MAJUKWAA YA TAARIFA SAHIHI (PLATFORM OF INFORMATION)


 

Lazima uwe na jukwaa la taarifa zinazokuwezesha kuvuka sehemu moja ya maisha kwenda katika kiwango cha mafanikio, kwani chochote kile kwenye maisha kinakua kwa taarifa unazozipata taarifa hukuza akili yako na akili yako inakuza utedaji wako wa kazi na mafanikio hutokea.

Kuna aina ya vyanzo vya taarifa tutayaangalia ukizimgatia kupata taarifa sahihi kwenye majukwaa haya utaona maisha yako yatabadilika.

1.Marafiki (Friends)

Mithali 27:17 “chuma hunoa chuma kama mtu aunoavyo uso wa rafiki yake”

Lazima uchaguae kuambatana na marafiki sahihi wakukujenga wewe kiroho, kimwili na kiakili kwani usipokua katika maeneo yote matatu hutafanya vizuri kwenye maisha. Ambatana na marafiki wanatunza muda wenye kukupa taarifa za kukuondoa sehemu ulipo kuelekea kwenye kisima cha mafanikio kama ilivyo kusudi la Mungu sisi kufanikiwa kupitia 3Yohana2 “mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yako  yote na kuwa na afya njema kama vile roho yako ifanikiwavyo.”

  1. Roho mtakatifu (Holy Spirit)

Yohana 14:26 “lakini huyo msaidizi huyo Roho Mtakatifu ambaye Baba atampeleka kwa jina langu atawafundisha yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Katika maisha ya mwanadamu kuna mtu wa ndani ambaye ni roho mtakatifu hukuwezesha na kukufundisha kukupa dira ya chochote kile unachokihitaji kwenye maisha, kukufundisha, kukusaidia,kukuonyesha mambo yajayo na kukuepusha katika njia zisizosahihi. Yohana 16:13 “lakini yeye atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie kwenye kweli yote kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari yake.”

  1. Wachungaji (Pastors)

Yeremia 3:15     “nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendazao moyo wangu wataowalisha kwa maarifa na fahamu.”

Kanisani ni jukwaa la taarifa za kujenga ufahamu wako ili kukupatia hekima ya Mungu kupitia Neno la Mungu hivyo jitahidi sana uwe na kanisa wanalofundisha neno la Mungu na uwe unaandika neno la Mungu kwa ajili ya kujifunza wakati mwingine kwenye familia yako na maisha yako kwa ujumla kwani vitu vyote vitapita lakini neno la Mungu halitapita kamwe ni kwa manufaa ya kizazi chako chote kusoma ulivyokuwa unaenda kuandika kanisani na kupata ufunuo utakaoleta mabadiliko kwenye maisha yao.

4.Maonyesho ya kibiashara (Trade Fare)

Jukwaa hili ni muhimu sana kwani mwanadamu anakua kwa kutizama kisha kuuliza maswali, kila wakati katika eneo unapoishi au umepata taarifa kuhusu maonyesho ya kibishara unapaswa kuandaa vitu maalum kwa ajili ya kukusanya taarifa na kuuliza maswali yatayojenga biashara  kusonga mbele kutoka hapo ilipohakikisha maonyesho yoyote yale unaenda na note book, kalamu, rekoda ,kamera kukuwezesha kukusanya taarifa ipasavyo.

  1. Wazazi (Parents)

Wakolosai 3:20 “Ninyi watoto watiini wazazi wenu katika mambo yote maana jambo hili lapendeza katika Bwana.”

Kuna taarifa wazazi wanazo zakukufikisha katika lengo unalokusudia kwani wazazi wameona mengi zaidi yako kulingana na umri walionao , ni muhimu kuwatii wazazi na kuwauliza maswali pale ambapo unauhitaji acha kiburi na dharau kwa kujiona wakisasa. Mathalani maswala ya ndoa wana uwezo wakukupa taarifa itakayokusaidia katika maamuzi sahihi kama mtoto wao kwani alikopita wewe ndio unapita sasa hivi. Hivyo tujifunze namna ya kuteka Baraka kutoka kwa wazazi kwa kulipa gharama ya utii kwao na kupata maneno ya Baraka yatayotufanikisha katika kila jambo tunalolifanya.

  1. Maktaba (Library)

Danieli 9:2 “katika mwaka wa kumiliki kwake, mimi Danieli kwa kuvisoma vitabu nalifahamu hesabu ya miaka ambayo neno la BWANA lilimjia Yeremia nabii ya kutimiza ukiwa wa Yerusalemu yaani miaka sabini.”

Jifunze kuwa na library nyumbani kwako kwa ajili ya kujenga akili yako kuwa njema wakati wote. Mfano nabii Danieli alikuwa anasoma wakati wote mpaka akagundua kuwa mda wa kuishi utumwani umeshaisha, hivyo na wewe pia huenda biashara unayofanya imekosa taarifa sahihi, huduma unayotoa haina taarifa za kutosha kukuwezesha isonge mbele hivyo ni sawa na kusema ipo utumwani mpaka utakapoanza kutafuta taarifa sahihi kwenye biashara hiyo itasonga mbele.

  1. THE KINGDOM BUSINESS CLUBSHIP.

Waebrania 5:14  “lakini chakula kigumu ni cha watu wazima ambao akili zao kwa kutumiwa zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.”

Jukwaa hili utajifunza namna ya kufanya biashara, huduma, kazi ,ndoa, mahusiano kwa kumtegemea Mungu na kutumia akili yako. Mafunzo haya yatakujenga kuingia katika ulimwengu wa kufanya jambo lolote kwa kumpenda Mungu, kuwapenda watu na kupenda Nafsi yako kupitia Imani ya neno la Mungu kwani Imani huja kwa kusikia na kusikia neno la Kristo ambalo huleta Hekima ya Kristo kufanya vitu visivyoonekana kuonekana kwani kila kitu kilitumika kwa yeye Yesu Kristo katika uumbaji. Kingdom business clubship utapata maelekezo ya kwenda kuyafanyia kazi sio maelezo kisha Mungu atakushangaza wakati unafanya kwa vitendo kwani Imani ni matendo. Watu wengi wanapenda vitu vya maelezo sio maelekezo, hivyo jukwaa hili litainua kiwango cha Imani yako na akili yako katika ubora unaompendeza Mungu. Zaburi 1:3 “naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji uzaao matunda yake kwa majira yake wala jani lake halinyauki na kila alitendalo litafanikiwa.”

Subscribe. 

Previous FANYA KAZI KWA MUDA NA KWA AKILI
This is the most recent story.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.