MAANDALIZI (PREPARATION)


Preparayion-is-the-key MAANDALIZI (PREPARATION)

 

Maandalizi ni ujuzi wa Imani na kuweka Imani kwenye matendo unapoifuata picha ya mwisho unayoielekea. Waebrania 11:1 “basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarayajiwayo ni bayana ya Mambo yasiyoonekana”.

Kila mmoja unayemwona amefanikiwa leo katika jambo lolote lile alijiandaa wakati wa nyuma kufikia hapo alipo. Hakuna matokeo ya bahati kwenye maisha na endapo kila jambo hutokea kwa mshangao  kwenye maisha yako moja kwa moja humaanisha hauna maandalizi uliyofanya.

Watu wengi huchukua muda kujiandaa kwa kila kitu kama vile kwenda mjini, kuhudhuria harusi au tamasha flani kadhalika na safari kwa mahitaji kulingana na mualiko husika.

Katika maandalizi ya maisha kuna madhabahu muhimu sana tunapaswa kujifunza na kuchukua hatua ya vitendo kuzifanyia kazi kwa neema ya Yesu Kristo.

Madhabahu ya kufikiri (The altar of prayer)

Yoshua 1:8 “kitabu hiki cha torati cha torati kisiondoke kinywani mwako bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliandikwa humo maana ndipo utakapofanikisha njia yako kisha ndipo utakapofanikiwa sana”

Hii ni ya kwanza na muhimu kila mmoja kujihusisha katika kufikiri kabla ya kufanya jambo lolote luka 14:28-30 “maana ni nani katika ninyi kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia? Asije akashundwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki wakisema mtu huyu alianza kujenga akawa hana nguvu za kumaliza.”  Yeyote yule anahitaji kujenga nyumba huhitaji ramani, kuanza biashara huhitaji maandalizi ya mchakato wa biashara( business plan & master plan), mjamzito hujiandaa kwa nguo za mtoto mtarajiwa malezi na mengineyo   kadhalika kuoa huhitaji mwanaume au mwanamke vyote hivi huhusisha akili kufikiri kuyakabili mambo haya.

Katika ulimwengu wa kiroho madhabahu ya kufikiri ni kujifunza neno la Mungu mpaka upate ufunuo (picha halisi) wa majukumu ya kufanya kuleta udhihirisho katika maisha. Mfano unahitaji kuingia katika maombi ya kukabithi biashara au huduma unayofanya, inakupasa kujikita katika madhabahu ya kufikiri kutafuta maandiko ya neno la Mungu katika eneo hilo la biashara au huduma uanze kuyasoma na kutafakari kwa kina ili unapoelekea katika madhabahu inayofuata uone matumizi yake.

Madhabahu ya maombi.( The altar of prayer)

Maombi hutegemea sana  madhabahu ya kufikiri, na hapa ni kuleta hoja kwa Mungu kupitia neno lake

Isaya 41::21 “haya leteni maneno yenu asema BWANA, toeni hoja zenu zenye nguvu asema mfalme wa Yakobo” lazima ujifunze kuomba kupitia neno la Mungu na jina la Yesu.  Yohana 14:13,14 “nanyi mkiomba lolote kwa jina langu hilo nitalifanya ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya”. Maombi ni matamshi yatokayo katika kinywa chako ,kadhalika unapaswa kuwa makini na jambo lolote litokalo kwenye kinywa chako kwani ni mbegu na huleta madhihirisho katika maisha yako baadae, jifunze kuzungumza hoja kupitia neno la Mungu likijaa kwa

Previous Kukumbatiana Inaweza Ikawa Ni Njia Nzuri Ya Kumaliza Tatizo
Next FIKIRI MABADILIKO  (THINK FOR CHANGE)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.