Mistari 27 Ya Neno La Mungu, Kila Mwanamke Anayehitaji Upendo, Uhakika Na Nguvu


tmp_26453-abeautifulblackwomansmiling117890343 Mistari 27 Ya Neno La Mungu, Kila Mwanamke Anayehitaji Upendo, Uhakika Na Nguvu

Kuna wanawake ambao hupenda watu wawathibitishe , wawapende ili wajisikie kuwa na nguvu,  Leo nataka ufahamu kuwa hakuna mtu ambaye ataweza kukuthibitisha au kukupenda  na kuwa na nguvu kama Mungu awezavyo.

Ondoa wazo hilo kwa watu. weka wazo lako kwa Mungu utaona hivyo vitu unavyotaka kupata vitakuja kwa urahisi kwa ajili yako mwanamke.

1.Mungu yu katikati yake , hautatetemeshwa, Mungu atakusaidia asubuhi na mapema. Zaburi 46:5

2.Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake, anaucheka wakati ujao. Mithali 31:25

3.Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumainia , nami nimesaidiwa , basi moyo wangu unashangilia na kwa wimbo wangu nitamshukuru. zaburi 26:7

4.Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi , kwa kuwa kristo alikufa kwa ajili  yetu. Warumi 5:8

5.Je si mimi niliyekuamuru uwe hodari? na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike, kwa kuwa Bwana Mungu wako  yu pamoja nawe kila uendako. Joshua 1:9

6.Hufumbua kinywa chake kwa hekima na sheria ya wema i katika ulimi wake. mithali 31:26

7.Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote; Nitasimulia matendo yako yote ya ajabu .Zaburi 9:1

8.Msijisumbue kwa neno lolote , bali kwa kila neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika kristo. wafilipi 4:6.8

Hatimaye ndugu zangu mambo yeyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya staha, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema, ukiwemo wema wo wote ikiwepo sifa nzuri yeyote, yatakafarini hayo. Wafilipi 4:6,7,8

Mithali 3:5,6maxresdefault-1024x576 Mistari 27 Ya Neno La Mungu, Kila Mwanamke Anayehitaji Upendo, Uhakika Na Nguvu9.Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo ,na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si  mimi , bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 1Cor 15:10

10.Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. katika njia zako mkiri yeye  naye atanyoosha mapito yako. Mithali 3:5,6

11.Naye ni heri aliyesadiki ; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana. Luka 1:45

12.Nitakushukuru kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu  ya kutisha. Zaburi 149:14

13.Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. 1Cor 16:14

14.Kujipamba kwenu , kusiwe kujipamba kwa nje , yaani kusuka nywele, , kujitia dhahabu na kuvalia mavazi , bali kuwe utu wa moyoni  usioonekana katika mapambo yasioharibika yaani , roho ya upole na utulivu, iliyo na thamani kuu mbele za Mungu. 1PETRO 3:3,4

15.Je si mimi na kuwa Bwana Mungu wako  yu pamoja nawe kila uendako. Joshua 1:9

16.Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, kupita mawimbi ya bahari yaumukayo, Bwana aliye juu ndiye mwenye ukuu. Zaburi 93:4

17.Walakini ni nani ajuaye , kwama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo? Esta 4 14b

18.Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka  .Wakolosai 2:10

19.Upendeleo hudanganya , na uzuri ni ubatili, bali mwanamke amchaye Bwana , ndiye atakayesifiwa .Mithali 31:30

20.Maana Mungu hakutupa roho ya woga , bali ya nguvu  na ya upendo na ya moyo wa kiasi.. 2Timoth 1:7

21.Unifanye kusikia fadhili zako asubuhi, kwa maana nimekutumainia wewe, unijulishe njia nitakayoiendea, kwa maana nakuinulia nafsi yangu. Zaburi 143:8

22. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu , wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Warumi 5:6

23.Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi , asema Bwana , ni mawazo ya amani , wala si ya mabaya , kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.Yeremia 29:11

24.Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya. Kutoka 14:14

25.Hapatakuwa mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako. kama nilivyokuwa pamoja na Musa , ndivyo nitakavyokuwa  pamoja na wewe sitakupungukia  wala sitakuachja. Joshua 1:5

26.Mpenzi wangu u mzuri pia pia, wala ndani yako hamna  ila. WIMBO ULIO BORA 4:7

27.Basi tangu sasa ninyi si wageni  wala wapitaji ,bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni . katika yeye jengo lote linaungamanishwa  na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana . Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja  kuwa maskani ya Mungu  katika roho. waefeso 2:19-22

Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko tuyaombayo  au tuyawazayo , kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu .

Mwanamke wa thamani.

Subscribe.

 

Previous MAOMBI YA UKOMBOZI WA NAFSI
Next Wakati Mzazi Apatapo Mwenza Mpya

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.