MABADILIKO YA MITINDO YA MILO AMBAYO ITAONGEZA AFYA YA AKILI YAKO


Corbis-42-26531074 MABADILIKO YA MITINDO YA MILO AMBAYO ITAONGEZA  AFYA YA AKILI YAKO

Wachunguzi wamegundua kuwa kati ya watu wanne mmoja ana tatizo la akili katika moja ya  vitu vya  maisha yake. Ingawa bado tunajitahidi kujiboresha wenyewe kimwili.

Tunalenga zaidi katika kuangalia mambo ya vyakula gani vya kula  au kufikiria zaidi  njia za kufanya  ili kupungua uzito  au ili kupata nguvu za kiume au kuwa na hamu ya tendo la ndoa. Lakini tunasahau  kuhusu  akili zetu na hisia za kibinadamu.

Hii ni mbaya  kweli  na inasemekana kuwa afya ya akili ndio chanzo cha kila kitu katika sifa  ya kuwa na maisha  ya utulivu. Kwa sababu inathiri vitendo vyetu  na jinsi tunavyofikiria, na hata maamuzi tunayofanya. Kuhusu mahusiano na jinsi ya kukabiliana nayo.

Kwa hio kama una mipango ya kuhakikisha kuboresha maisha yako sasa, usisahau kuweka kipaumbele afya ya akili. Na hapa kuna mitindo ambayo itabadilisha  na kuongeza afya ya akili  iwe vizuri,

1.Kuongea Ukweli Na Dactari wako

Ni kama unavyohitaji kuongea na dactari kabla ya kuanza mazoezi, pia unahitaji kuongea na mtaalamu   kuhusu jinsi gani utaboresha afya ya akili.. Atakupima  kama kuna woga na kama kuna wasiwasi au msongo wowote na kukuelekeza kwa mtu ambaye anaweza kukusaidia  hilo.

2.Boresha Mlo wako

Tunachokula pia kinaathiri mfumo wa akili zetu. Ni vizuri na ni muhimu kufahamu kitu tunachokula  kiwe kinaboresha akili . Wachunguzi wameonyesha kuwa matunda  na mboga  ni vyakula ambavyo vinaongeza afya ya akili. Wakati  mlo wa mafuta mengi unaleta madhara kwenye akili. Tazama mlo wenye mboga nyingi na matunda.

3.Weka Kipaumbele Mazoezi.

Zoezi la ubongo na neva vinaongeza afya,  inafanya mtu ajisikie vizuri wakati wa mazoezi  na homoni zake zinakaa vizuri. Weka kipaumbele kwenye mazoezi  utavuna  faida  za kimwili na kiakili. Huna haja ya kukimbia kwa saa nzima, au  workout kwa  saa nzima. Unaweza hata kuchukua jukumu la kulima bustani inatosha.

4.Jifunze njia za kuondoa Stress.

Stress zinaathiri   afya ya akili,  kwa hio ukiwa na njia ya kupunguza au kuondoa  utafanya makubwa kwenye maisha. Meditation au yoga ndio  nzuri  kwa kupunguza  stress na kutunza afya ya akili . Fanya meditation kwa dakika 10 to 30 kwa siku  inatosha kwa ajili ya kutunza afya yako ya akili. Na itakuwa na nguvu.

5.Pata Usingizi Mzuri.

Kukosa usingizi , akili na mwili wako  havitaweza kufanya kazi vizuri . wachunguzi wanasema ni ngumu kufanya maamuzi yalio sahihi  na hutaweza kutawala hisia zako  kama utakuwa hupati usingizi wa  kutosha.

Kwenda kulala kwa wakati na bila ya kupata usumbufu usiokuwa na maana inasaidia kusukuma afya ya akili na mwili.

Ni vizuri pia kama utaepuka kutumia  caffeine, pombe, chakula kizito muda mfupi kabla ya kwenda kulala.

6.Nenda Kwenye Tiba

Watu wengi huwa hatuoni umuhimu wa kwenda kumuona tabibu wa afya ya  akili kwa sababu ya kutofahamu umuhimu wake. Tunafikiria kwenda huko ni wakati ukiwa na tatizo la akili tu.

Wataalamu wa  afya ya akili wanaweza kukuongoza  kujua jinsi ya kukabiliana na mawazo mabaya. Kukufundisha jinsi ya kuepuka,  na kufahamu ni tiba ipi itakusaidia.

7.Anza Kuandika Mambo

Kuandika mambo yako , kama mawazo ulio nayo  na hisia ulizonazo ni afya na ni njia  ya kupunguza  stress na kuwa na amani ya akili. Anza kuandika  na kuweka wasiwasi na  mawazo yako kwenye karatasi . unaweza kusahau ulichokiandika au kurudi tena kuangalia . lakini wachunguzi waliona ni vizuri ukiandika na kutupa mbali  karatasi au kulichoma itasaidia kupunguza stress.

8.Tafuta Ufahamu Mwenyewe.

Elimu  ni msingi,Hasa inapokuja kwenye afya ya akili.Unaweza kuwa na hisia nzuri  kwa yule unaempenda  kutokana na uelewa ulionao  na kufahamu kitu gani kinaendelea kati yenu. Umuhimu zaidi , kujifunza mbinu mpya , kusoma vitabu, au  kwenda kwenye jumba la  makumbusho itakusaidia  kuifanya akili   iwe sharp.

9.Jiondoe mwenyewe.

Kuna mitandao mingine inaleta  huzuni, au inaweza kukuathiri afya ya akili yako , na unaweza kupata wasiwasi mwingi kutokana na mambo unayoona. Jiondoe kwenye mitandao hio.  Tafuta kitu ambacho kitakupa afya ya akili  fanya.

10.Onyesha Wema.

Kuna kitu kinachosema kuwa inalipa , unapofanya  vizuri kwa watu .onyesha wema na mfanye mtu awe na furaha . kumfanya mtu ajisikie vizuri  pia utapata  faida. Huko ndiko kupanda na kuvuna.

11.Usisahau Waliokusaidia

Tunahitaji marafiki na familia. Kuungana na watu inasaidia kujenga afya ya akili. Kuwa na muda kidogo wa kufurahia na marafiki au familia ni bora kuliko kuwa mwenyewe. Inapunguza stress.

Tusisahau afya  za akili zetu na hisia zetu. Ni muhimu kama afya ya mwili. Tunapojitahidi kubadilisha mitindo kwa ajili ya kuuweka mwili vizuri, pia ni muhimu tusisahau kuweka mitindo ya  kuboresha afya ya akili  zetu..Humo ndio kuna kila kitu .

Previous DALILI 10 ZINAONYESHA KUWA UHUSIANO WENU NI MZURI
Next SWALI MOJA LINAWEZA KUOKOA NDOA YAKO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.