MAAGANO AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUWABARIKI WATU WAKE


Agano ni kubaliano Fulani ambalohuambatana na vitendo katika makubaliano hayo ili kutimia kwa kusudi/ahadi inayotegemewa kupitia utekelezaji huo.

Watu wa Mungu wengi tumekuwa na tabia ya kumpenda Mungu kupitia kutii amri zake bila kukumbuka utelezaji wa agano ambalo huleta mafanikio katika biashara na kazi maishani mwetu. Ufalme wa giza wengi wao huwa na umakini wa hali ya juu sana katika kutekeleza maagano wanayopewa kulingana na taratibu walizojiwekea, watoto wa Mungu tukiwa na Muongozo wa Bibilia ambao umegawanyika katika sehemu mbili agano la kale na agano jipya, lakini utekelezaji wetu umekuwa hafifu sana na wakutoridhisha kabisa na hivyo kuwafanya wakristo wengi kuwa ni watu wakuhangaika na kufanya mara nyingine wayumbishe kwa kuwa wakristo wa muonekano tu huku wengi wao wakiwa wanatekeleza maagano ya ufalme wa giza kutimiza uhitaji katika biashara na kazi.

Tujifunze pamoja maagano ya ufalme wa Mungu na katika utekelezaji wake tutaona mafanikio na utajiri udumuo mithali 8:18

  1. AGANO LA KUFUNGA NA KUOMBA

Kuomba ni maongezi kati ya mtu na Mungu, maongozi haya unapaswa pia kujifunza namna ya uwasilishaji wake. Ili usije ufanya maongozi haya katika mpangilio wenye matokeo katika yale uyaombayo. Jifunze kupitia vitabu mbalimbali vya watumishi wa Mungu kadhalika ni vyema ukatumia zaburi kwenye kuomba kwako kwani zaburi ni mjumuisho wa sala na tenzi mbalimbali kulingana na hitaji lako. Mfano zaburi ya 2 –sala ya asubuhi,zaburi ya 4- sala ya jioni ,zaburi ya 31-sala katika shida kubwa,zaburi ya 41-sala ya mgonjwa, zaburi ya 51-sala ya toba na kumuomba Mungu rehem, zaburi ya 91- sala ya kumuomba ulinzi.

zaburi 55:17

Daudi aliweka agano na Mungu la kumuomba mara tatu kwa siku, mimi na wewe ni jukumu letu kuweka ratiba katika muda wetu kwa kudhamiria kuwa tutamuomba MUngu mara ngapi kwa siku.

1wathesalonike 5:17

Tumepewa maelekezo ya kuomba bila kukoma hivyo kwa kumaanisha kuwa Mungu wetu hatatuchoka pale tunapoenda kuongea naye, yeye yu tayari kutusikiliza sikio lake sio nzito kutusikia na mkono wake sio mfupi kwamba atashindwa kutuokoa, hivyo mar zote Mungu hufikiri namna ya kuokoa nafsi zetu zisipotee katika uasi wa aina yeyote.

Isaya 59:1,2

 

Kufunga ni kanuni ya ulimengu wa roho wa kuhusisha nguvu za kiroho ili kufanya jambo lililokusudiwa.

Isaya 58:6-8

  1. AGANO LA SIFA

Sifa ni chakula cha Mungu, na ndio kusudi la Mungu kutuumba na watu wengi hukutana na ishara na miujiza wakati wa sifa. Sifa zinakupeleka viwango vingine katika ufalme wa Mungu , kutoka kuitwa mwana wa Mungu kwenda kuitwa rafiki mfano daudi ( Mungu anamuita daudi rafiki – hiki ni kiwango kikubwa sana)

Zaburi 119:164

Daudi alimsifu Mungu mara saba kwa siku kama mfalme, mimi na wewe inabidi tujifunze uishi maisha ya sifa kila wakati kila mara

Zaburi 150;6

Kila mwana wa Mungu anayetumia pumzi ya Mungu ni amri kumsifu Mungu haijalishi unapitia changamoto gani.

Unapomsifu Mungu wakati wa changamoto Mungu husababisha mpenyo wa kiungu kulifanya swala lako kuwa shuhuda katika maisha yako

Mfano Paulo na sila Matendo

Sifa ni agano la muhimu sana maishani mwetu, ndio maana familia ya huduma ya   kingdom business tumeamua kumsifu Mungu kila baada ya dakika 60, dakika 1 tu, tunamsifu Mungu katika muda kamili na tunaona Mungu akifanya matendo makuu ndani ya maisha yetu na katika maeneo ya biashara shuhuda kuongezeka zaidi na zaidi.

 

  1. AGANO LA KUKUMBUKA

1samweli 17:34

Kila mmoja wetu katika maisha yake kuna jambo Mungu amemtendea maishani mwake, hivyo utimilivu wa changamoto iliyo mbele yake unapaswa uwe ni  mtu wa kukumbuka ukuu na matendo makuu Mungu aliyokufanyia kama daudi alivyomshinda goliati kupitia kukumbuka Mungu  aliyemuokoa katika samba na dubu. Kadhalika katika biashara hujauza leo lakini unapaswa kukumbuka muujiza Mungu aliokutendea siku za nyuma na kuanza kudhamini uwepo wa Mungu huyohuyo kuwa ataonekana katika changamoto yako inayokukabili mbele. Wana wa Mungu wengi siku hizi tumekuwa ni watu wa kulalamika na kusahau anayotufanyia Mungu katika biashara zetu na hivyo kufanya wengi kurudi nyuma katika kumtegemea yeye na kujilimbikizia majukumu yasiyotuhusu ikiwa maisha yote tunayoishi hapa suniani ni biashara ya Mungu.

 

  1. AGANO LA KUSHUKURU

1WATHESALONIKE 5:18

Kila jambo ni jukumu letu liabatane na neno la asante kwa Mungu kupitia katika jina Yesu kristo, shukrani ni mapenzi ya Mungu sio ya mtu yeyote hivyo ni jukumu letu sote kujijengea tabia ya shukrani kwa Mungu na sio watu kwani ukimshukuru mtu maana yake amechukua nafasi ya Mungu, hivyo tuwe makini sana mtu awe ni baba yako, mama yako  au yeyote Yule amekupa  kitu muambie Mungu akubariki na akuzidishie maisha marefu uongezewe maradufu na afya ya kiungu itawale maishani mwako; kisha ukiingia kwenye maombi unamuambia Mungu asante na kumshukuru kwa matendo makuu aliyokufanyia kupitia mtu huyo uliyembariki.

 

Wakati mwingine utamsikia Mtu hutamka neno” ASANTE YESU” kila wakati ikiwa ni agano ambalo ameliweka kati yake na Mungu kumshukuru kila wakati kwa kila jambo na Mungu humtumia na kumuongoza katika njia zake zote.

cropped-1024x482 MAAGANO AMBAYO MUNGU HUTUMIA KUWABARIKI WATU WAKE

 

  1. AGANO LA KUMFIKIRIA MUNGU.

Kiwango unavyomfikiria Mungu sana kinaamua kufanikisha safari yako vizuri na kustawi katika kila jambo la maisha na biashara, kwani unavyomfikiria mwenye biashara na kutafakari kwa kina muongozo wa neno lake unapata njia sahihi na kutambua ni kitu gani cha kufanya kwa wakati gani na mahali gani na kuchukua hatua hatua.

Joshua 1:8

Wakolosai 3:16

Neno la Mungu inabiadi liwe kwa wingi sana katika akili yako nah ii huja kwa kulitafakari na kulisoma kwa bidii kuliko ilivyo kawaida huku ukiwa na Muongozo war oho mtakatifu kwa ajili ya kukufundisha na kukufunulia nini cha kufanya katika maisha.

 

  1. AGANO LA NGUVU

Tunaamini kuwa jambo lolote linaitaji nguvu ili kulipata na kumiliki

Mathayo 11:12

Ufalme wa Mungu unatekwa na wenye nguvu pekee,hivyo ukiamua kufanya jambo Fulani kwa ajili ya Mungu jitoe na kujikana kwelikweli usifanye kawaida nawe utaona matokeo yasiyo ya kawaida yakikurudia maishani mwako na katika kila Nyanja za maisha yako

Mwanzo 32:22-32

Inakubidi ushinde kama yakobo mpaka jina lake likabadilishwa kuwa Israel, ukijitoa kwa nguvu zako zote katika ufalme wa Mungu ushindi utadhihirika na maisha yako yatakuwa mfano wa kuigwa.

 

  1. AGANO LA MUDA

Kila siku kila mtu amepewa mbegu ya 24 kutoka kwa Mungu sawa na sekunde 86400 inategemea wewe utagawa kwa watu au utawekeza vizuri kwa ajili ya mavuno ya kesho, hivyo ni vyema ukatambua hazina ya muda Mungu aliyowekeza ndani mwako kuwa ni mbegu amekupa usipopanda katika udongo mzuri itakufa na kukuletea majuto na maisha ya huzuni katika uzee wako. Hivyo tambua vyema umuhimu wa mbegu hizo kupanda katika shamba la bwana kwa kumtumikia Mungu na Mungu atakushangaza katika maisha yako.

 

  1. AGANO LA UTOAJI

Yohana 3:16

Utoaji wa kudhamiria huleta matokeo mazuri sana katika ufalme wa Mungu, jifunze utoa muda na mali zako kwa ajili ya ufalme wa Mungu kusaidia wahitaji kupitia

yakobo 1:27 Mungu hatakutupa kwani utoaji ni moja ya agano ambalo Mungu hubariki nalo watu.

Malaki 3:10

Utoaji wa fungu la kumi ina nguvu kubwa sana ya kulinda mali zako na maongezeko mara dufu katika matarajio yako.

 

  1. AGANO LA KUMTUMIKIA MUNGU

Kutoka 23:25,26

Agano hili hufanya uthihirisho wa afya ya kiungu na kubarikiwa katika chakula na maji na kufufua kila kilchokuwa tasa iwe ni kwenye biashara taaluma na familia aMungu huondoa utasa huo na kufanya uzao wenye Baraka na kutimiza idadi za siku hapa duniani kupitia neno la Isaya 65:20

Mathayo 6:33

Kumtumikia Mungu kwanza kwa kutafuta ufalme wake huleta matokeo yasiyo na kelele kwani yale mambo wengine wanayopambana kuyapata wewe unazidishiwa.

                                                           

  1. AGANO LA KUMHOFU MUNGU NA KUISHI MAISHA YA KUTENDA HAKI.

Hofu ni kutii maelekezo ya Mungu kwa ajili yako kama mtumishi wa Mungu hata kama hayakuandikwa katika neno lake.

Isaya 20:1-4

Tunaona isaya alimhofu Mungu na kutii sauti ya Mungu kwa kuitekeleza kwa kumtumikia Mungu akiwa uchi kwa muda wa miaka mitatu bila kujali chochote au watu waliomzunguka watasemaje na hakuna mahali imeandikwa bali ni maelekezo Mungu alimpatia isaya moja kwa moja kama mtumishi wake. Hivyo ni jukumu la kila mtu kutambua kuwa muda wote Mungu anaweza kukupa agizo na kupaswa kulitekeleza yote ni kwa ajili ya sifa na utukufu wake.

Kutenda haki ni agano lenye mipenyo katika biashara na maisha kwa kiwngo cha juu sana

Mithali 4:18

Hali kadhalika kulipa kodi ya serekali ni jukumu letu sote kama wafanyabiashara kwani maendeleo ya nchi yeyote huletwa na wananchi wenyewe kupitia malipo ya kodi.

Na kukwepa kodi ya serekali ni jambo lisilompendeza Mungu na huleta madhara makubwakatika jamii husika

Mfano: madawa hospitali na vifaa vyote hununuliwa kupitia kodi ya wananchi na malipo ya watumishi wote wa serekali

Previous UKITAKA MPENYO FIKIRI KAMA MTUMISHI
Next FANYA KAZI KWA MUDA NA KWA AKILI

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.