MAOMBI YA UKOMBOZI WA NAFSI


prayer3 MAOMBI YA UKOMBOZI WA NAFSI

Ufalme wa Mungu hupatikana kwa nguvu na wenye nguvu wauteka.  Omba usiku na asubuhi ili uweze kuona matokeo haraka.

1.BABA  MUNGU KATIKA JINA LA YESU NAKWENDA KINYUME LEO NA MAWAKALA WA KUZIMU WALIOKAMATIA NAFSI YANGU, KWA DAMU YA YESU NAIACHILIA HURU NAFSI YANGU  ITUMIKE KWA AJILI YA BWANA. ZABURI 142:7

2.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NINAMREJESHA LEO MTU WANGU WA MBINGUNI KOKOTE ALIKOSHIKILIWA KWA DAMU YA YESU KRISTO. 1COR 15:45,46, 47.

3.KWA DAMU YA YESU NINAYEYUSHA VIFUNGO VYOTE VILIVYOSHIKILIA NAFSI  YANGU NA KUVICHOMA MOTO WA ROHO MTAKATIFU.  ZABURI 147:7

4.BABA KATIKA JINA LA YESU NINATAMKA KOKOTE NAFSI YANGU ILIKOZUILIWA ACHILIA SASA KWA DAMU YA YESU. AYUBU 33:18

5.KATIKA JINA LA YESU KOKOTE  NAFSI YANGU ILIKOWEKWA  KATIKA SHIMO NA KUANGAMIZWA, NATAMKA  KUACHILIWA HURU SASA KWA MOTO WA ROHO MTAKATIFU. AYUBU 33:22

6.BABA KATIKA JINA LA YESU NATAMKA UKOMBOZI WA NAFSI YANGU NA KUWA HAI SASA KATIKA NURU YA YESU KRISTO. AYUBU 33:38

7.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO KOKOTE WALIKOTEGA NAFSI  YANGU IINGIE SHIMONI , NAIKOMBOA SASA NA KUWAANGAMIZA MAWAKALA WOTE  WANAOCHEZEA NAFSI YANGU KWA MOTO WA ROHO MTAKATIFU. ZABURI 35

8.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NATAMKA AKILI NJEMA  KUANZIA SASA  NA NAFSI YANGU IMTUMAINIE  BWANA KWA MOYO WANGU WOTE KATIKA UFALME WA MUNGU. MITHALI 3:4,5

9.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NATAMKA KUWA NAFSI YANGU IWE NA AKILI YA KRISTO KWA DAMU YA YESU. 1COR2:16

10.KWA DAMU YA YESU KRISTO NIPE AKILI YENYE UBORA  KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YANGU. DANIEL 6:3

11.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NIWEZESHE KUFUNGUA MACHO YANGU KIROHO NIWEZE KUONA FUMBO ZA IBILISI ANAZONIJILIA NAZO KUTEGA NAFSI YANGU. WAEFESO1:18

12.BABA KATIKA JINA LA YESU  ASANTE KWA KUOPOA  NAFSI YANGU WAKATI WOTE KWA MAANA FADHILI ZAKO NI ZA MILELE. ZABURI 86:13

13.BABA KATIKA JINA LA YESU NAOMBA NEEMA  YA MUNGU KUIANGAMIZA NA  KUIKANA NAFSI YANGU KWA AJILI YA UFALME WA MUNGU. LUKA 9:24

14.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYEJITOA MSALABANI ADHIHIRIKE KATIKA NAFSI YANGU SASA. WAGALATIA 2:20

15.BABA KATIKA JINA LA YESU NAACHILIA DAMU YA YESU  KUBADILISHA  NIA YANGU KWA AJILI YAKE. WARUMI 12:2

16.BABA KATIKA JINA LA YESU, MAWAKALA WOTE WA SHETANI ACHILIA HISIA ZANGU KWA JINA LA YESU. ZABURI 119:11

17.KWA DAMU YA YESU MAWAKALA WALETA GIZA NA TAMAA MBAYA KATIKA  FIKRA  ZANGU NAWAKANYAGA KUWA MAJIVU KWA DAMU YA YESU NA HAWARUHUSIWI KUNIDHURU TENA  KWA JINA LA YESU. LUKA 10:19

18.MASHETANI AINA YA MAJINI MAHABA  MAIMUNA  AINA YA MAJOKA MLIOKAMATA NAFSI YANGU LEO NAKUANGAMIZA KWA MOTO WA ROHO MTAKATIFU UWE MAJIVU KWA JINA LA YESU KRISTO.

19.KWA JINA LA YESU KOKOTE UTASHI WANGU ULIKOSHIKILIWA ACHIA KWA JINA LA YESU.

20.BABA KATIKA JINA LA YESU NAWEKA AGANO NA MACHO YANGU LEO, MACHO YANGU YASIRUHUSU TAMAA ZA DHAMBI KWA DAMU YA YESU KRISTO. AYUBU 31:1

21.KWA DAMU YA YESU NINAWEKA ,MALAIKA WA NIDHAMU KATIKA MACHO YANGU NISIZINI NAFSINI MWANGU KATIKA JINA LA YESU  KRISTO. MATHAYO 5:28

22.BABA KATIKA JINA LA YESU NINAKATAA NAFSI YANGU KUSHIKILIWA KOKOTE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO, KWENYE NDOTO KUPITIA  MAJINI NAYACHOMA NA KUYATEKETEZA KWA MOTO  WA ROHO MTAKATIFU. KUTOKA 15:19

23.BABA KATIKA JINA LA YESU, NIPE NEEMA YA KUJIFUNZA NENO LAKO LIJAE KWA WINGI  NAFSINI MWANGU. WAGALATIA 3:16

24.BABA KATIKA JINA LA YESU  KUPITIA NENO LA MUNGU LICHOME NA KUTENGANISHA  NAFSI YANGU NA ROHO ZOTE ZA KUZIMU  KWA DAMU YA YESU KRISTO. WAEBRANIA 4:12

25.BABA KATIKA JINA LA YESU, FANYA HARAKA UJE KUIOKOA NAFSI YANGU KATIKA KILA AINA  YA MITEGO YA YULE MWOVU. ZABURI 22:19

26.BABA KATIKA JINA LA YESU NINAKOMBOA NAFSI YANGU  KATIKA JERAHA LOLOTE MAISHANI MWANGU KWA DAMU YA YESU. YEREMIA 30:17

27.BABA KATIKA JINA LA YESU NAFUNGA MINYORORO ADUI WOTE WA NAFSI YANGU WASIWE NA FURAHA KWA DAMU YA YESU. MARKO 3:27

28.BABA KATIKA JINA LA YESU NATAMKA UWEPO WA MUNGU NDANI YA NAFSI YANGU WAKATI WOTE, KUSIWE NA YEYOTE KATIKA ULIMWENGU WOWOTE KUSIMAMA MBELE YA NAFSI YANGU  NA MAAMUZI YANGU  ROHO MTAKATIFU  ANIONGOZE  WAKATI WOTE KWA DAMU YA YESU KRISTO. JOSHUA 1:5

29.MUNGU BABA NAKUSHUKURU KWA KUFANIKISHA  NAFSI YANGU , KILA NENO LAKO NIPE NEEMA YA KUTII AGIZO LAKO NA KUISHI KATIKA NENO LAKO. 3YOHANA 1:2

30.BABA KATIKA JINA LA YESU  FUNGUA NAFSI YANGU NIWEZE KUONA VIZURI MAAGIZO  NA MAELEKEZO  YA KIROHO KWA DAMU YA YESU. YEREMIA 1:12

31.BABA KATIKA JINA LA YESU KUPITIA  FUNGUO ZA KIROHO NILIZOKABIDHIWA , NAFUNGA MILANGO YOTE YA ADUI KATIKA NAFSI YANGU  NA WALA HAKUNA AFUNGUAYE NA  KUFUNGUA ROHO YA UFAHAMU NA AKILI NJEMA KATIKA NAFSI YANGU WALA HAKUNA AFUNGAYE KATIKA JINA LA YESU NA KWA DAMU YA YESU. UFUNUO 3:7

32.BABA KATIKA JINA LA YESU NIFUNGUE MACHO YANGU YA KIROHO NIWEZE KUONGOZA NAFSI YANGU KATIKA HALI YA KIUNGU  WAEFESO 1:18

33.BABA KATIKA JINA LA YESU NASHUKURU KWA KUWA NAFSI YANGU INAFURAHI KUJIUNGANISHA NA FAHARI YA KRISTO BWANA WETU . WAFILIPI 3:3

34.BABA KATIKA JINA LA YESU  NASHUKURU KWA KUWA NAFSI YANGU IMESHINDA VITA VIZURI  VYA ULIMWEWNGHU WA ROHO. WAFILIPI 6:12

35.BABA KATIKA JINA LA YESU NAKUSHUKURU KWA KUWA AKILI YANGU IMEKOMBOLEWA KUIJUA KWELI YAKO  KWA KUSOMA NENO NA  KUWA NA IMANI  KWAKO PEKE YAKO. YOHANA 8:32

36.NAKUSHUKURU BABA WA MBINGU NA NCHI KWA KUWA NAFSI YANGU ITAFIKIRI MAMBO MEMA WAKATI WOTE. WAFILIPI 4:4

37.BABA KATIKA JINA LA YESU ASANTE KWA TUNDA LA ROHO LINALODHIHIRIKA KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YANGU SASA WAKATI WOTE. WAGALATIA 5:22, 23.

38.BABA KATIKA JINA LA YESU , NASHUKURU KWA MWONGOZO WA KIUNGU KATIKA KUTUMIA MUDA WANGU VIZURI KWA KAZI YAKO KWA DAMU YA YESU KRISTO. WAEFESO 5:16

39.NAKUSHUKURU BABA KWA JINA LA YESU NAFSI YANGU IPO NDANI YA  YESU , YA KALE YAMEPITA , NAANZA UPYA KATIKA JINA LA YESU. 2COR 5:17

40.BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NIPATIE MOYO MPYA NA KUFANYA JAMBO JIPYA MAISHANI MWANGU, MGEUKO MPYA WA KIUNGU KATIKA UFALME WA MUNGU. ISAYA 43:18,19

41.BABA KATIKA JINA LA YESU, KAMA MAGHARIBI ILIVYO MBALI NA MASHARIKI, WEKA NAFSI YANGU MBALI NA DHAMBI NA KULALAMIKA KWA DAMU YA YESU. ZABURI 103:3

42.BABA KATIKA JINA LA YESU, NIEPUSHE NAFSI YANGU NA KUHUZUNIKA NYAKATI HIZI ZA MWISHO, NIPE UWEZO WA AKILI KUTHUBUTU KATIKA KUFIKIRI NA KUWA NA KAZI YA MIKONO YANGU UTAKAYOIBARIKI. KAZI YA MSHAHARA SIO FUNGU LANGU MAISHANI MWANGU KWA DAMU YA YESU. ISAYA 19:10

BABA KATIKA JINA LA YESU, NAKUSHUKURU KWA MALAIKA WA AKILI WATAKAOKUWA WANANITEMBELEA KILA WAKATI KUNIPATIA ROHO YA UFAHAMU  KWA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI. DANIEL9:22

AMEN.

subscribe.

Previous Fomula Ya Maisha. Ni Muhimu
Next Mistari 27 Ya Neno La Mungu, Kila Mwanamke Anayehitaji Upendo, Uhakika Na Nguvu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.