Mambo Ya Kukumbuka Wakati Unapohisi Kuumizwa Na Upweke


5acf9ed1146e711e008b46d7-750-563 Mambo Ya Kukumbuka  Wakati Unapohisi Kuumizwa Na UpwekeWapo watu unaowafahamu , wa kawaida na hata wale wanaojulikana , watu maarufu, wakati mwingine wanajikuta kupitia hali hii ya upweke na kujiona kama wametengwa.

Ni vizuri kutambua kwamba hauko peke yako, Yupo Mungu pamoja na wewe. Swali la kujiuliza ni kwamba , Utafanyaje unapokutana na hali kama hio?

Vifuatavyo ni vitu vya kukumbuka

1.Tambua kwamba ni sawa kupitia hali hio !

Mungu humpa yeye aliyemridhia  hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji  humpa taabu.

Muhubiri 3:1-8, kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati wa kila kusudi chini ya mbingu.

Wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa. wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa yaliopandwa wakati wa kuua na wakati wa kupoza, wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga, wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza.wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe, Wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatiwa. wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,  wakati wa kurarua na wa kushona,  wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena,  Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wa amani.

2.Tumia Upweke Huo Kama   kujifunza  kujitafuta mwenyewe

Huu ndio wakati wa kumtafuta Mungu, kujitahidi kupata mahusiano yako wewe na Mungu, kujiongoza, kujiheshimu, kufanya kazi zote, kutafuta hekima, maarifa mbalimbali, kusoma vitabu, kwenda semina mbalimbali.

Maana hekima itaingia moyoni mwako na maarifa  yatakupendeza nafsi yako, ili kukuokoa na mambo ya uovu. linda moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana  ndiko zitokako chemchemi za uzima.

3.Tambua kwamba Huo Ni Wakati wa  kujua uhalisia wako.

kabiliana na ukweli, kama ulikuwa umeajiriwa na umefukuzwa kazi au kazi haikulipi, usikimbie tatizo kabiliana na changamoto mpaka utoke, Anza kutumia muda wako vizuri kwa kugusa maisha ya watu. tumia akili ipasavyo na umtegemee Mungu sio mwanadamu.

general-5228401-604 Mambo Ya Kukumbuka  Wakati Unapohisi Kuumizwa Na Upweke

4.Kuwa Makini na Mawazo yako. 

Awazavyo mtu moyoni mwake ndivyo alivyo,  Kile unachokiamini ndicho unachokiishi.  iko njia ionekanayo sawa machoni pa mtu lakini mwisho wake ni njia za mauti.

Mawazo mabaya huharibu tabia njema. badili mtazamo wako. Ukianza kuwaza vibaya, utaanza kusema vibaya, Ukianza kusema vibaya, utaanza kutenda vibaya.

5.Kumbatia Uhuru Ulionao Sasa.

Badala ya kuanza kujihurumia  kwa sababu tu ya upweke ulionao, Jaribu  kutafuta watu   au mtu wa kumuonyesha upendo. Unaweza kuwatembelea Yatima, Wagonjwa, Wajane, Wafungwa, Wazee wasiojiweza. Fanya kazi za kutosha nyumbani mwako, hata zile ambazo huwa unaona ngumu, kazi za kutumia akili nyingi.

Jaribu kufurahia kila kitu unachokifanya , wala huhitaji mtu wa kukusapoti kwenye maamuzi yako.

6.Itambue Hali Uliyonayo Sasa.

Huenda unahisi kuwa umekuwa hivyo kwa sababu ya  mazingira uliyopo sasa. kumbuka kuwa  maisha hubadilika hasa kama ulikuwa ukitegemea akili yako bila kuwa na Mungu.  Hata mwili wa mtu hubadilika , sura hubadilika, kutoka utoto kwenda uzee.

7.Endelea Kujitengeneza Kuwa Mtu Bora.

Mara nyingi unapojisikia kutengwa ni kutokana na kuwa mbali na Mungu. Mtazamo wako uko tofauti na jinsi Mungu anavyokuwazia. Mungu anakuwazia Mema , lajini wewe Unajiwazia mabaya. umeumbwa kwa mfano wa Mungu , Ishi  tabia za Mungu, Changanoto zako zote zitakwisha.

8.Usisahau Kuwa Muda Ni Mali

Unapokuwa unawaza sana ndipo upweke unapokuja na msongo wa mawazo  , kujilaumu pasipo sababu, hutaki kujisamehe wala kusamehe watu. unabeba watu, matokeo yake  magonjwa yanakufuata. Komboa wakati . Usiache wakati wako upotelee kwenye  hisia mbaya. Hizo hisia zako zinaiba Muda.  Waefeso 5:16. mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

9.Kumbuka Kila Kitu Hutokea  Kwa Kusudi Fulani.

Hakuna jambo linakuja kwa bahati mbaya. Inawezekana ni kwa sababu ya kujifunza kutokana na makosa au Ulikaribisha mwenyewe matatizo, kama ulipanda mabaya lazima utavuna. chochote upandacho utavuna.

Kanuni ni moja, bali yoyote mtakayo mtendewe na watu nanyi watendeeni vivyo hivyo.

10.Kumbuka wewe sio Mtu Wa Kwanza Kukutana na Hali Kama Hii.

Ni kawaida kujihisi kuwa ni wewe tu unapitia changamoto hio, kwa kuangalia watu kwa nje, huwezi kujua jinsi gani watu wanaficha  hisia zao. si kila mtu unayemuona  yuko sawa, kuna wengine wanatembea wamekwisha kufa ndani yao.

Jaribu kuongea na mtu ambaye unamwamini ,  utagundua  maumivu aliyonayo , huenda ni mara  tatu yako.  utabaki unashangaa, lakini ni kujifunza.

Wazo la Mwisho. 

Acha kujiona mpweke, acha kulalamika, kunyoshea watu vidole, Naamini kabisa kuwa hivi vitu vinaumiza , lakini yupo Mungu anaweza yote, ni wewe Kumtafuta kwa bidii na kumuomba   na kumuita wakati wa changamoto kama hio, atakusikiliza.

Pamoja na yote hayo, Endapo unapitia hali kama hio jitahidi kuingia kwenye TOBA. Toba ni kuomba msaada kwa Mungu, ya kwamba umenyoosha mikono  huwezi , unamuhitaji Mungu.  Soma neno  la Mungu, likae kwa wingi ndani yako.

Tunda la roho  likae ndani yako, Upendo, Furaha Amani, Utu wema, Fadhili, Uaminifu, Upole, Uvumilivu na Kiasi

Soma kitabu cha Zaburi.  soma Mithali kila siku kulingana na tarehe.

Kama unahitaji ushauri  , maelekezo  zaidi   toa maoni yako, mashwali yako  hapo chini.

Subscribe

Previous Wakati Mzazi Apatapo Mwenza Mpya
Next Wakati Unapofika Wa Kubaki Mwenyewe, Ni Kwa Ajili Ya Kujiboresha

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.