MASWALI 10 KAMWE HUPASWI KUMUULIZA MWENZA WAKO


unhappy-black-couple-2 MASWALI 10 KAMWE HUPASWI KUMUULIZA MWENZA WAKO

Makala nyingi   zinazungumzia  kitu gani  kizuri cha kumwambia mpenzi wako , na watu wengi wanaepuka  kitu kisichofaa kumwambia mpenzi wake. Ingawa hizi zote zinasaidia, na ni za undani sana,  lakini kuna maswali muhimu kamwe hutakiwi kumuuliza mwenza wako

Kama wote wawili mnaepuka haya maswali, basi mahusiano yenu  yatakuwa mazuri na kama  unapenda kuuliza  haya maswali , mahusiano yenu yatakuwa yamekamilishwa na usanii zaidi kuliko kawaida.

1.Una Matatizo Gani? Kwa Nini Kila Mara Unafanya Hivyo?

Sio vizuri kumuwazia vibaya au  kumlaumu kwa kumuona mtupu  mwenza wako. Hio yote unafanya kumlaumu  na kumtenga , unafikiri unambadilisha tabia kumbe ndio unazidi kumtenga mbali na wewe.

Badala ya kumshambulia utu wake kwa kile usichopenda, mshirikishe kile kitu usichokipenda  na jinsi unavyojisikia  wakati anapofanya kitu kama hicho , unawea kujaribu kutengeneza na kupata baadhi ya vitu  vilivyo muhimu kwako.

Kwa mfano, tuseme hivi, anapenda perfume  yenye harufu kali, au pengine hupenda kuacha wazi tube ya dawa ya mswaki kila siku, au chakula anachopika hukipendi, au anachelewa kuamka. Badala ya kusema una matatizo gani? Kwa nini kila siku unafanya hivyo? Unaweza kusema hivi,  mpenzi,  unaweza kubadili aina ya perfume yako, au unaweza kupika aina nyingine ya chakula, au unaweza ukawa unaamka mapema ?kwa sababu nakujali sana  wangu.

Halafu, ukiona anafuata jinsi ulivyotaka, jisikie furaha kwa kumjali na fanya iwe furaha kwake pia. Mkumbatie na kumbusu

Na kumwambia kuwa ulijua ni vitu vidogo , lakini nimefurahishwa sana. Mwenza wako anapojisikia kukubalika  kwako,  huhitaji kufanya zaidi ya hapo ulipotaka afanye.

2.Kwa Nini Hufanyi Kama Ninavyokuambia?

Lawama sio mapenzi,  huleta hali ya kukosa matumaini , chuki, mashaka, na utengano katika mahusiano.sio tu madhara ,  haifai kabisa pia.

Unapoona watu wanakosa amani katika maisha yao ujue wamekuwa wakilaumiwa sana. Watu mara nyingi hubadilika kwa sababu wanajisikia  vibaya  na wameumizwa ndani yao .kwa wakati huo, hujikuta wanabeba  vitu ndani yao ,  kwa njia zao nyingine mpya, usiwe hivyo mtu wa kumfanya mwenza wako awe na hali kama hio. Kuna njia zingine za kutengeneza  athari kama hizo

Hata kama umechukizwa na mwenza wako , lenga kwanza kuchukua jukumu la hisia zako mwenyewe, fikra, na matendo , chukua kama  maulizo, badala ya kuzidi  kuwaza  kuwa mwenza wako anafanya sivyo, badilisha  mawazo hayo na uanze kuwaza  jinsi gani utaboresha mahusiano yako.

Mara unapopata majibu , umetulia na uko sahihi kwenye hali hio yote, mkaribie mwenza wako kwa uwazi, mawasiliano ya wazi na ushirikiane nae  ili kupata  majibu  ya kuwafanya wote muwe na furaha.

3.& 4’’.Kwa Nini Wewe Ni Msumbufu, Mvivu, Usie Na Shukrani, Mchoyo?’’Kwa Nini Usiwe  Mtu Bora, Na Mwema?

Unapokuwa umekasirika ,umechukizwa na jambo, usimshambulie mwenza wako,haisaidii. Uko pamoja nao, yuko na wewe,  package nzima kwako, kama mko pamoja ,ina maana mnafanana kwa baadhi ya  mambo.

Kama unataka sifa za mwenza wako kuboreka, inaanzia kwako jinsi unavyowasiliana nae. Mawasiliano mazuri  ni yale ya ukweli na uwazi.

Kujielezea ukweli na uwazi jinsi unavyopenda na jinsi unavyojisikia, bila ya kutumia lawama, zarau, au madai. Wakati mwenza wako anapoongea , lenga kupokea  jinsi alivyo na jinsi anavyopenda bila ya  kusikia lawama , madai au dharau.

Aina hii ya mawasiliano inahusiana na uwazi,ukweli, na uelewa  unaokuza mahusiano.

5.Kwa Nini Huwezi Kupumzika Tu?

Kama mwenza wako  yuko katika kupambana na kukimbia majibu, hawezi kutulia kwa kulazimisha. Kusisitiza, kitu kinachomkwaza. Vinginevyo angeweza kutulia.kuna mambo yanayomfanya asitulie na kupumzika.

Njia nzuri ya kumsaidia  ili aweze kupumzika  ni kutafuta kuelewa. Kwanza unatakiwa kuelewa kitu kabla  hujaanza kubadilisha, mara nyingi uelewa ndio unaohitajika.

Ukiwa wazi , mpole na muhitaji wa kuelewa kuhusu  kitu kinachoendelea kwa mwenza wako, hio ni hatua nzuri. Mnapoanza kuongea pamoja  katika hali hio  iliotokea, mtaweza kufanikiwa.

6.Unataka Kuachana Na Mimi?

Kutumia hili neno kila mnapokuwa kwenye mabishano fulani , mara nyingi huonekana kama kutishia mtu. Watu wengi wanaouliza haya maswali , wao ndio hutaka kuvunja mahusiano, lakini hutaka wasionekane kuwa wanahitaji hilo. Huanza kutishia wenza wao ili  waanze wao kumbe yeye ndio mwenye kutaka kuvunja.

Kama unataka kuvunja mahusiano , uwe wazi kuliongelea na mwenza wako ,  na uwe  mpole  na uulize kwa upole, na kama itaonekana  ataumia kwa kitendo hicho, anza kuchukua hatua taratibu ili akuelewe, ongea nae wakati kila mtu yuko sawa.

Na kama kweli unaogopa mwenza wako anapokuwa anataka kuvunja mahusiano, mwambie tu  mpenzi naogopa sana. Mwambie mchukue muda kidogo ili utulie baada ya kusikia hayo. Mara utakapoona uko sawa muulize,  unajisikiaje sasa? Unataka  nini? Au unahitaji nini katika mahusiano yetu?

Unapouliza hayo maswali bila ya njia ya vitisho,  unampa mwenza wako kufikiria jibu . kama kweli huyo mwenza wako anataka kuvunja mahusiano au la, anaweza kusema kama alitaka hivyo,  kuuliza haya maswali kwa utulivu na upole kwa uwazi  inaleta urafiki wa kimapenzi  katika mahusiano.

7.Una Uhakika Unataka Kuwa Na Mimi?

Wakati ni muhimu kwa afya ya mahusiano kila mwenza  kumheshimu na kumfanya mwenzake awe na furaha  , kila mwenza ana wajibu wa kufanya hivyo.

Kuonyesha kuvutiwa na  mwenza wako na kuvutiwa nae ni ufunguo wa kukamilisha mahusiano.

Wakati huo huo ni vigumu kuvutiwa ili muweze kujamiiana  na mtu ambae huna uhakika . kama unataka muwe katika hali sawa unayohitaji , basi  itakuwa vigumu mwenza wako kukuheshimu na hata kukupenda.

Jibu ni kwamba kuwa na uhakika kuwa ulihitaji kuwa nae, na bado unafurahia kuwa mwenyewe, unapojisikia vizuri  kwenye hisia zako ,  itakuwa ni rahisi zaidi kwako kuwa na uwazi wa akili kuwa huyo ulie nae  mnaweza kuwa mnafanana  baadhi ya mambo na unakubaliana nae.

8.& 9.’’Naweza Kukuamini’’?/’’Unaniambia Ukweli?’

Kuuliza haya maswali hatua tupu kamwe si mawazo mazuri. Kitu kimoja, kitamweka mwenza wako kwenye hali ya kujilinda kwa haraka sana. Kwa kitu kingine hutaweza kuamini majibu utakayopewa.

Hii ni kwa sababu kama huna uhakika wa kumwamini mtu ,  kisha muulize kama  utawaamini ama  sio vinginevyo utachanganyinikiwa.

Inapokuja watu kuwa na wivu  na kutochukua mahusiano, ni rahisi sana,  kumwamini mwenza wako ama kutomwamini. Kama unamwamini mwenza wako, funga mdomo wako. Kama  humwamini   fanya uwezalo  ili kuachana nae.

Haina haja ya kumuuliza maswali ya mitego.

Haya, inakuaje kama unamwamini na bado anakudanganya hata hivyo? Kisha mwamini hio siku na ipo siku utapata ukweli. Kutokuwa mkweli kwao  haiwezi kuficha ukweli wao  siku zote.siri Itakuja kuvumbuka tu . Na kwa siku hio ndipo utakuwa na maamuzi.

10.Kama Ulijua Utanifanya Nisiwe Na Utulivu , Kwa Nini Ulileta  Haya?

Mahusiano mazuri huwa hayatulizwi na  kuepukana na hali iliopo.  Hutulizwa na watu wawili walio wazi na wakweli kwa kusudi la kujenga mahusiano  ya urafiki wa kimapenzi na kukamilishana .

Ili mahusiano yako yadumu  unahitaji  ukubali kuongea kuhusu vitu vigumu  ambavyo havileti utulivu mnapokuwa mnaongea.

Ili kwenye mahusiano kuwe na utulivu inabidi kila mtu kujishusha   kwa ajili ya kuelewana. Ni changamoto kubwa kujishusha, lakini huo ndio ukweli. Ina maana kwamba  inapokuja hali ya sisi  kutopenda  kuona  zaidi, kama woga wetu wenyewe,  wasiwasi, na kukosa usalama.

Ni kama zawadi  kama ugumu, ingawa.

Kujua nini hasa kinaendelea ndani  ya uwazi na udadisi, ina  maana kuwa  hakuna mahusiano yenye  kuendelea  na hakuna maisha yanayoendelea

Kwa hio acha kuuliza maswali ya mtego, na uwe muwazi kwa mwenzi wako , pia jielezee hisia zako kwa mwenzako .kama kuna mambo huyapendi weka mezani, na ueleze nini unakipenda kwa mapenzi  nawe utaeleweka.

Toa maoni yako.

Previous UNATAKA KUANZA KUTAFAKARI? JARIBU HII.
Next MLO WA SIRI WA WAJAPANI WA KUPUNGUZA UZITO

8 Comments

 1. Avatar
  November 6, 2016
  Reply

  Ila ki2 k1 naomba nijue hv nikwann mwanamke ukimuhuliza swali gum kwenye cm akujibu au km kukujbu atajbu kwa kujiamin tofaut na ukiwa nae karbu

  • Avatar
   November 9, 2016
   Reply

   Rahim sawli lako ni zuri, naomba kukujibu hivi. Mara nyingi wanawake majibu yao huo ni kinyume cha kile unachouliza. mfano mdogo tu . wanawake huwa nataka sitaki. huo ndio ukweli. kukujibu kwa ujasiri akiwa mbali, hamaanishi kitu chochote. Lakini mwanamke makini hawezi kukujibu swali ambalo lina utata . atasubiri mkionana atakujibu.

 2. Avatar
  Eric
  June 24, 2017
  Reply

  Naomba niulize. Kuna msichana mwingine ukimusalimia kujua khari take yeye badala ya kujueleza japo kwa ufupi anajumuisha jibu lake kwa neno moja tu.mfano Jana alikuwa anaumwa ukimuuliza aaubuhi take ili ujuwe maendeleo yake anaweza kusema *sijambo”,nipo,mungu mwema n.k no kwanini asielezee?

  • Avatar
   June 24, 2017
   Reply

   Eric. Wanawake wengi huwa hatuwezi kujielezea hisia zetu, usimlaumu, Inawezekana anakuhitaji Uwepo wako, anahitaji kukuona , kukukumbatia, kuongea na wewe karibu yake sio kwenye simu. Na hasa kama alikuwa ni mgonjwa na hujaenda kumuona. hio pia ni mbinu ya kukutaka uende, lakini kwa sababu ya ugumu wenu wanaume kuelewa ataendelea kukujibu kwa mkato hivyo. Kwa hio nenda kamuone kama ni mpenzi wako au mchumba wako atajisikia vizuri. Inawezekana haumwi ila anakujaribu kama utachukua hatua gani.

 3. Avatar
  Ellyclassic19
  August 2, 2017
  Reply

  Utamjuaje mwenzie kuwa yy ndo chaguo sahh?

 4. Avatar
  August 3, 2017
  Reply

  Ellylassic19 , Kujua kuwa mwenzio ni chaguo sahihi, mtu ambaye utaishi kwa maisha yako yote yaliobaki. Ni rahisi, Utaona tu kwa jinsi ambavyo atakusaidia kukua kiakili, kiroho na kihisia. utafanya vitu ambavyo hutaweza kufanya kwa mtu yeyote. Utakubali tofauti yake na yeye atafanya hivyo. Utakuwa unapata hisia hata bila ya kuonana naye, furaha yako, mafanikio, huzuni zako ni zake pi. Utamkubali, utampenda, utamuheshimu na utamwelewa na yeye atakuwa hivyo kama wewe.
  Malengo yenu yatakuwa sawa. Mtaheshimiana. Familia na marafiki wataona kitu unachokiona kwake. Hakutakuwepo drama.Utakuwa unatatua matatizo kwa wepesi sana.Hutayafukuzia mahusiano, yatakuwepo kwako.Na utajisikia vizuri unapokuwepo karibu yake, wengi husema unajisikia upo nyumbani. Uaminifu utakuwepo na Utaona Ukweli . vitu ambavyo ni muhimu sana katika mahusiano ndio hivyo. Natumaini itakusaidia.

 5. Avatar
  Dat Said
  April 3, 2018
  Reply

  Habari, vipi ikiwa mtu huyo hukumuamini na ikatokea mmeachana lakini tayari mna mtoto lakini uwepo wake bado unakuumiza utafanyaje kuachana na hisia ulizonazo juu yake?

  • Avatar
   April 7, 2018
   Reply

   Habari nzuri Dat Said, Ikiwa mna mtoto tayari na hamko pamoja, Endelea kuonyesha upendo kwake japo mmeachana , Acha kujilaumu kwa kilichotokea, mshukuru Mungu kwa kila jambo. Ukiwa unajilaumu au kujihukumu , kwa kosa ambalo lilishapita , hutaweza kuwa na Amani, utasikia maumivu kila unapomuona hasa kama wewe ndio uliyesababisha mkaachana . Njia nzuri na rahiusi ya kuepuka maumivu ni kuonyesha Upendo kwa mtu anayekuumiza bila ya kuhesabia kitu. Jitahidi kutokukaa bila ya kufanya kitu , kila wakati ratiba yako ijae, Umemaliza kazi , tafuta mahali kajifunze kitu kipya hata kama ni kigumu. Tumia Akili kufikiri sio moyo wako. tafuta semina mbali mbali hudhuria, soma vitabu mbalimbali vya maendeleo sio vya mapenzi. Hakikisha hukai bila ya kufanya kitu, Masaa 24 yajaze vizuri. Nakupa mwezi mmoja tu utakuwa ni mtu mpya kabisa kimawazo , mtazamo. na vitendo vyako. Mungu akusaidie.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.