Maana Ya Maisha Huenda Ni Maisha Yenyewe


Tunapata maana ya maisha kila tunapoamka , na kupata uzoefu wa mambo yote

Ni nini maana ya maisha ? Unaweza kuona kama swali la kijinga lakini  ni gumu sana kulijibu,

the-tree-of-life-terrence-malick-jessica-chastain-movie-brad-pitt-1200x520-1024x444 Maana Ya Maisha Huenda Ni Maisha Yenyewe

naweza kufikiri tofauti kidogo kutokana na wasomi na wengine wanavyofikiria siku hizi , tunaweza kubishana kuwa maisha hayana maana  halisi , tupo tu  kwa ajili ya kuzaa ili tuongezeke.  Lakini hii sio maana halisi ya maisha.

Tunaweza kusema kuwa  na dini fulani ili ufike mbinguni, maisha ni kujulikana,  ni kujaribu kuifanya Dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi,  lakini  yote tunayofanya tunafuata mambo yale yale yaliopita zamani , mipango iliyopita, hata ufahamu wetu tulionao tunafikiri tuna uzoefu wa kitu fulani  ndani ya vichwa vyetu ambavyo havijawahi kutokea, au vinatokea tu kama kivuli kwenye kazi za ubongo wetu. Ni kweli ndani yetu tuna vitu vikubwa lakini hatuelewi.

Mimi nafikiri ipo maana ya maisha  lakini bado hatujaelewa, tunajiona kama tumetengenezwa na mashine  au tunaishi kwa kutegemea mashine iliopo ndani yetu. Sidhani kabisa kama maisha hayana maana  kati ya kuzaliwa na kufa  kuna kitu mtu anatakiwa kukifanya ili aweze kufurahia maisha yake ya huo muda. Na hii sio kwa sababu mimi ni mtu wa dini sana hapana .

Kwa hio kwa nini nafikiri maisha yana maana ? huenda nimekuwa disappointingly, Ni ngumu kuweka katika maneno, lakini ngoja nijaribu japo kidogo.

Mateso ya mwanadamu Huletwa na Mabadiliko Ya Uzoefu

Katika miaka 10 ya uzoefu wangu  nimeona watu ambao hupitia mateso  hukutana na matatizo makubwa hasa maradhi  ya saratani na kisukari na hata ugonjwa mbaya wa moyo na kusababisha vifo vya haraka.

Kitu gani hasa kinawapata hawa watu , ni kwa sababu kila wanapoamka hawachukui maisha mazuri yanayoachiliwa na Mungu kwa sababu ya kuzoea mateso, hawana ufahamu wa kutosha kuhusu maisha, wanamiliki miili badala ya Roho, wameshindwa kujiunganisha na watu wazuri, ni watu wanaoweka mioyo yao kwenye vitu sio kwa Mungu.  Wanasahau vitu vya muhimu  kama Upendo , Amani, Furaha, Fadhili Uaminifu na mengine. Wanakimbizana na vitu. Kutafuta Pesa Ili kujilinganisha na wengine.

Kwa mtindo huu huwezi kuishi bali utateseka kila siku. hutajua maana ya maisha ni nini kwako.

Baadhi Ya mifano 

Kuna mama mmoja ambaye alikuwa amepimwa na kuonekana na saratani  alisema hivi,  Nashukuru Mungu kuwepo kwenye sayari hii.. Nahisi ni bahati ya ajabu  kwepo na kuweza kupata ufahamu huu . Mtu mmoja aliniambia kuwa nikitumia pombe  nitajisikia vizuri na kuwa mwenye nguvu, pia nitajiona kuwa salama, nitajitambua  na kugundua siri za ajabu  katika Dunia hii.

Akasema kama akiambiwa kuchagua maisha au kifo , Ataweka Ahadi kwamba , kama akipona  ataishi maisha ya kweli , yaliojaa utajiri wa Mungu, Sitachukua kitu chochote nilichonacho, Nitaifurahia Kila siku kwa kuwa Ninaishi.

Mtu mwingine anasema kwamba anasikitika kwa kuwa amepoteza muda mwingi kutokubaliana na vitu vidogo , yeye alikuwa anataka kupata vitu vikubwa kwa mara moja ili kukamilisha malengo yake kwa upesi zaidi, akawa anahitaji pesa nyingi  na kwa kuwa hakuwa na ufahamu , hakuwa na maarifa wala Ndani yake hapakuwepo hekima ya Mungu . alikuwa gizani kwa kiasi kikubwa , Sasa anateseka . hakujua kabisa maana ya maisha . Ingawa baadae aliona maana ya maisha  ni kujifunza sio kutafuta pesa, kukua na kupata uzoefu kwanza.

Hawa watu wote hawakuwahi kusikia kuokoka , hawakuwa watu wa kujifunza , walikuwa wanawaza pesa ili kununua vitu nao waonekane . Ipo njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za Mauti.

Haya mabadiliko hayawezi kuja kwa haraka yanachukuwa muda mrefu. mpaka  mtu afundishwe afahamu ndio atagundua maisha ni nini. Nafikiri mabadiliko yanaweza kuelezewa kwa namna nyingi ili kuleta maana halisi ya maisha.

Mabadiliko ya Kwenye Mazingira.

Spiritualawakening-1024x576 Maana Ya Maisha Huenda Ni Maisha Yenyewe

Usipende kuteseka kwenye mambo mabaya , Jifunze  mambo mbali mbali kwenye maisha ili uishi kama wengine wanavyoishi. Soma vitabu , Nenda kwenye semina , nenda kanisani, nenda msikitini, sikiliza video nzuri zinazohusu kitu unachokitaka maishani mwako.  Fanya mazoezi, Tumia Muda wako vizuri, ukiwa bize kujifunza kuhusu jinsi gani utatumia muda wako , utaanza kuishi kwa njia rahisi sana.

Tumia muda wako kufikiri , kutafuta mawazo mapya na kutafuta taarifa sahihi kila mahali unapokuwa.  Uwe mtu wa kusamehe , kushukuru,  mwema, mwenye upendo, jikubali, jiheshimu, jitambue. Kujitambua ndio mtaji wako mkubwa.

Kwa maana nyingine tunapata maana ya maisha kila tunapoamka na kuwa na kitu  cha kufanya kwa uzoefu . Lakini ukiwa gizani bado utaona maisha hayana maana , Tafuta Nuru ya Neno la Mungu  upate ufahamu mkubwa , ufunguliwe ndani yako na urudi nyumbani maana umepotea. Rudi kwenye maana . Hiyo Maana ni Mungu .

Ili kuweka katika sentensi moja  hii maana ya maisha ni kwamba. Maisha sio biashara yako Ni Biashara ya Mungu. Rudi nyumbani.

Subscribe uendelee kujifunza.

 

Previous Pambana Na Nguvu Inayozuia Unabii Wako Kukamilika
Next Njia 10 Za Kukufanya Uwe Mtu Bora

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.