Kwa Nini Wana Wa Nuru Hawafanikiwi,Lakini Wana Wa Giza Wanafanikiwa


Watafiti waligundua kuwa ndani ya Biblia Kuna mistari 2350 inayoongelea pesa na mali.

getty_468868827_970566970450047_60099 Kwa Nini Wana Wa Nuru Hawafanikiwi,Lakini Wana Wa Giza Wanafanikiwa

Yesu alifundisha Pesa zaidi kuliko kitu kingine chochote. Kuna aina 38 ya mifano ya

Yesu . Mifano 16 ilizungumzia pesa.

Kwa kuwa  hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Wana wa Nuru wengi wanafikiri pesa ni dhambi. pesa sio dhambi, dhambi inakuja kutokana na matumizi yako ya pesa, unaitumia wapi, wakati gani.

Mungu hampi mtu pesa asiyekuwa na maarifa na ufahamu. Asiyekuwa na Hekima. Mungu anakupa pesa kulingana na akili , na uwezo ulionao wa kufikiri. Utalalamika sana, utaomba sana, utafunga sana, lakini kumbuka kuwa ,

Kuna madeni makubwa ambayo wana wa Nuru hawayafahamu , Nayo ni madeni ya kiroho. vifurushi vikubwa.

1.Deni la Muda

Mungu anakupa masaa 24 kila siku lakini  haupo tayari kujifunza maarifa ya nenbo la Mungu. hauko tayari kwenda kuwatazama Yatima, Wajane, Wafungwa, Husomi neno la Mungu, Huandiki neno la Mungu. Muda wako mwingi unapotelea kwa adui. upo tayari kukaa bar masaa matatu na zaidi , kijiweni, kwenye smartphone  kuchart na kusambaza dhambi zilizojificha, halafu unajiita mwana wa Mungu. Hutaweza kufanikiwa. Wakati huo huo wana wa giza wako bize kupigana na  maisha  wewe umelala.

2.Deni la mazingira

Mungu alimtwaa Adamu  akamweka katika Bustani ya Eden Ailime na kuitunza . Adamu wa leo ni wewe na Mimi je,  unafahamu kuwa umefungwa ufahamu wako kwa kutokufanya usafi wa mazingira  na Akili yako imelala haiwezi kufikiri mambo makubwa  bali inafikiria vitu vya kawaida kila siku ? Kugusa ardhi ni kufungulia baraka , ulinzi wa kazi zako, kuanza kuona fursa mbalimba. Ni kuanza kuwa na furaha, Amani ndani yako, inakusaidia wewe na mimi tutumie muda vizuri. Badala ya kuongea umbea , kuangalia movies siku nzima, kuchart na kusoma magazeti , tumia muda wako kufanya usafi wa mazingira, nyumbani mwako, kazini kwako,  barabarani, kuzibua mitaro na vingine vingi, utaanza kuona Mungu anakushirikisha baraka zake.

3.Deni la UPENDO

Kumpenda mke, mume, kuwapenda watoto, kuwapenda majirani, kujitoa kwa ajili ya wengine. kumpenda Mungu, Kujipenda wewe mwenyewe.

4.Deni la Kutoa

Kutoa ni lazima kwa sababu   tunatakiwa kuonyesha upendo kwa Mungu. Mungu alitupenda na akawa mfano kwetu katika kutoa.  Tusipotoa tunaharibu Agizo la Mungu , Tunaruka maandiko ya Mungu. Mungu hawezi kukushirikisha Baraka zake  Kama humtolei kwa moyo wa kupenda. Mungu hawezi kuweka ulinzi kwenye mali zako, hawezi kuweka ulinzi wa kazi zako na familia yako pamoja na vitu mbalimbali katika maisha yako.

Lakini wana wa giza wanatoa sana kwa Mungu wao , Ndio maana wanafanikiwa. Hata kama kitu  ambacho kinamuumiza moyo anakitoa  .Mfano kuua  mzazi, watoto, mke na ndugu.

Kaa fikiria kama Mungu angesema kila mtu awe ananunua pumzi, ingekuwaje? maana kila siku inawezekana tungekuwa tunaenda kujipanga makanisani au misikitini ili kununua Pumzi. Sidhani kama watu wangeweza kupona , maana watu wengi  hawana uwezo wa kununua .

Huwezi kumpenda Mungu kama hutoi muda wako kumtumikia , hutoi pesa  kusaidia wengine, unajiangalia wewe.

Badilika , anza kutumia muda wako vizuri, anza kumpenda Mungu, Fanya usafi wa Mazingira. Wapende watu na kuipenda nafsi yako. ukiwapenda watu hutawafanyia vibaya, hutawaua kwa kuwauzia vitu hatari ambavyo wewe mwewnyewe huwezi kuvitumia. hutaweza kuwawazia mabaya.

Linda moyo wako kuliko kitu chochote unachokilinda.

Subscribe . utaweza kupata makala mpya mara nyingi.

Previous Soma Hii Kama Akili Yako Inaumia Na Unahisi Kuboreka
Next Kitu Gani Unachokipenda Umekificha Kuhusu Mwenza Wako?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.