Masharti 10 Ya Mafanikio Katika Biashara Na Maisha.


Kiwango cha Imani ni kufanya kitu. Ni lazima kuchagua imani ambayo unaitaka kufanikiwa nayo.  Imani ya Nuru au Ya Giza.

ed302b3b-46d4-4c34-b919-80e4bdc23be1-1024x683 Masharti 10 Ya Mafanikio Katika Biashara Na Maisha.Masharti yanakuza imani ya mtu. Kumbuka kuwa Vigezo na masharti lazima yazingatiwe.

1.Kusoma Neno La Mungu.

Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya  Unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo, kwa maana wakati u karibu.

Umeumbwa kwa neno lazima usome neno. mwili  unafanya kazi na neno la Mungu. Neno la Mungu ni Hekima ya Mungu. Neno la Mungu ni Maarifa ya Mungu.

August_Speedreading_700x400 Masharti 10 Ya Mafanikio Katika Biashara Na Maisha.2.Kuandika Neno la Mungu.

Unapoandika neno la Mungu unaweka Agano na Mungu wako.  Mungu ni Mungu wa records. alimwambia Habakuki , iandike njozi uifanye iwe wazi sana katika vibao.Ili aisomae apate kuisoma kama maji, maana njozi hii bado kwa wakati ulioamuriwa.

Haiwezekani vitu vingine unaandika lakini neno la Mungu huandiki. unaenda kanisani au kwenye semina bila dayari na kalamu ni mbaya sana . Unaweza ukawa na simu kubwa, nyumba kubwa, gari zuri,  na pesa za kutosha lakini huna Biblia na wala huna dayari nzuri ya kuandikia neno la Mungu , bado hueleweki , hayo mafanikio yako ni ya kitambo kidogo sana.

3.Kwenda Kwenye Nyumba ya ibada.

Nyumba ya Ibada ni jukwaa la kupatia taarifa sahihi.Sehemu zingine utapata taarifa za siasa, mpira, kubeti, drafti na mengine. Huwezi kupata taarifa sahihi  bar.

Mfalme Daudi alisema  Hakika siku moja katika nyua zako  ni bora kuliko siku alfu.Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu kuliko kukaa katika hema ya waovu.

Neno moja nimelitaka kwa bwana , nalo ndilo nitakalolitafuta, nikae nyumbani  mwa Bwana siku zote za maisha yangu.

4.Kumshukuru Mungu kila baada ya dakika 60

Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, na wenye nguvu ndio wanaouteka. Daudi alimsifu Mungu mara saba kwa siku, wewe unamsifu mara ngapi?  Daudi alikuwa analalama na kuugua  kwa Mungu mara tatu, asubuhi, jioni na adhuhuri mpaka Mungu akaisikia sauti yake. wewe unalalama na kuugua mara ngapi.Familia ya Kingdom Business tunamshukuru Mungu kila baada ya dakika 60. Je wewe unamshukuru Mungu mara ngapi?

Ukimkumbuka Mungu, atakufundisha na kukupatia faida ya kazi yako, biashara yako, ndoa yako na watoto wako na wote wanaokuzunguka mtakuwa salama.

5.Amini Kazi Za Yesu.

Waliotengeneza meli, boti na vingine, waliamini kazi za Yesu , waliamini kuwa Yesu alitembea juu ya maji.

Waliotengeneza Hospitali, waliamini kazi za Yesu, Yesu aliponya wagonjwa, viziwi, viwete,  vipofu waliweza kuona.

Walianzisha shule waliamini kazi  za Yesu, Yesu alikuwa akifundisha na kufungua watu akili zao, alikuwa anawaonea huruma watu ambao hawana maarifa, akawafundisha maarifa .

Kitakachokufungua ni mikono yako. Mungu anabariki kazi ya mikono yako.

6.Kazi Ya Adamu.

Kazi ya Adamu ni kutunza mazingira. Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu , akamweka katika bustani ya Edeni  ailime na kuitunza. Leo hii wanaume wanaishia kwenye mikeka. Wanabeti, wanataka bahati nasibu, hawataki kufanya kazi. Mwanaume anasifiwa kazi sio kubeti, sio tatu mzuka.

Hayo mafanikio ya bahati nasibu hayadumu. halafu sio lengo la Mungu wewe  kutokufanya kazi. muombe Mungu kazi. Wanaume wengi wanamuomba Mungu awape mke mwema, wakati huo huo hajui hata kutumia muda   wake mwenyewe, halafu anaongeza muda wa mtu mwingine. Acha ujinga huo. Mke ni msaidizi  wa maono yako. kama huna maono wewe unaoa ili kupata raha, au ni muoga wa kulala peke yako. Kumbuka kuwa wanaume wenye akili  wanaoa ili  kupata mtu wa kumsaidia kwenye kazi yake sio sex , wala sio kufua na kupika.  Wanawake kuweni makini sana na wanaume wa namna hii, mtatembea makanisani  , kufunga sana  , kwa ajili ya kuombea wanaume ambao hawataki kutekeleza majukumu nambayo Mungu aliwapa. Usitake kubeba mizigo ya mtu. msubiri Mungu  akupe mume mwenye maono.

7.Utoaji .

Chanzo cha kutoa ni Mungu . Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu , hata akamtoa mwana wake wa pekee , ili kila mtu amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.

Mungu anampenda mtu anayetoa kwa moyo mkunjufu, naye huwajaza kwa neema na wingi ili kuwa na riziki za kila namna kila siku. Lakini apandaye haba atavuna haba, apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. apandacho mtu ndicho atakachovuna.

8.TOBA.

Tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia. Omba rehema kila wakati, mwanadamu ana tabia ya kuwaza maovu kila wakati. mawazo yake mara nyingi ni mabaya. Tubu. Mungu anakusamehe maovu yako yote na kukuponya na magonjwa yako yote.

9.Nidhamu Ya Muda |Hekima ya muda.

Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda, sio kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye Hekima, Mkiukomboa wakati , kwa maana zamani hizi ni za uovu. Una masaa 24 lakini hutumii muda vizuri, Muombe Mungu hekima ya muda.

Mungu amekupa wewe wachungaji wampendezao moyo wake, watakaowalisha maarifa na ufahamu. Jifunze matumizi ya muda. Muda ni mali. Siku utaanza kuthamini muda , ndipo siku ambayo utaanza kuthamini muda wako.

10.Pigana Vita Vizuri Vya Roho Ya Pesa.

Misingi ikiharibika mwenye haki wangu atafanya nini?  Mwenye haki anatakiwa aishi kwa imani.  Lakini kama unasitasita huwezi kufanikiwa. Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atampenda huyu na kushikamana na huyu. huwezi kumtumikia Mungu na mali .

Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda pesa. ambayo wengine hali wakiitamani hio wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu makali.

Bali utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na Haki yake na mengine yote mtazidishiwa.

Subscribe.

Previous Fahamu Mbinu 5 Za Kumwabudu Mungu?
Next Kuwa Single Sio Laana Wala Ugonjwa , Twende Tuone.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.