MBINU ZA KUONGEA NA MTU KWA MARA YA KWANZA UNAPOKUTANA NAE:


 

two-worlds-apartff1 MBINU ZA KUONGEA NA MTU KWA MARA YA KWANZA UNAPOKUTANA NAE:

Sio peke yako, kuna watu wengi wanapata taabu sana wanapotaka kuongea na watu ambao ni wageni kwao,  au pengine ni wafanyakazi wenzako , au marafiki. maongezi huwa ni shida . hasa kwa wale  wanaume wanapotaka kutongoza mwanamke kwa mara ya kwanza.

Zipo mbinu ambazo sio ngumu  ni rahisi zitakusaidia  wakati unapoona aibu ya kuongea. unaposikia woga .

1.Tumia mawasiliano ya macho.

Unapohisi sio kawaida kwa mara ya kwanza tumia macho yako kuwasiliana nao ili watambue kuwa unawahitaji. kwa mwanamume kutumia macho kwa ajili ya kutaka mwanamke aelewe kuwa anamuhitaji ni rahisi  .macho yatajulisha kuwa unawaalika kwa hatua  nyingine.

images-8 MBINU ZA KUONGEA NA MTU KWA MARA YA KWANZA UNAPOKUTANA NAE:

unaweza kuongea maneno , lakini  maneno peke yake hayatoshi. Sasa basi ,unapotumia macho yako , usiyafumbefumbe wala kuangalia pembeni, mawasiliano ya macho yanakutambulisha vizuri wewe. maneno yako yaendane na macho, pia sauti yako iwe ya chini

Ukiona unapata woga, jaribu kuangalia juu kwa muda kidogo kuliko kawaida ili kuendelea kukamilisha mwendelezo  wa nia yako. utaona utajisikia vizuri na kuendelea kuwa na ujasiri wa kuongea.

2.Dhihirisha woga kidogo.

Ukitambua kuwa hauko vizuri kichwani mwako  na  hujui kitafuatia nini cha kuongea, onyesha  hio hali kwa huyo mtu unaeongea nae. je utajisikiaje endapo mtu atasema kwako kwa hali hio inayokupata wewe,  utamuhukumu?  au utampenda kwa kuwa amekuwa mkweli na utakubaliana nae tu.

Lakini pia kuna watu wenye uzoefu wa kutumia njia hii, na usipokuwa makini hutaonyesha maana kwa kuwa  utaonekana unaforge ili upate unachohitaji.

3.Ukubali ukimya.

Ukimya ni mama wa hofu, woga, wasiwasi na kukosa ujasiri. pamoja na kwamba mila zingine huona kuwa mtu akikaa kimya ni dalili ya  tatizo , endapo utaachia kicheko. na ukipata ujasiri wa kukaa kimya basi utapata muda wa  kukusanya  maneno sahihi ya kuongea na yatakuwa ya ukweli. na mara zote  unapotaka kuongea maneno yenye akili tulia kwanza.

4.Kitu cha kufanya  endapo simu itapigwa.

Una ndugu na una marafiki  ambao wakati wowote wanaweza kupiga simu yako, usipende kuongea uongo mbele ya mtu ulienae, ungea ukweli kitu gani kinaendelea mahali ulipo. na unatakiwa utulie kwanza kidogo ndio ujibu . sio uanze aaaa, mmmm, niiiiiiiii.. hio ni kubabaika na kuwa mtu asie na ujasiri  na kuwa huna msimamo.

Onyesha kuwa unamthamini huyo mtu ulienae pale , ongea kwa ujasiri , niko poa niko vizuri , lete maneno , au mipango  inaendaje na mengine, hapo utaeleweka  vizuri na utaaminika.

shirikisha familia na marafiki na utoe mawazo yako.

 

Previous NJIA 7 NZURI ZA MAWASILIANO KATIKA MAHUSIANO YAKO:
Next SABABU ZA UKWELI 5 ZA WANAWAKE KUBAKI SINGLE.

4 Comments

 1. Avatar
  magida chimija
  May 27, 2016
  Reply

  very fantastic

 2. Avatar
  June 19, 2016
  Reply

  ahsante sana kwa somo mdadaaa

 3. Avatar
  June 24, 2016
  Reply

  thank you Magda.

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.