazi  na mtazamo wako utakuwa mzuri.

images-2 Kwa Nini Ni Ngumu Kupata Upendo Ndani Yako (kujipenda)

Halafu utaanza kujikubali.  Wakati ambao tayari una uelewa wa kutosha  kwamba kuna mambo ambayo hutaweza kuyatawala. Si kila kitu utaweza kukifanya. Ndipo utakuwa na maamuzi kwamba kila mara huwezi kutarajia  kitu vile vile kama ulivyotaka kufanyiwa na watu wengine ,  hapo utakubali kuwa maisha yana nyakati,  Mambo mabaya hutokea, Ni wewe uamuzi wako kukubali au  kujiweka mwenyewe katika  uchungu na kujilaumu.

Kujikubali  haiji kwa kupanga kitu cha kufanya, Inakuja na hali inayotokana na nyakati  za maamuzi yako  kama mtu uliyekomaa kufanya mambo makubwa na madogo.

Inatokana na kujisamehe. Unaona, Hiki ni kipengele cha kujipenda, kumsamehe mtu aliyekufanyia kitu kibaya , kujisamehe mwenyewe kwa maamuzi uliyoyafanya mabaya au mazuri ni kitu kingine.  Ni vita ya ndani mwako . Kati ya Moyo wako na Roho yako.

Imekuwa kawaida watu kujilaumu wenyewe na kubeba mizigo mizito bila ya kuwa na ufahamu  wa mahali pa kutua hio mizigo.  Tunajiona hatufai.  Tunadharau mawazo yetu , maamuzi yetu kwa kuogopa  kujihukumu  kutokana na kanuni zetu wenyewe.  Tunaishi  kwa kuongozwa na jamii.

Tunafikiri ni ubinafsi kujipenda, Lakini Hapana. Kwa sababu  ni mbaya sana kuishi kwa kufuata  maagizo ya jamii tu kuliko kuishi kile unachokiamini wewe kama wewe.

Ndio maana inakuwa ngumu. Ndio maana watu wanachanganyikiwa. Lakini kuna uzuri uliopo ndani yake. kwa sababu inapokuja  nyakati za  kujipenda  na kitu unachohitaji,  kiakili na kihisia , hapo ndipo utaanza  kujipenda. utaona urahisi  wa kujisamehe kwa kutokuwa mkamilifu,  na wakati unapojiona umekamilika hio ndio hali halisi ya kujipenda.

 

Previous Ukitaka Kuendelea Kulenga Kitu Ukitakacho
Next Kabla Hujampata Mtu Wa Kudumu Kwenye Mahusiano ,Jitafute Kwanza Wewe. Ujitambue.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.