Mahusiano Yaliopo Kati Ya Imani Na Maombi


TheRelationshipBetweenFaithandPrayer Mahusiano Yaliopo Kati Ya Imani Na Maombi

Imani ya  kila dini ina nyenzo nyingi za kumsaidia muumini  anaeamini kwenda hatua nyingine. Mfumo huu ni wa maombi. Maombi ni njia yako  ya mawasiliano na Mungu.Unaweza kuomba chochote Unachokitaka Kwa imani yako.Ukienda kwa Mungu Bila mashaka.

Mungu anajua kila kitu kuhusu wewe na mimi. Woga wetu, Familia zetu,  Lakini kuna kitu cha kushirikishana naye kimawazo, na kile kinachohusiana, Na hamu ya Mungu ni kuwa na urafiki wa karibu na wewe. Anahitaji utambue kuwa anakujali. anakutaka wewe ukikaribie  kiti cha  neema  kwa ujasiri ili akupe rehema   na neema ya kukusaidia wakati  unapohitaji. Onyesha kuwa unamuhitaji  na kwamba hakuna mwingine  anaweza kujibu maswali yako ila ni yeye tu kwa sababu ya imani yako kwake.

Ingawa Maombi ni zaidi ya kuongea  na Mungu , Lakini pia Usikivu wako kwa Mungu. Ndio.Bado anatumia mbinu nyingi za kuongea na  wewe. kama aliweza kuongea na watakatifu wa zamani kwa nini asiweze kuongea na wewe kama unaamini anaweza. Ni kweli anaweza  kuongea na wewe.  Ana majibu ya maswali yako yote, matatizo yote,  hamu yako, wasiwasi wako, na matumaini yako.

Kama hujawahi kumsikia  kwa sauti, jaribu kusoma maneno yake kwa sauti. hapo utajua kuwa Mungu anaongea na wewe. Ni baba yako , anatamani akupe vitu vizuri.anasema ikiwa wewe waweza kumpatia  mtoto wako kipawa chema, je si zaidi sana yeye  ataweza kukupatia mema  wewe unayemwomba? Hatazami mtu, sehemu, au kitu chochote kujibu maombi yako. Mchumba wako, rafiki au wazazi  wanaweza kuwa na vyanzo vya kukusaidia, lakini Mungu ndio Chanzo chako. Chanzo chake ni cha kudumu.

Kila mara Mungu anataka kuona moyo wako, mahali ambapo kuna hazina yako, mahali ambapo kuna Imani yako. Anataka kujua Unamwamini vipi.  Imani yako itafungua milango  kwa ajili ya maombi yako  na kujibiwa. Na atakuongeza  sehemu ambazo umekuwa pungufu.

luke-18-1-400x400 Mahusiano Yaliopo Kati Ya Imani Na Maombi

Maombi ni Silaha yenye nguvu sana kwako, kwa kadri unavyoamini , Utapata.  Silaha hio itakusaidia kushinda mawazo mabaya. Hata hivyo utamjuaje mtu kama huna muda na yeye?  Huwezi kusema kuwa Mungu ni rafiki yako hata huna muda na yeye, humfahamu vizuri. Hufahamu chochote kuhusu yeye. Hutaweza kuweka Imani yeyote kwa mtu ambaye humfahamu vizuri na hujui uwezo wake. Kwa kujua hili , Unatakiwa kuwa na muda wa kutaka kumjua . Ukweli wa Mungu.

Kama hupati muda wa maombi hutaweza kumjua. Unaweza kufahamu jina lake na historia kuhusu yeye, lakini  huna ufahamu wa kirafiki na yeye. Katika maombi utajenga Imani yako kwa Mungu.  Kwa kadri unavyokaa kwenye maombi, Ndivyo Mungu anavyojitokeza kwako kwa sababu  wewe ni rafiki yake. yeye anajua, yupo popote, ni mwenye nguvu. Ni upendeleo wa kiasi gani kuchukua kila kitu kwa rafiki kama huyu.

 

Previous Ipo Siku Utapata Mapenzi Unayostahili
Next Mambo Mawili Nimekuwa Nikiyafikiria (Na Sitaacha kuongea Kuhusu Hili)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.