Mambo 10 Watu Wenye Ujasiri Huyafanya Ili Kuwa Na Maisha Bora


ZARI Mambo 10 Watu Wenye Ujasiri Huyafanya Ili Kuwa Na Maisha Bora

1.Wanafahamu Umuhiumu wa mitazamo  mizuri.

Ukiwa mtu wa mitazamo mizuri  hasa kwa kila kinachoendelea katika maisha yako, Kila unachovutia ni kizuri . Haushughuliki na mambo mabaya .Mtazamo wako ndio uchaguzi wako  na umewafanya wengine wajisikie vizuri katika uwepo wako

Hakuna kati yetu aliye mkamilifu,  lakini kama utaanza kuvutia vitu vizuri ambavyo unavitaka, wewe ni mtu wa mabadiliko mazuri. unahitaji kuwa mtu fulani.

Sio tu mtazamo wako mzuri ulionao  bali hata mtazamo juu ya watu wanaokuzunguka  na jinsi unavyowafanya wajisikie vizuri. Lakini kama maneno yako  ni Negative na unawadharau watu, mtazamo wako hautakuwa mzuri , hata hivyo utakuwa unavutia  vitu vibaya. Kumbuka kuwa nguvu uliyonayo inavuta nguvu hio hio.

Jaribu kuangalia kila kitu kwa njia nzuri, Ingawa wakati mwingine sio rahisi . wakati mwingine mazingira  yake yanakuwa magumu , lakini tafuta kitu kidogo  ambacho utashikilia  na jaribu  kutunza mtazamo wako uwe mzuri.

Fikiria vitu unavyosema, Ni negative? kama ndio hivyo jaribu kutambua na ufanyie kazi ya kurekebisha.  Huwezi kusema mambo mabaya halafu uwe na mtazamo mzuri.  Ondoa maneno kama, siwezi, chuki,  labda, ipo siku.

Jifunze kusema asante. kujifunza kushukuru  na kuwakubali wengine  na kuwa mtu wa shukurani kwa watu wema maishani mwako utavutia zaidi.

2.Wana Vipaumbele Sahihi

Ukitambua thamani ya muda wako utajifunza kutoupoteza hata kidogo.

Masaa uliyonayo ni 24. kila mtu , kila mwanadamu anayo masaa hayo.  Yapo mbele yako, Ni juu yako kujua jinsi gani unautumia muda wako.

Nunua Muda halafu muuzie Mungu, ili Mungu akulipe yeye. Kumbuka muda ni mali yako umepewa na Mungu. Tumia kitu ambacho unacho tayari. Muda wako. Kama huna pesa bado muda unao. Utajiri upo ndani ya muda. Muda una nguvu kuliko Upendo. Muda una nguvu kuliko Imani. Tazama jinsi muda ulivyo na umuhimu katika maisha yako.

Upendo ukiondoka  unaweza kuendelea kuishi, lakini muda wako ukiondoka  na wewe unaondoka. Yaani unakufa. vivyo hivyo na imani.

Mungu amekupa vitu vitatu muhimu navyo ni  Hekima, Maarifa, na Furaha.  huu ni utajiri. Na Mungu anaweza kukupa muda wa ziada kama utakuwa unatii muda.

3.Wanajali  Afya Zao na Ustawi.

Afya sio kuonekana vizuri. ni kuhusu kujisikia vizuri na kujijali  nafsi yako, mwili wako  na kujipenda mwenyewe.

Sio tu kimwili bali na kihisia pia.

Kutambua jinsi ya kukabiliana na madhara ya misongo ya maisha, itakufanya kuwa na afya nzuri ya moyo wako, maisha ya furaha, na mahusiano yako kwa ujumla.

Stress nyingi zinasababishwa na fikra zetu wenyewe.  tunasababisha wenyewe. lakini kama utachukua hatua ya  kujali  afya ya akili yako, kama unavyojali mwili wako, hutakuwa na stress.

Mwili wako unaweza kukuongoza kwa kila kitu unachokimiliki ili kuweza kuwa na shape nzuri. Ukichoka mwili utakupa saini. unahitaji kupumuzika, kama ukifanya hivyo hutapata magonjwa. Kama utaupatia mwili chakula sahihi, vinywaji sahihi, utaishi kwa muda mrefu.

Afya sio tu kuwa na mwili mzuri, unakuwa mwenye ujasiri, inaongeza nidhamu, unakuwa na mahusiano mazuri yako mwenyewe, kitu ambacho ni cha muhimu sana maishani mwako. mahusiano yako binafsi.

4.Wanaweka Familia Zao mbele.

Haijalishi una mafanikio kiasi gani , lakini kama utajali sana mafanikio bila familia ni kazi bure. Weka mahusiano yako  mazuri ndani ya familia yako.

Wazazi wako wanahitaji  muda wako na usikivu wako tu.

5.Wanafahamu  majukumu na kutoa  kwa moyo.

Ipo gharama  katika mafanikio . ni kazi yako kutambua  kitu unachokitaka kiwe na malengo mazuri kama unavyotaka.

Lakini inahitaji uwe na kipaji, ni muhimu.  Watu hawa kama mambo yakienda vibaya huwa hawakati tamaa, maana wanaelewa kuwa watakinua tena. kwa sababu wanacho kitu ndani yao.

Kujitoa ni zaidi ya  uchaguzi unaofanya.

6.Kuelewa  Umuhimu wa mzunguko wao wa ndani

Watu wenye mawazo mabaya hujishusha chini wao wenyewe.

Huwezi kuwa mwenye mawazo mazuri kama watu uliowachagua  ni watu wenye mawazo mabaya.

Sikiliza mambo wanayoongea, jinsi gani wanajijali wao wenyewe, mambo wanayofanya,  umbea wao, mambo ya kijinga wanayoonyesha.  Watu wenye mafanikio hawapotezi muda wao kuongea kuhusu wengine. hawajali kusemwa, ukimsema unampa faida.

Badala yake huwainua wengine , na kuonyesha ubora wao, sio mabaya yao. utatambua kupitia haya.

1.Watu hawa wanaongezeka kiakili , kukua kiakili kila wakati

2.Hawasemi wengine vibaya

3.Wanakuinua na wakati huohuo wanajisikia vizuri kufanya hivyo.

 4.Wanakupenda na kukujali

5.Wanakuona wewe ni wa maana kwao.

7.WANAFAHAMU KUWA UKARIMU SIO PESA.

Kuwa mkarimu sio kiasi cha pesa ulizonazo. Ukarimu ni muda unaowekeza kwa watu kwa kuwajali, kuwapenda, kuwakubali, kujua thamani zao. Ni kufanya kitu ambacho pesa haiwezi kununua.

Watu hawajui kuwa kama huna pesa ya kumpatia mtu , mpe muda wako.  Usifikirie pesa , fikiria muda .

Wanaamini kwamba kitu chochote kizuri utakachofanya kwa mtu , ni lazima kitakurudia. Kile unachopenda kufanyiwa, mfanyie na mwingine.

8.Wanajua jinsi gani Wanaweza Kujisukuma wenyewe.

Wanaelewa jinsi ya kuwa bora wao wenyewe.

Ni kuhusu kupanga malengo, Na kufanyia kazi kwa bidii. Kuyaandika malengo yao kila siku ili kuyaona.  Yanakuwa nI malengo ya muda mrefu na mfupi na mipango ya kufanikisha.

Uwezo wao ni mkubwa, kujisukuma Kwao  katika kufanikisha, kuondoka katika hali nzuri. Hawaogopi changamoto za mabadiliko.

9.Hawalaumu mtu mwingine Kwa makosa yao.

Wanachukua majukumu  katika maisha yao, hata kama hajakosea kitu hatakulaumu wewe, atajilaumu yeye. hata mambo ambayo hawawezi kudhibiti.  Kama kitu hakiwezekani wanaachana nacho.

Mtu yeyote anayelaumu mtu mwingine  ambaye amekosea, utakuta analaumu wengine hata kwa kushindwa kwake. lakini wenye mafanikio huchukua yote, mabaya na mazuri ni yao.

10. Hawatulii, hawakati tamaa

Hawakati tamaa kwenye kazi zao, kwenye mahusiano yao,  Wanafahamu thamani zao na kustahili kwao. Na kama watagundua kuwa wapo sehemu ambayo sio  sahihi kwao , hawakai. Kama mtu haoni wanachokitoa, Wanaondoka, kwa sababu kazi yao sio kumlazimisha mtu ili  kuwapenda au kuwajali, Wao tayari wako full katika kila kitu.

Share kwa wengine.

kisha  Subscribe.

Previous Tatizo Kubwa Ni Kujiona Uko Sahihi Kila Mara
Next Tabia Inayoua Urafiki Ndani Ya Mahusiano

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.