Kwa Nini Watu Wabaya Wanasonga Mbele


 

Wachunguzi wamegundua kitu kinachowafanya watu  wabaya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko watu wale ambao ni watiifu.

Unapokuwa kwenye mahusiano mabaya  na mtu, kitu unachohitaji ni kukimbia, ingawa ubaya huo unaweza kuwepo upande wako. Kama bosi wako ni mtu mbaya, itakuwa ngumu kwako kupona  bila ya kujitoa muhanga  kufanya kazi kwa bidii na kwa umakini ili uweze kuendelea kubaki kazini. Itakugharimu kufanya kazi nyingi bila ya  malipo ya ziada.Sio kwamba kazi nyingi kiasi hicho ili kukufanya  uone hali ya hewa mbaya ulingane na wengine wote.

Huwa tunafikiri kwamba watu wabaya wana tabia ya kuwaza mabaya kila wakati na hupenda kurudisha watu nyuma.  kwenye mahusiano ya karibu  huwa wanakufanya ujione hauko sahihi kila wakati.  Hata kazini pia hivyo hivyo  utakuwa unawaza kukosa kazi kama ukilalamikia bosi. Wana nguvu kubwa,  wanajua wanaweza kukufanya uone kuwa maisha ni mabaya. marafiki na familia watakuona mtu mwenye stress na huzuni nyingi. Utakuwa unateseka kiakili na kimwili pia.

Unaweza kuwa unashangaa kwa nini watu hawa wabaya wanafanikiwa? Inaonyesha kuwa ufunguo wa  mafanikio ya watu hawa upo kwenye tabia zao za UONGO ndani ya mpangilio wao wa akili zenye ujuzi mkubwa wa kudanganya watu wengine wajione hawafai.

Mimi nimewaona hata wewe unawaona kila siku. ni watu ambao wanacheza na wenye vyeo vikubwa. huenda kuchongea wengine waonekane wabaya ili wao wapande vyeo. mara zote wako macho kuhakikisha  wanafanikiwa bila kushindwa.

Wakiwa katilka nafasi za juu maamuzi yao huwa ya kibinafsi, ni wadanganyifu,  na waongo.  Unaweza ukawa unafikiri kuwa ipo siku watashindwa, lakini watu hawa mara nyingi wanazidi kupandishwa cheo na kuongezewa mshahara.

Sababu kubwa inayowafanya watu hawa wafanikiwe ni kutokana na mabosi wao kupitia njia kama za kwao. Walifanikiwa kwa uongo na utapeli mkubwa hadi kufikia mahali walipo.  Wanawapenda watu ambao wana tabia kama zao.

Ukweli nikwamba Nuru Na Giza  Haviwezi kukaa pamoja. Kwa kuwa Nuru ikiwepo giza hutoweka, na mahali penye Giza hakuna Nuru. Kama wewe unafanya kazi na watu wa aina hii ni ngumu kufanikiwa. Labda kama shirika linahitaji watu waaminifu utaweza kupona.  Kumbuka wakati mwingine shirika huhitaji watu  wabaya kwa kutaka kujulikana pasipo halali au kukata kazi zifanyike kwa njia watakazo wao.

Utafanyaje kama utajua uko mahali  penye sumu kama hio? Watu wenye utu wa giza. Ni bora kufanya utaratibu wa kutafuta mahali kwingine, vinginevyo utafanyiwa vibaya , utafanya kazi zako kwa shida. Kama unaweza kucheza mchezo wenye nguvu. cheza na Mungu mwenye nguvu, Simama katika kweli, fanya kazi zako vizuri kila siku. jijengee utu wako vizuri , uwe jasiri, uwe na imani, tafuta maarifa ya kutosha , onyesha upendo.  Usiende kushoto wala kulia, baki na Mungu Hapo utashinda.

Jitosheleze kazini , vilevile  hata katika mahusiano, usiige ubaya, funika ubaya kwa wema. Hukuumbwa na hofu wala woga, kufanikiwa kwako ni lazima, usiteseke na mtu . Uwezo ulionao ni mkubwa huhitaji kuteseka.

Subscribe.

Previous Nunua Kweli Usiuze,Baki Nayo Ikulinde
Next Mbinu 5 Zinazo ondoa Aibu na Wasiwasi Wa Muda Mrefu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.