MBINGU INAPOKUWA KIMYA: THAMANI YA MAOMBI HUJIBIWA


faith-1024x768-1024x768 MBINGU INAPOKUWA KIMYA: THAMANI YA MAOMBI HUJIBIWA

Maombi ni zaidi ya kufika mbali kuliko kupokea Neema.

Watu wengi humwomba Mungu  kwa kumshukuru kwa ajili ya baraka, kuwaondoa kwenye masikitiko na  kwenye magumu, Kuongea nae, kumwambia vitu ili kuepukana na  matatizo mbalimbali.

Sababu kubwa ya maombi ni  kutafuta ulinzi,  kumshukuru,  kutaka msamaha na kuomba msaada wa uponyaji au kuumia.

Ingawa maombi mengine huwa yanachukuliwa  kutoka kwenye vyanzo , kama kurudia maneno ya Zaburi au ujumbe wowote waliopata, Wengi hutumia maneno yao badala ya kufuatia ya  vitabuni. Wengi huomba  vitu—Neema, ulinzi, uponyaji, mafanikio, ulinzi miujiza na msamaha.

Wakristo  huamini kupitia maombi walioomba,  kwa kutumia ahadi za Mungu kama , Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona , bisheni nanyi mtafunguliwa.Wapo ambao hawaamini, na wapo ambao wana imani ndogo, na wengine  wanasema hakuna Mungu.

2546252 MBINGU INAPOKUWA KIMYA: THAMANI YA MAOMBI HUJIBIWA

Asilimia kubwa ya wakristo huamini na kupokea majibu ya maombi yao, Na ni asilimia ndogo tu ndio hawaamini. Na wengi hupata majibu sahihi kutokana na maombi walioomba.

Kwa nini dua nyingi zinakubaliwa na zingine hazikubaliwa zaidi ya wigo wa kisaikolojia. Ingawa , misingi ya tabia inaweza kuwa  ya kueleweka  kwa imani na tabia ya maombi.Haishangazi pale unapoona watu wanaoamini maombi huendelea kuomba kwa ajili ya mafanikio.Lakini  ni nini athari ya wale ambao majibu yao hayajajibiwa?

Kuna mtu alisema kuwa nimeomba kwa zaidi ya miezi sita mfululizo kila siku kwa ajili ya mgonjwa , lakini hali yake  ilizidi kuwa mbaya, kwa hio nilianza kuomba kidogo na kwa vitu tofauti.Wakati viungo vyake viliposhindwa kufanya kazi niliacha kabisa kuomba vyote.

Majibu yasipojibiwa  yanaweza kumfanya mtu kujisikia kama mksaji,  hakustahili  kupokea Neema ya Mungu, mwingine anaweza kufikiria kuwa hakuomba vya kutosha au hakuomba mara nyingi au hakuomba kwa maneno sahihi.Ndio maana watu wanaona ni bora kurudia maneno ya vitabuni sehemu , kwa sababu  hawatagundua kushindwa kwao  kwa matokeo ya udhaifu wa sifa ya maneno ya kwao wenyewe.

Kutumia maneno ya utawala wa utakatifu  ni njia ya kuepuka kupunguza  kujilaumu.

Namaz1 MBINGU INAPOKUWA KIMYA: THAMANI YA MAOMBI HUJIBIWA

Ingawa watu wengi huona kama Mungu hayupo  kwa sababu ya kukosekana kwa majibu waliotarajia, Hukata tamaa ya maombi. Lakini wengine huendelea kama kawaida   kutokana na mitazamo yao ya kimila, huendelea na kazi zao  na imani yao.

Kuna wengine ambao tangu udogo wao wamekuta imani hio na huendelea kuomba kama kawaida . lakini kukutana na mafunzo mapya ya maombi , sio kuomba kwa kawaida yao ya siku zote, inaweza kumletea  hisia za wasiwasi , kujilaumu, upweke, kutengwa, au kupoteza ulinzi aliokuwa nao.

Kwa hio hata kama mtu  haamini tena  katika maombi ya ufanisi, lakini akawa hana  tabia ya kishirikina na akawa anatenda yalio mema,Mungu atamsikiliza kutokana na matendo yake.

Kisaikolojia , kwa yule ambae aliomba kwa ajili ya kuponywa mgonjwa wake , ilitakiwa aendelee kuamini kuwa ugonjwa umeondoka hata kama alikuwa anaona bado upo, Katika kuomba na kuendelea na matibabu majibu yangekuja , Na yeye angeanza kujisikia kuwa amepona kutokana na kufarijiwa na ndugu, kuamini ni kukubali , faraja ya kihisia, kupata maana  ya kuteseka  .

Watu wengi huanza kujilaumu kwa kufikiria  tofauti,  Nimeshindwa kwa sababu sikuomba kwa usahihi, nimetenda dhambi, sikuanza  kuomba msamaha kwanza , sikuwa na utakatifu. , Mungu hajibu maombi.

Kwa sasa wengi wameanza kutambua kuwa suluhisho la matatizo ni kuomba kisaikolojia  na sio kimwili. Kuwa na imani na kufahamu kuwa Mungu yupo, Badala ya kuendelea kujilaumu , njia bora ni kukubali , kumpenda, na kufikiria mazuri . kutunza  na kujengauhusiano na Mungu, Kujua kuwa yupo ,Mungu wa uponyaji, wa ulinzi , wa kutupigania ,  wa kutuokoa,  wa kujibu maombi  wa kutusaidia na kutuongoza.

Maneno ya Mungu hayawezi kuvunjika kati yake na mwanadamu , lakini ni kwa imani tu, kumwamini . maombi ndio  yanayokuunganisha na Mungu

trust-and-obey-2-1 MBINGU INAPOKUWA KIMYA: THAMANI YA MAOMBI HUJIBIWA

 

Kama umependa hii makala washirikishe wengi wajifunze.

Previous JIWEKE VIZURI UWEZE KUVUTIA MAHUSIANO YEYOTE
Next ACHA KUTUMIA MAKEUP NA UTAONA KITAKACHOTOKEA

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.